Dereva wa UDART anahatarisha usalama wa abiria

pererge

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2012
Posts
571
Reaction score
206
Leo tarehe 14 basi la mwendo kasi namba ya usajili T120DGW leo muda wa saa kumi na mbili jioni likitokea Kimara kwenda Kivukoni tulipofika fire akafungua mlango wa mbele tu, abiria waliokuwa nyuma walipoona milango haifunguliwi wakaenda mbele ambapo mlango umefunguliwa, mmoja akawahi kutoka mwingine kabla hajatoa mlango ukafungwa ikawa inambana akarudi ndani gari likaomdoka, wakashukia DIT, walikuwa ni vijana wawili.

DIT napo ni hivyo hivyo ufunguaji wa milango, wengine wakapitishwa wakashukia Kisutu. Kisutu napo mchezo ni huohuo, jamaa mmoja almanusura abanwe na milango wakati akiingia, akamuuliza dereva inakuwaje, huyu dereva akatoka kwenu kiti chake kuja kuzozana na huyu abiri.

Nawaomba wahusika wa UDART mumpe elimu huyu dereva ili awe dereva bora.
 
Walianza vizuri ila kwa sasa Customer care imeshuka, wastaarabu wako wachache madereva. Management wafanyie kazi changamoto hiyo lakini pia waweke namba za simu watu wapige ofisini kwa malalamiko kama hayo.
 
Bado kuna tatizo... sijui lini kutakuwa na jambo la asilimia 100 %
 
Haya magari yanaweza kufunguliwa juu ili upepo uingie km ilivyo gari za mkoa...inashangaza kuona gari imeshona hata pa kupumulia hakuna ila madereva hawajali japo kufungua kule juu ili kuongeza hewa. Madereva wa mwendokasi wengi wanafanya kazi kukomoa na sio km watoa huduma
 
Watakuwa hawajapewa chao hivyo hasira wanazihamishia kwa abiria.

Back
Top Bottom