Dereva wa Uber mwenye uzoefu, natafuta gari la kufanyia kazi

Duh! Kaka me ni mtu na family najielewa (educated) Hayo mambo huwa yapo kweli kwa vijana wasio na majukumu uthamin wa kazi unakuwa mdogo
 
Ma boss njooni muokoe jahazi nitakuwa mwaminifu au nitawasalimia kwa jina la jamhuri ya uaminifu ili kazi iendelee
 
Hii ni kweli hawa madereva wengi pasua kichwa. Mimi nimeexperience (madereva wa 4) Sasa hivi mtu kama sio mlokole simpi gari. Maana angalau walokole watasumbua hesabu ila gari yako watatunza.

Dereva mmoja alichomoa rim sport kauza akaweka marim yakawaida, radio kauza na AC compressor katoa kauza kaeka mbovu. Nikamueka ndani changombe ndugu wamekuja kulia ikabidi nimwachie kibinadamu.

Kabla hawajapewa kazi wanakuwa na maneno ya matumaini sana, ipite miezi kadhaa sasa
 
Sehemu ya tangazo langu limekuwa na replies za watu wa lawama kuliko msaada wa tangazo husika.

Hii na sawa mwanamke aliyetendwa na mwanaume mmoja half akaja na majumui kuwa wanaume wote ni mbwa''
Sasa ulitumwa utembee nao wote"

Anyway just jokes tu. Ni mtu ninaejielewa kama una gari tufanye kazi kuharibu nyuzi za watu siyo ustaarabu.
 
Mimi gari nnalo nipo dom natafuta account nijiongezee kipato hasa weekends
1.Leseni c1, c2, c3 & C
2.Hati ya tabia njema
3.Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
4. DOCUMENTS za gari zenye usajili wa biashara.
(I) insuarence
(ii) car regstration card.
(iii) latra

HAPO UTAKUWA UMEKAMILISHA
 
Tunapozungumzia online taxi hawa ni uber, bolt, qtaxi, liltle ride nk .
Nimekuwa ndani ya kazi hizi za usafirishaji wa abiria kwa njia ya mtandao sasa yapata miaka miwili na nusu.
Changamoto mbalimbali ya kazi hizi nazifahamu dereva fanya yote ila hesabu ya Boss ndio ulinzi wa kibarua chako hili nimeliona wengi hupishana na waajili wao hakuna sababu kubwa km hesabu japo
Kuna waajili nao wanachangamoto zao kwa madereva mf ninayeachananae ni suala la kila ijumaa, jumanos na jpili nimkabidhi gari nilifuate tena j pili jioni na kwa uzoefu wangu ktk kazi hizi hizo ndio siku rasmi ambazo kuna nafasi ya kupata chochote.

Nisiandike mengi ila chonde Waungwana km kuna mmiliki wa chombo (gari) anahitaji dereva nipo tayari kufanyanae kazi kwa uaminifu na weledi wa hali ya juu iwe mkataba au hesabu ya kawaida nipo tayar anipe uhuru sitomuangusha kwa sababu za hovyo hovyo kama vijana wengine wasio na majukumu wanaendesha kwa tafsir ya kujishkiza.

Mawasiliano: 0789702863.

NJOO TUINGIZE KIPATO.
 
Hakuna hata aliyejitokeza hofu yangu ni madereva wa awali huenda waliwafanyia vitu vibaya hawa watu.
 
Back
Top Bottom