oruguyo
Senior Member
- Jul 28, 2012
- 132
- 37
Mpendwa Kilaza,
Nakuandikia nikiwa ndani ya basi lenye mwendo usiomithilika, machozi yanatutoka kwa upepo mkali unaopenya kwenye madirisha huku vumbi na harufu za jasho zikiumiza pua zetu.
Ni matumaini yangu u buheri wa afya tele. Mimi si mzima, hofu na mashaka ya kuiona kesho yangu imekuwa kubwa mno. Safari tuendayo hatuna uhakika kama tutafika salama kwani mwendo kasi wa dereva wetu hausemeleki.
Juzi tu wakati tukitoka Kijiji cha Kumi na tano dereva wa gari alibadilika na kuingia dereva mpya ambaye kwa kelele na uchachafya wa baadhi ya abiria walisema ni lazima yeye atuendeshe kuelekea kule Kijiji cha ishirini.
Safari ilianza taratibu baada ya yeye kuamua kukagua siti zote kama zina abiria na kugundua wapo watu waliosimama ilihali wengine siti waliziweka mifurushi ya mihogo wakidai ni watu. Baada ya kuweka mafuta na ule Mngurumo kulia gari ilianza kuondoka kwa kasi. Baadhi yetu tukaanza kupiga kelele kwamba mwendo ni mkali sana na hivyo apunguze. Baadhi ya abiria walianza kututukana na kutukashifu kisa tu dereva aliyeendesha gari lile walitoka naye kijiji kimoja.
Kilio chetu kiligeuka masengenyo na kuambiwa kama tunaona gari inakimbia sana tujinyonge, Kilaza, chakula garini hakuna, dereva amegoma kupunguza kasi walau tushuke tuchimbe dawa. Hapangiwi.
Barabara tunayopita Shanisa ni mbovu, imejaa misitu na milio ya simba na ngurumo za radi. Mvua kali inayonyesha si kitu kwa dereva na hakuna trafiki polisi yoyote wa kumsimamisha. Muda unavyozidi kwenda hata wale ndugu zake wa ukoo mmoja wanaanza kunyamaza na hofu zinawatanda. Harufu Kali ya tairi ikiungua inasikika lakini bado wapo wanaomvisha kilemba cha ubwana na kumtonya eti azidishe kasi.
Nakuandikia kukupa urithi wa mali kidogo niliyonayo ambayo kama sitapona kwenye safari hii basi utoke huko ng'ambo ulipo uje kuifata nyumbani. Naandika haya kwa kujificha kwakuwa kile apigaye kelele kuhusu spidi ya gari kwa sasa wanamchukua na kumtupa kwenye buti la gari.
Tunatia huruma sana, nyuso zimekosa upako na mashavu yametudorora kama utumbo wa mbuzi. Baadhi ya ndugu zake wa ukoo mmoja na makenika wake aliopanda nao kituoni pale wameanza kuhofia pia iwapo hata rejeta kama ina maji. Baadhi ya mafundi alioingia nao hawaeleweki nyuso zao na wapo abiria wanaolalamika kwamba wengine sio mafundi kweli, wamefoji ustadi, lakini nani anajali Kilaza.
Matairi yameota matege, taa zimekwaa makengeza na nafsi zimevimba kwa mdondo wa mawazo tuliyo nayo. Matapishi yamelifanya gari lizidi kunuka kwa ndani lakini kila kelele tunayopaza ni ama dereva au makenika wake wengine alioingia nao watakukamata na kukupiga ngoto.
Nina nyumba Kijijini Kolo pembeni kabisa ya nyumba ya Mzee Shite yule wa BA. Ufikapo muulizie Mije kama atakuwa amenusurika safarini, mwambie upendeleo wa nafsi zalimu hujitwika kinyesi cha moto giza litandapo, lakini harufu na joto halitamuacha. Mwambie akupatie fungua nawe uitwae iwe yako.
Kilaza, sikufahamu binadamu ni weusi wa nafsi na mitazamo hafifu. Kazi ya udereva aliomba kwa unyenyekevu, mathalani walikuwapo wengi, ila kwa hila na fitina Cheupe alitemwa na wa kwao na kupewa yeye, kwa spana na bisibisi akaingia na wengine wakimshangilia kwamba yeye ni simba wa nyika na kwamba amefuzu Rally. Lakini hasilani hatukutegemea mbio zilizosababisha tuache njia na kuingia kusikojulikana. Ramani yetu haikuonyesha njia hii, kadi ya gari ilionyesha namna ya uendeshaji na masharti ya kuzingatia, lakini wanatung'ong'a. Midomo imebabuka na visogo vimetoka nywele kwa upepo. Tunapokwenda siko lakini mingurumo ya simba na harufu ya tairi vinanipa wasiwasi itakuwaje kama tutaishiwa mafuta katikati ya nyika.
Niishie hapa kwakuwa hata kalamu yangu inaisha wino. Nimekupatia nyumba hiyo iwapo itatokea sifiki. Naamini lipindukapo wataikuta barua hii.
Wasalaam
Abiria.