dereva teksi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

dereva teksi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 4, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MFUNGWA anayetumikia kifungo cha miaka 11 jela, Amin Konshuma (28) jana alihukumiwa kifungo kingine cha miaka 10 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwaibia mali wanawake.

  Kifungo hicho cha jana ni cha tatu kwa Konshuma na awali alidaiwa kuwaibia kinamama mali mbalimbali wakati alipokuwa dereva teksi.Wakili wa serikali Ester Kyala alidai mbele ya Hakimu Mkazi Genivitusi Dudu kuwa Konshuma alikuwa akiwaibia wanawake baada ya kuwadanganya gari walilokodi limearibiika na wakati wakilisukuma alikuwa akiondosha gari kwa kasi ili kuwatoroka wanawake hao.

  Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Dudu alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka pamoja na utetezi wa mshtakiwa, hakuna shaka kwamba mshtakiwa huyo, alihusika katika wizi huo.

  Alisema ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo, Konshuma anapaswa kutumikia kifungo cha miaka mitano jela katika kosa la kwanza la wizi wa vitu mbalimbali zikiwemo dola za Kimarekani 200 mali ya Nuru Mohamed.Katika shtaka la pili, Konshuma alidaiwa kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 240,000 mali ya Sild Sanga.

  Hakimu Dudu alisema kwa kuzingatia umri wa mshtakiwa aliweka amri kuwa vifungo hivyo alivyohukumiwa Konshuma vitakwenda sambamba.Mshtakiwa huyo aliamriwa kulipa fedha na mali zote alizoiba wakati akiwa gerezani Amri nyingine ni akiwa gerezani au mara atakapomaliza kutumikia adhabu.

  Awali Juni 8, 2008, katika kesi namba 199, Konshuma alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na Novemba 11, 2010 katika kesi namba 100 mbele ya Hakimu Ritha Tarimo wa mahakama ya kisutu, mshtakiwa alikuhumiwa tena kifungo kingine cha miaka sita jela, hadi sasa bado anaendelea kutumikia adhabu hizo.
   
Loading...