Dereva teksi abaka mteja wake

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Dereva teksi katika Manispaa ya Iringa, Elain Mahenge (27), anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mteja wake.

Mahenge, Mkazi wa Semtema, Kihesa katika Manispaa ya Iringa, anadaiwa alikutwa akifanya kitendo hicho dhidi ya mteja wake saa 3:45 usiku.

Kitendo hicho cha ubakaji kimetokea ikiwa imepita takribani miezi miwili, tangu Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Iringa, kutoa elimu kwa wananchi wa Kihesa juu ya kuwafichua watu wanaodaiwa kufanya vitendo vya ubakaji.

Elimu hiyo ilitolewa kutokana na kuripotiwa kukithiri kwa vitendo hivyo, ikiwamo dhidi ya watoto wa kike na kuwalawiti watoto wa kiume, huku zaidi ya watu 10 wakiwa wameshakamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kujihusisha na unyama huo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita, katika eneo la Kihesa. Alisema mtuhumiwa alikutwa akimbaka mteja wake huyo, ambaye ni mkazi wa Mgololo, Mufindi mkoani Iringa.

Kakamba alisema mteja huyo alimkodi dereva huyo, baada ya kushuka kwenye gari katika kituo kikuu cha mabasi cha Iringa na kumtaka ampeleke kwenye nyumba ya kulala wageni iliyoko Kihesa.

“Inadaiwa dereva teksi huyo alimchukua stendi hapo na kwenda alikoambiwa ampeleke lakini alipofika njiani kwenye giza alisimama na kisha kumbaka binti huyo,” alisema.

Kamanda Kakamba alisema wakati dereva huyo akiendelea kufanya kitendo hicho, binti huyo alipiga kelele ambazo zilisikika na askari polisi ambao waliokuwa doria usiku huo na wakati polisi wanafika eneo la tukio tayari mtuhumiwa alikuwa ameshamaliza kufanya kitendo hicho na ndipo walipomkamata.

Alisema kuwa mtuhumiwa yuko polisi na ushahidi umeonekana pale pale kwa kuwa mazingira na hali waliyokutwa nayo dereva na binti huyo, yalidhihirisha mtuhumiwa alitenda jambo hilo bila ya huruma tena kwa mteja wake, hivyo mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakani wakati wowote kuanzia sasa.

Aidha kamanda huyo aliwataka wakazi wa mji wa Iringa na viunga vyake kupanda teksi ambazo zimesajiliwa na si kupanda teksi bubu kama aliyokuwa ameipanda msichana aliyefanyikwa unyama huo.
 
Hao walikubaliana... pesa ya guest wakaona hawana.. kheri wamalizane ndani ya gari... kukamatwa na doria ndiyo habari imepindishwa...

Ilitakiwa iwe..wakutwa wakifanya mapenzi ndani ya gari... unajua kubaka ndani ya gari kwa mazingira ya gari mziki wake mkubwa...

Lakini kama mkikutwa mmebetua seat... au mpo siti za nyuma... siyo kubaka huko...
 
Labda alitishwa na bastola feki akaamini ni ya ukweli
 
Umri wa aliebakwa naona haujatajwa. Isije kuwa walikubaliana baada ya kukamatwa binti kabadilika.
Polisi walisikia kelele. Kama wangekubaliana pasingekuwa na kelele. Na kwa kuwa alimwambia ampeleke kwenye guest house wangeenda kufanya uasherati wao huko. Huyu alimbaka. Asubiri miaka 30.
 
watu wa IRINGA inabidi wakutuna kujadili hii mada na kupata itimisho. Inasikitisha sana wadada kibao wako town wanatafuta wanaume apelekwe kifungoni
 
Tuanzie kwenye chup....i Kama imeraruriwa na nguo za mbakwaji Kama zilifinyangwa zime raruka kupitia haya ushahidi wa mazingira ututoonyesha hakukuwa na makubaliano (nguvu ilitumika) otherwise ushahidi wa one against one huwa ni mgumu kuthibitisha
 
Hao walikubaliana... pesa ya guest wakaona hawana.. kheri wamalizane ndani ya gari... kukamatwa na doria ndiyo habari imepindishwa...

Ilitakiwa iwe..wakutwa wakifanya mapenzi ndani ya gari... unajua kubaka ndani ya gari kwa mazingira ya gari mziki wake mkubwa...

Lakini kama mkikutwa mmebetua seat... au mpo siti za nyuma... siyo kubaka huko...
mkuu ulikuwepo eneo la tukio?
 
Mkuu maelezo yako yaonesha una utaalamu wa ubakaji.
 
Tuone pia tiketi ya huyo dada kua je ni kweli alitoka safari na alikua aenda wapi au iringa kafuata mini? Hawa jamaa zetu me huwa siwaamini sana coz ni wazee wa
........

Back
Top Bottom