Dereva mwingine wa pikipiki auawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dereva mwingine wa pikipiki auawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Feb 28, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Feb 28, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KIJANA mwingine dereva wa pikipiki anayejishughulisha na kubeba abiria kupitia usafiri huo katika eneo la Kimara Suka ameuawa.

  Kijana huyo anakadiriwa kuwa na miaka kati ya 14 hadi 16 ambaye anafahamika kwa jina moja la Solo ameuawa jana majira ya usiku, wakati akiwa anampeleka mteja wake.

  Marehemu alikuwa ni dereva mwenye umri mdogo kabisa kuliko madereva wengine waliopo kituo hicho.

  Mmoja anayemfahamu marehemu wakati akizungumza na Nifahamishe alisema kuwa marehemu alikuwa ndio kwanza amemaliza darasa la saba mwaka jana na wazazi wake waliamua kumnunulia pikipiki hiyo ili aweze kujikomboa kimaisha.

  Inasemekana kuwa kama kawaida mteja alifika na kumtaka kijana huyo ampeleke sehemu husika na kijana huyo bila kujua kama ni mbaya wake alianza safari ya kumpeleka mteja wake huyo.

  Inasemekana kuwa mteja huyo alitaka ampeleke sehemu inayoitwa Golani nje kidogo ya Suka stendi.

  Ndipo mtu huyo ambaye hakuwa mwema kwake alipofika eneo ambalo aliona anaweza akafanya mauaji hayo alimtaka kijana huyo kusimamisha pikipiki.

  Inasemekana mtu huyo alitumia kisu kumuulia kijana huyo na kufanikiwa kuondoka na pikipiki hiyo.

  Baadhi ya mashuhuda walioenda eneo la tukio na kukuta maiti hiyo walisema kuwa marehemu alichomwa na kisu sehemu za kichwani na usoni na kusababisha kifo chake.

  Pia walikuta kiatu kimoja ambacho inadaiwa kuwa mtuhumiwa alikiacha baada ya zoezi la mauaji kukamilika na kuondoka na pikipiki na kusahau kiatu hicho

  Source: Nifahamishe.com
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Feb 28, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana jana nilipanda bajaj kwenda masaki dereva wa bajaj akaniambia siku hizi wanakabwa sana na vibaka ila bajaj muundo wake sio wa kiusalama ni rahisi sana mtu kuingia na kutingisha
   
 3. B

  Babuji Senior Member

  #3
  Feb 28, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania tutaendelea kuwa masikini milele
  Kila watu wanapojaribu kujikomboa wanakwamishwa
  Viongozi wetu wengine mafisadi wanatufanya tuendelee kuwa masikini
  Sisi raia nao tunaleteana wivu wa ajabu ajabu na kukwamwishana
  TUTAKUWA MASIKINI MILELEEEE
   
Loading...