Mandasi Technologies
Member
- Dec 19, 2012
- 77
- 13
Jackson Simbo anayedaiwa kumgonga kwa gari marehemu trafiki Elikiza Nko wiki iliyopita maeneo ya Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam amepandishwa kizimbani leo katika read more
Naona umeamua kuipa promo blogu yako ila ina rangi mbaya mno ibadilishe ipo kilocal sana
hivi kesi za mauaji zina dhamana? si kaua huyu?
Hiyo ni Traffic Offence sio Criminal mzee ukitaka maelezo zaidi google difference between them
Nilikuwepo eneo la tukio siku hiyo, nashangaa polisi kumpeleka mahakani kwa traffic offense, nadhani hata uelewa wao nao ni mdogo, mimi si mwana sheria lakini mtazamo wangu ni kuwa alitumia gari kwa makusudi kumwua yule polisi, hakuwa kwenye msafara, wenzake walioingilia msafara walisimamishwa na wakatii, yeye hakutii amri ya polisi akatanua pembeni na kumwua yule polisi... na sasa eti yupo nje kwa dhamana. Polisi wametendee haki polisi mwenzao aliyetangulia mbele ya hakiHiyo ni Traffic Offence sio Criminal mzee ukitaka maelezo zaidi google difference between them
Nilikuwepo eneo la tukio siku hiyo, nashangaa polisi kumpeleka mahakani kwa traffic offense, nadhani hata uelewa wao nao ni mdogo, mimi si mwana sheria lakini mtazamo wangu ni kuwa alitumia gari kwa makusudi kumwua yule polisi, hakuwa kwenye msafara, wenzake walioingilia msafara walisimamishwa na wakatii, yeye hakutii amri ya polisi akatanua pembeni na kumwua yule polisi... na sasa eti yupo nje kwa dhamana. Polisi wametendee haki polisi mwenzao aliyetangulia mbele ya haki
Inashangaza kama kuingilia msafara wa mkuu wa nchi ni kosa la kawaida la matumizi ya barabara.....
Trafic offence hapo ni kukataa kutii amri ya kusimama baada ya kusimamishwa na polisi. Na kuendesha gari kwa uzembe na kuua.
Kuingilia msafara sidhani kama ni trafic offence. Nilishawahi kuingilia msafara japo sikugonga mtu. Nilipelekwa kituoni na kupewa elimu tu. Ningepaparika kutaka kutoa rushwa nadhani wale trafic wangefanya sherehe. Waliponikamata niliwaambia twende kituoni. Niliishia kuapologise na kupewa kitabu cha usalama barabarani. System huwa tunaiharibu wenyewe.