Dereva afariki akijaribu kuvuka mto kwa gari

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Dereva mmoja mkoani Morogoro amefariki dunia wakati akijaribu kuvuka mto kwa gari wakati mvua kubwa ikinyesha.

Dereva huyo alikuwa akivuka mto huo ukiwa umefurika maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.

Kikosi cha jeshi la polisi linafanya uokozi wa kuopoa mwili na gari lililozama katika mto ambapo mashuhuda wa tukio hilo wameiomba serikali kuweka kingo za vyuma pembeni mwa daraja hilo ili kuzuia ajali za kutumbukia magari.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tukio hilo ni la kusikitisha ambapo amewatahadharisha wananchi mkoani humo kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini wakati wanapovuka mito kutokana na mito mingi kujaa maji.
 
Watu wengine ni vichwa maji, hana tofauti na mtu anayeamua kujinyonga, poleni wafiwa
 
Hii habari inanikumbusha ajali kama hii iliyotokea mwaka 1987 baada ya dereva mmoja kulazimisha kuvuka mto fulani njia ya kutokea mkoa wa Mara kuelekea Arusha na gari jipya aina ya Landrover 110 kwa kujiaminisha kuwa gari yake isingeweza kuzama. Enzi hizo 110 ndiyo kama V8 kwa Sasa.

Hapo kwenye mto alikuta magari kibao yameegeshwa pembeni yakisubiri maji yapungue ndipo yavuke lakini yeye akiwa na hiyo 110 alijiaminisha na kuwaambia madereva wenzake "mimi kwa hii 110 yangu tunapita". Matokeo yake yeye dereva na abiria wake karibia kumi tena wote wakiwa ni wa familia moja ya kigogo mmoja wa idara ya ardhi mkoani Mwanza walipoteza maisha yao katika ajali hiyo.

Ilivyosimuliwa ni kwamba sehemu kubwa ya abiria hao walikuwa ni watoto waliokuwa wanawasindikiza wakubwa wao waliokuwa wanarudi shule mjini Arusha baada ya kuwa wamemaliza likizo yao iliyoambatana na sherehe za sikukuu ya krismasi nyumbani kwao mjini Mwanza.
 
Marehem alikuwa ana wito wa Kwao,aisee we unaaminije mto.
Hizi sifa hizi,haya marehem rest in mto.
Maana utakuta wengine wenzao wapo wanasuburia mto upungue ili waone kingo na surface kama ipo salama,ila yeye kwa kuona ni mjanja akaona ni super controller anaweza kupenya ili baadae ajisifu,hatima yake anapata sifa moja tu kwamba Marehem amekufa kwa uzembe wake.
 
Badili heading ya Uzi wako "Beth" sema hivi " mjinga mmoja afariki dunia akijaribu kuvuka daraja lisiloonekana kwa kufunikwa na Maji huku akiendesha gari morogoro"

Apumzike kwa aonavyo Mungu.
 
Hii habari inanikumbusha ajali kama hii iliyotokea mwaka 1987 baada ya dereva mmoja kulazimisha kuvuka mto fulani njia ya kutokea mkoa wa Mara kuelekea Arusha na gari jipya aina ya Landrover 110 kwa kujiaminisha kuwa gari yake isingeweza kuzama. Enzi hizo 110 ndiyo kama V8 kwa Sasa.

Hapo kwenye mto alikuta magari kibao yameegeshwa pembeni yakisubiri maji yapungue ndipo yavuke lakini yeye akiwa na hiyo 110 alijiaminisha na kuwaambia madereva wenzake "mimi kwa hii 110 yangu tunapita". Matokeo yake yeye dereva na abiria wake karibia kumi tena wote wakiwa ni wa familia moja ya kigogo mmoja wa idara ya ardhi mkoani Mwanza walipoteza maisha yao katika ajali hiyo.

Ilivyosimuliwa ni kwamba sehemu kubwa ya abiria hao walikuwa ni watoto waliokuwa wanawasindikiza wakubwa wao waliokuwa wanarudi shule mjini Arusha baada ya kuwa wamemaliza likizo yao iliyoambatana na sherehe za sikukuu ya krismasi nyumbani kwao mjini Mwanza.
Hiyo habari nilihadithiwa na mmoja wa wahusika,alikuwa ni dereva alietumwa kuwarudisha watoto shule ambao kama sikosei ni wa familia moja.
 
Mnakumbuka ajali ya air shengena mto ziggy handeni 1996?mto ulifurika na kingo za daraja zikawa hazionekani lakini ca ajabu dereva akalazimisha kupita na watu 76 walipoteza maisha
 
Hiyo habari nilihadithiwa na mmoja wa wahusika,alikuwa ni dereva alietumwa kuwarudisha watoto shule ambao kama sikosei ni wa familia moja.
Ndivyo ilivyotokea mkuu. Kulikuwa na watoto wakubwa waliokuwa wasoma Arusha na wakawa wamerudi kwao Mwanza kwa ajili ya likizo ya mwisho wa mwaka.

Baada ya likizo na sikukuu za Christmas na mwaka mpya wale watoto wa shule wakatakiwa kurudi shule. Wadogo zao wakataka wawasindikize wale wakubwa wanaporudi shule. Sasa kwa vile baba yao alikuwa ni mtu mwenye wadhifa na usafiri wa bure ulikuwepo (yaani ile landrover 110 mpya ya ofisini kwake) hakuona tatizo kuwaruhusu wale watoto wawasindikize ndugu zao na watu wengine wakubwa ili wakishawafikisha wanafunzi shuleni warudi Mwanza na gari hiyo hiyo. Ajali ilipotokea ndiyo wote wakapoteza maisha.

Siku zilivyozidi kukatika zikavuma habari kwamba yule dereva alikuwa kapona baada ya kufanikiwa kuogelea na kwamba alikuwa amekimbilia mafichoni nchini Kenya kukwepa mkono wa sheria na pia hasira za ndugu wa marehemu. Lakini pengine hili la dereva kupona na kwenda mafichoni ilikuwa ni uzushi tu.
 
Na ajali hizi miaka ya karibuni zimekuwa nyingi sana,mwaka jana sikumbuki vizuri nahisi ilikuwa Dodoma jamaa aliteketeza watu saba akiwa na Land Cruiser Hardtop,mwingine na gari aina ya Nadia akafa dereva pekeyake wengine Mungu saidia waliokoka,mwaka huu pia ilitokea tena ajali akafa msaidizi wa IGP,mkewe na watoto wao wawili..mie nadhani ni uzembe na ili kuzuia madhara haya inatakiwa popote penye mto ikionekana limit ya ujazo wa maji kuzidi kiwango basi waende police kuwapa raia elimu na atakaekaidi achukuliwe hatua.
 
beth naamini wewe ni jornalist kutokana na baadhi ya taarifa unazoziweka hapa.Lakini mbona hujaandika hiyo ajali imetokea sehemu gani na mto gani hapo Morogoro.
 
Mnakumbuka ajali ya air shengena mto ziggy handeni 1996?mto ulifurika na kingo za daraja zikawa hazionekani lakini ca ajabu dereva akalazimisha kupita na watu 76 walipoteza maisha
Hii inatokana na madereva vichwa ngumu kujiaminisha ujinga hata pale pasipofaa,maji ya mto mtu uyasikie tu yaani ni one mistake two goal,kipindi cha nyuma nilishuhudia mtu anasombwa na maji yaani hatua hamsini hakumaliza alibaki kama alivyozaliwa na zile shusha pandisha plus magogo hakuweza hata kupiga mbizi maana wenyeji walisema jamaa alikuwa bingwa wakuvusha watu,haya mambo ya magari ingetakiwa wawepo polisi kuweka ulinzi pale maji yanapojaa ili kuwadhiti watu kama hawa manaa ndo kazi yao.
 
RIP,

NASI TU WASAFIRI INGAWA HATUJUI NI NJIA IPI TUTAKAYOPITIA.

POLENI WAFIWA
 
Back
Top Bottom