GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,651
- 14,318
Nimegundua ana tatizo kubwa sana kisaikolojia na kiakili. Sisemi hajasoma au si msomi, hapana hilo sijasema ila inawezekana amepatwa na msongo wa mawazo kwa kiasi kikubwa sana kiasi kwamba kwa sasa hajui afanye na nini. Hajui abwekee nini ni kama mbwa kichaa anabwekea kila kitu hata kivuli. Akiona ndege angani anabweka, akiona mkia wake anabweka.
Huyu kijana mdogo ambaye alipaswa awe anatoa mawazo tunayoita madini sasa naona anakuja na kila post ya kuonesha uwezo wake una deteriorate katika kufikiri. Najiuliza amepatwa na nini? Si hali ya kawaida kuanzia kuponda vyama vingine, kuja kuanzisha chama cha ajabu ajabu na hata kusema jinsi alivyorubuniwa na CCM leo hii.
Katika akili timamu utagundua watanzania hawahitaji chama kipya, kama unabisha utanambia. Watanzania wana mahitaji mengi sana ya muhimu. Vyama vimekuja na kuondoka na vyenye nguvu vimekaa. Huyu hiki chama chake hakitaweza chukua hata jimbo moja la ubunge maana watanzania wanapata wazo kimeanzishwa na mtu ambaye ameshachanganyikiwa.
Nauliza Deo Kisandu amekula au kunywa nini? Amepatwa na nini?
--
Majibu ya Deogratius Kisandu, soma hapa
------------
Jembekillo anasema,
Nimekuwa nikifuatilia nyuzi mbalimbali za mwanachama mwenzetu anayejiita Deogratius Kisandu ambazo nyingi zimekuwa zikionyesha kuwa analaumu watu wakubwa nchini mfano aliwahi kumlaumu January Makamba kwa kukataa kwenda kwenye sherehe yake ya kumaliza chuo kikuu. na pia huwa anatoa mada zisizo za kawaida zenye dalili za uwendawazimu. lengo langu si kumtusi mwenzetu huyu ila kumsaidia kutokana na kuguswa na dalili za matatizo yake.
Ndugu Wanachama,
Tunapozungumzia afya tunamaanisha hali ya ustawi wa mwanadamu kimwili, kiakili na kijamii. Mtu mwenye afya njema ya akili anaaminika kutengemaa katika namna anavyofikiri, anavyohisi, na anavyotambua mambo, ambayo kwa pamoja hujionyesha katika matendo yake ya kila siku.
Magonjwa ya akili ni magonjwa ambayo yanaathiri uwezo wa mtu kufikiri, kuhisi, kutambua na kutenda, na hivyo kuwa na tabia au mwenendo uliotofauti au usioendana na jamii husika kiimani, kimila, desturi, na nyanja nyingine za kijamii. Tabia hizo zinatokana na ugonjwa wa akili kuathiri ufanisi na shughuli za mtu husika (mgonjwa) au huathiri jamii nzima inayomzunguka endapo mgonjwa huyo hatopatiwa matibabu stahiki na kwa wakati muafaka. Hapa nchini kwetu wagonjwa wengi wa akili hawafiki katika vituo vya kutolea huduma za afya na badala yake kuishia kwenye tiba za jadi au kutelekezwa na kunyanyapaliwa.
Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ina idadi ya watu takriban milioni 45 na kutokana na taarifa ya afya ya akili kwa mwaka 2014/15 inaonyesha kuwa idadi ya watu 817,532 wanaugua magonjwa mbalimbali ya akili nchini, hii ni karibu asilimia 2 ya watanzania wote. Pia idadi hii ni ongezeko la wagonjwa 367,532 ukilinganisha na takwimu za mwaka 2013/14 walikuwa ni 450,000. Kati ya wagonjwa wote wa akili kwa mwaka 2014/15 wanawake ni ni 332,000 na wanaume ni 485,532. Mkoa wa Dar-Es-Salaam unaongoza kwa kuwa n awagonjwa wengi nchini ukifuatiwa n amkoa wa Dodoma na mkoa wa mwisho ni Lindi. Idadi hiyo ya wagonjwa ni wale walioweza kuhudhuria katika vituo vya kutolea huduma ya afya hapa nchini.
Magonjwa ya akili yapo ya aina nyingi na mengi huwa hayatambuliki kwa urahisi kwa jamii na hata kwa watoa huduma wa afya na hivyo wagonjwa wengi huchelewa kupata matibabu stahiki. Aidha wagonjwa wa akili wamekuwa wakibaguliwa na kunyanyaswa na jamii kutokana na imani potofu katika jamii yetu kuhusiana na sababu zinazo sababisha magonjwa ya akili pamoja na kutofahamu kuhusu matibabu ya magonjwa ya akili.
Dalili zinazoashiria magonjwa ya akili ni nyingi sana, baadhi tu ni ambazo zimegawanyika katika makundi matatu ni kama ifuatavyo:
i) Kihisia
- · Kukosa furaha kuhuzunika sana
- · Kuwa na furaha sana kupita kiasi
- · Wasiwasi na/ au woga kupita kiasina
- · Kupunguza kuongea au kutokuongea kabisa au kuongea sana kupita kiasi
- · Hasira za haraka haraka hata kufikia kupiga wengine
- · Kuwa na msongo wa mawazo
- · Kujitenga na watu na kupenda kukaa mwenyewe muda mwingi au kupenda kuwa na watu sana kuliko kawaida
- · Kutokuwa na ari ya kufanya kazi au kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja bila ya kuzikamilisha
- · Kutokuonyesha hisia yoyote usoni mwake (mf. furaha au huzuni nk)
- · Kutokujijali usafi na muonekano wake
- · Kuhisi maisha hayana thamani na kuona bora kufa kuliko kuishi na hatimaye kufikia uamuzi wa kujiua na hata kuua wengine.
ii) Kimwili
- · Mwili kukosa nguvu au kuhisi mwili una nguvu sana kupita kiasi
- · Kukosa usingizi au kulala usingizi sana kupita kiasi
- · Kukosa hamu ya kula au kuwa na hamu sana ya kula
- · Kutokutulia (kuhamanika) au kutulia sehemu moja muda mrefu bila ya kujisogeza
- · Maumivu sehemu mbalimbali za mwili kama vile kichwa, mabega, mgongo, na viungo mbalimbali ambavyo akienda hospitali vipimo havionyeshi tatizo lolote la kimwili.
- · Kukosa umakini wa shughuli zake za kila siku
- · Kusahau kwa haraka au kupoteza kumbukumbu
- · Kukosa uwezo wa kupambanua mambo kwa mitazamo tofauti
- · Kusikia sauti ambazo hazipo na kuona vitu ambavyo havipo
- · Imani ya ajabu ambazo haziendani na mila, imani au desturi za jamii yake ; kama vile yeye ni mtu maarufu, au anaamini kuwa yeye ni Nabii
- au anaamini kupokea taarifa kutoka kwenye redio au mitandao ya simu
- · Pia anaamini ana nguvu ya ziada kutoka nje ya mwili yake inayomsababishia kutenda au kuwaza mambo anayoyawaza
- · Anaamini mawazo yake yanapunguzwa au kuongezwa na watu wasiojulikana, vyombo vya habari kama vile Radio na TV kuwa vinazungumzia yeye, au vinaongea mawazo yake yeye
- · Mawazo yake hayana mtiririko unaoeleweka.
Ndugu Wanachama,
magonjwa ya akili yanaathiri hisia (mood disorders) ambayo hupelekea watu kujiua pamoja na matatizo ya jinsia (sexual dysfuctions). Magonjwa haya mara nyingi yanapoanza yanaonekana ni hali ya kawaida tu na huenda pasiwepo na jitihada yoyote ya kupata msaada wa kitabibu hadi hali itakapokuwa mbaya au kuzidiwa.
Lengo langu tushauriane jinsi ya kumuokoa ndugu yetu kwani kila siku anazidi kupost mada zenye dalili za kuongezeka matatizo ya akili kichwani mwake. ikiwezekana mods wachukue hatua dhidi yake japokuwa natambua sheria ya uhuru wa kujieleza but not to that extension
NB: kwenye maandishi yenye rangi nyekundu ndio hasa dalili za matatizo ya akili anazoonyesha Deogratius Kisandu
Jembekillo
Paka Mweusi Gizani
Zaidi kuhusu Deogratius Kisandu soma =>Deogratius Nalimi Kisandu katika ubora wake