Deo Kisandu akacha siasa

Huyu Kisandu ni msaka tonge kupitia siasa. CCM hatuhitaji watu wa dizaini hii.

mbona wewe ni mmoja wa wasakatonge wakubwa sana bhana! Nani asiyekujua humu , kwanza WASALITI , MAMLUKI NA WAZANDIKI NDIYO NGUZO YA CCM , TANGU LINI WATU KAMA HAWA WAMEKATALIWA CCM ? MFANO HALISI NI TAMBWE , KABOURU , NGAWAIYA NK .
 

Nadhani uamuzi huu una heri nawe na pia kwa manufaa ya upinzani

Kila la kheri .Pole sana
 

...tafadhali naomba kujulishwa shule utakayopangiwa kufundisha ili nimuepushe mwanangu na ujuha wa namna hii.
 
Tarehe 04/01/2013 Tulisoma kwa mbwembwe bandiko la kamanda wetu - leo ni Mwaka Mmoja tu na miezi 5 mambo yamebadilika tena: Hebu tujikumbushe tamko la kamanda wetu.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI

Ndugu wanahabari,
Mimi ninaitwa Deogratius Kisandu, nimehitimu katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa huko Lushoto (SEKUCO) nina Shahada ya Elimu Maalum, Siasa na Utawala.
Nilikuwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA katika nafasi za; Katibu wa Wilaya ya Lushoto na Katibu wa Vijana wa Mkoa wa Tanga (Bavicha).
Mwaka 2010 niligombea ubunge katika jimbo la Lushoto, nilishika nafasi ya pili kwa kupata kura 5000+ dhidi ya mgombea wa CCM aliyepata kura 14000+ .
Ndugu wanahabari,
Kwa muda mrefu nikiwa ndani ya CHADEMA, tumekuwa katika maelewano mabaya na hata pengine kujengewa chuki na fitina pale nilipojaribu kuhimiza viongozi wenzangu kufuata katiba ya Chama chetu.
Mwishoni mwa mwaka jana (2012) niliamua kujivua uanachama ndani ya CHADEMA na kuahidi kujiunga na Chama kingine.Vile vile nilisema siku hiyo nitaeleza sababu za msingi zilizonifanya nijivue uanachama na kukabidhi kadi ya Chama hicho.


1. Mnamo mwaka 2012 nilitangaza nia yangu ya kugombea urais kupitia CHADEMA. Msimamo huo umenijengea chuki na uhasama kwa viongozi wakuu wa CHADEMA akiwemo muasisi wa Chama hicho Mzee Edwin Mtei, kupinga vijana kuonesha dhamira zao.
Nimejiridhisha kwamba, CHADEMA ina watu wake inaowataka wagombee urais na hususan watu wa Kaskazini mwa nchi hii.
Yaliyonikuta mimi pia yamewahi kuwatokea marehemu Chacha Zakayo Wangwe, Zitto Zuberi Kabwe na John Magane Shibuda pale walipojaribu kuwania nafasi hiyo ndani ya Chama.
Inasikitisha sana kwa watu wanaotaka kugombea urais wanasakamwa, wale ambao hawataki kugombea na wala kutangaza kugombea urais ndiwo wanaolazimishwa kugombea nafasi hiyo.
Itakumbukwa kwamba, Dkt. Wilbroad Peter Slaa hakuwahi kujitangaza kuwa anataka kugombea urais, bali amekuwa analazimishwa kugombea urais, hata juzi Mwenyekiti wa CHADEMA ameonekana kumlazimisha Dkt. Slaa kugombea urais (2015).
2. Mnamo mwaka 2012, Dkt. Slaa ametangaza na kukiri kuwa anamiliki Kadi ya Chama Cha Mapinduzi na kwamba Kadi hiyo ililipiwa ada kwa miaka 20 hadi mwaka 2017.
Ninajua kuwa Dkt. Slaa anayo haki ya kuwa na Kadi hiyo kwa sababu aliinunua kwa fedha zake na hivyo ni mali yake.
Binafsi siridhiki na vitendo vya Dkt. Slaa, amekuwa anahamasisha watu wanaotoka CCM wamkabidhi Kadi za CCM. Je, hao nao hawakununua kwa fedha zao? Je, hawataki nao kuwa na kumbukumbu kama yeye? Bila shaka kuna siri kubwa imejificha nyuma ya pazia.
3. CHADEMA haitaki kuona vijana wanaochipukia wanakuwa na umaarufu ndani ya Chama hicho. Kwenye ziara za M4C wamekuwa wanawatumia watu wasioijua CHADEMA, wanazunguka nao Mikoani, wanawaacha vijana waliokipigania Chama hadi kikafika hapa kilipo.
Watu wanaopata nafasi nyeti ndani ya Chama hicho ni wale tu wenye udugu au uhusiano na viongozi wakuu wa Chama. Mfano mzuri ni mgawanyo wa vitu maalum vya ubunge.
Zaidi ya nusu ya viongozi wa juu wa Chama wamehakikisha ndugu zao au wake zao ndio wamepata nafasi hizo, zingine zinagawiwa kwa njia za kudhalilishana. Hivi sasa kuna mmoja wa wabunge wa viti maalum ana ujauzito wa mmoja wa viongozi wakuu wa Chama.
Ndugu wanahabari,
Yapo mambo mengi na ambayo siwezi kuyamaliza kwa leo, ila kwa ufupi nianze na hayo ili yakikanushwa ndipo nitaeleza mengine.
Baada ya kusema hayo, ninatangaza sasa rasmi kuwa, kuanzia leo tarehe 04/01/2013 nitajiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi.


SABABU ZA KUJIUNGA NA NCCR-MAGEUZI
1. Ni Chama kikongwe, waasisi na waanzilishi wa mageuzi hapa nchini. Ni Chama kilichopitia migogoro na misukosuko mingi ambacho ninaamini kimekomaa.
2. Ni chuo kizuri cha wanasiasa,watu wengi wamepitia hapa, wakafundwa na baadaye wakatamaniwa hata vyama vingine. Mifano michache ni Dkt. Masumbuko Lamwai, Dkt. Festus Limbu, Steven Wasira (CCM) na Ndesamburo, John Mnyika, Joseph R. Selasini, Chiku Obwao, Suzana Kiwanga, Profesa Mwesigwa Baregu, Mabere Marando nk.
Ninaamini kwamba, kujiunga kwangu na Chama hiki nitajifunza mambo mengi.
3. NCCR-Mageuzi ni Chama na kipimo cha demokrasia kwa vitendo. Ni Chama ambacho hakina mtu mmoja tu kwa ajili ya nafasi ya za uongozi, yeyote ana nafasi ya kugombea nafasi anayotaka na mkutano mkuu wa Chama ndio uamue nani anafaa kuwa mgombea urais.
Mfano, Mwaka 1995 Chama kilimsimamisha ndugu A.L. Mrema kugombea urais. Mwaka 2000 Chama kilimsimamisha ndugu Edith S. Lucina kugombea urais. Mwaka 2005 Dkt. E.A. S. Mvungi aligombea urais na mwaka 2010 Chama kilimsimamisha ndugu Hashim S. Rungwe aligombea urais. Hii ni tofauti na baadhi ya vyama vingine.
4. Nilipotangaza kugombea urais kupitia CHADEMA, niliwekewa mizengwe, nikajengewa chuki. Nilitangaza kugombea urais, lakini sikutangaza kwa mwaka gani, kwani mwaka 2015 umri wangu wa kikatiba wa kugombea urais hauniruhusu, nilikusudia baada ya mwaka 2015, lakini kwa CHADEMA inaonekana wana wagombea wao wa Kaskazini kwa miaka hamsini ijayo.
Ninaamini ndani ya NCCR-Mageuzi, umri wangu ukifika, mkutano mkuu ndio utaamua na siyo kiongozi mmoja.
Baada ya kusema hayo, ninaomba sasa nikabidhiwe Kadi ya NCCR-Mageuzi.


04/01/2013
D. KISANDU


 
Wapinga UKAWA ni CCM. wenye serekali 2 ni CCM na hakuna mahali popote ambapo wananchi waliposhirikishwa kutoa maoni yao kama wanahitaji serekali 2 ama laa.Cha kushangaza umewawekea wananchi maneno ili waonekane kuwa maoni ya serekali 2 ni ya wananchi wakati maoni ya wananchi ni serekali 3 hilo hata wewe mwenyewe unalitambua pamoja na CCM wote wanalitambua hilo ila kwa vile wamejitoa ufahamu wanaona maoni ya serekali 3 ni ya Waryoba.Pamoja na kwamba unazuga maelezo yako yote yamekaa ki CCM CCM.Kuzunguka kote huku usipojiangalia mwisho wake utajikwaa.
 
Dhambi ya usaliti haitawaacha wasaliti itaendelea kuwaandama mpaka kwenye mapango watakayokimbilia kujificha.
 
Hapa ndugu umechemka sana.Sababu halisi si kutelekezwa inavyoonekana maana umechanganya story nyingi hadi UKAWA ndani.Jinsi ulivyojieleza hufai kwa chama chochote labda ukalime tu sasa.
 

huyu si wa kuhurumiwa hata chembe .
 
Kwa staili hii hata ule urais uliotaka kugombea ingekuwa ni balaa, eti ukawa lazima ujumuishe wapinzani wote, duh ndo elimu yako ya chuo inavyokudanganya? Kwa kweli nimeamini mapandikizi ni mengi ndani ya upinzani! Kwa macho manne wewe ni ccm pure! Jiandae kwenda ccm kaka!
 

hawa jamaa watakuwa na historia nzito juu ya maisha yao na mtandao zitto

huko ndipo zitto alitaka kufanya mapinduzi kwa kupitia kafulila ili akimbilie kwa hiyo NCCR inalifahamu vizuri kundi la wasliti i mean kundi zitto
 
hawa jamaa watakuwa na historia nzito juu ya maisha yao na mtandao zitto

huko ndipo zitto alitaka kufanya mapinduzi kwa kupitia kafulila ili akimbilie kwa hiyo NCCR inalifahamu vizuri kundi la wasliti i mean kundi zitto

nimekuelewa aisee !
 
ACT iko na wanachama 2000 wenye kadi go na uongeze idadi ya waslaiti
 
tatizo la usaliti mwisho unakuwa peke yako pole sana heri ya upinzani kupunguza wasaliti poleni sana najua kwa akili zenu ni kurudi kwa waliowatuma au chama chenu tatizo waliowatuma kazi imeisha awana pa kuwatumia zaidi ya jukwaa na chama chenu wote mnajuana na hamini hamuaminiani sababu wote wasaliti zambi ya usaliti inawamailiza wenzako wamebaki kwenye mitandaoo tu toka walipomalizika kutumiwa kwenye majukwaaa
 
kumbe ni mwalimu huyu punguwani? sasa badala ya kwenda kufundisha alidhani siasa ndio njia ya mkato ya utajili?
.
Kama uwezo wake kwa kujenga hoja ndiyo huo hafai hata kwenda kufundisha Vijana wetu. Hakustahili hata kuwa kiongozi kwenye chama.
 


Kwaheri kapunzike salama. RIP katika siasa.

Eti mgonjwa ana pata nafasi ya kushinda mitandaoni badala ya Kitandani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…