Deni matibabu India balaa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,124
Deni matibabu India balaa
www.ippmedia.com/sw/habari/deni-matibabu-india-balaa

Januari 11, mwaka jana, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ikishirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ilitangaza masharti mapya kwa wafanyakazi na maofisa wa serikali kwenda kutibiwa nje ya nchi, ikifuta utaratibu uliokuwapo ambao ulikuwa rahisi kupata kibali cha kwenda kutibiwa ughaibuni.

Akitangaza masharti mapya siku hiyo, Msemaji wa Wizara wa Afya, Nsanchris Mwamwaja, alisema mtu atakayetaka kwenda kutibiwa nje ya nchi, atalazimika kuidhinishiwa safari yake na jopo la madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Alisema uamuzi huo umelenga kuondoa mwanya wa baadhi ya watumishi wa umma kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa maradhi ambayo yanaweza kutibiwa kirahisi katika hospitali zilizopo nchini.

Wakati serikali ikipambana kupungumza mzigo wa kugharamia matibabu ya Watanzania nje ya nchi, Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2015/16 imeonyesha kupaa kwa deni la serikali katika hospitali za rufani za India.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo ilikabidhiwa kwa Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam Machi 27 na baadaye kuwasilishwa bungeni mjini hapa Alhamisi iliyopita, hadi Juni 30, 2016, deni la serikali katika hospitali za rufani za India lilifikia Sh. bilioni 19.193.

Katika ripoti hiyo, CAG Prof. Mussa Assad, anasema, deni hilo limeongezeka kwa Sh. bilioni 2.252 kulinganishwa na lilivyokuwa Juni 30, 2015 ambapo Tanzania ilikuwa inadaiwa Sh. bilioni 16.94 na hospitali hiyo.

Katika mchanganuo wake, CAG Assad anazitaja hospitali za rufani za India zinazoidai Tanzania kuwa ni Ahmedabad Sh. bilioni 2.056, Bangalore Sh. milioni 548.323, Chennai Sh. bilioni 6.164, Madras Sh. milioni 5.274, Hyderabad Sh. bilioni 2.594 na New Delhi Sh. bilioni 7.824 zinazotengeza jumla ya Sh. bilioni 19.193.

Ripoti ya CAG kwa mwaka 2014/15 iliyowasilishwa bungeni Aprili 24, mwaka jana, ilionyesha kuwa mbali na kudaiwa Sh. bilioni 16.94 na hospitali za rufani za India, Tanzania pia ilikuwa inadaiwa Sh. milioni 448.144 kwa ajili ya malipo ya matibabu ya nje ya nchi ya maofisa wa balozi mbalimbali.

Serikali kupitia kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, imekuwa ikisisitiza kupunguza idadi ya Watanzania wanaopelekwa nje ya nchi kupata matibabu ili fedha zinazookolewa zitumike kuboresha huduma za kibingwa katika hospitali kubwa zilizopo nchini ikiwamo MNH, Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).
 
Kwa maana hio kutoka juni 30 2015 hadi juni 2016 zimetumika/kuongezeka tzs 2.2bn hapo Magu kabana?!!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa nini serekali inashindwa kuchukua wazo la kila raia kuwa na kadi ya bima? Hii ingesaidi mtu kupata matibabu kwa urahisi na kwa gharama ndogo.

Kuwe na utaratibu wa lazima kwa kila raia lazima awe na bima ya afya. Ikionekana kuwa matibabu yake yanatakiwa kufaanyika nje ya nchi basi bima ilipe gharama.

Haya mambo ya serekali kulipa gharama yana harufu ya kifisadi kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Shangaa na wewe Mkuu. Sijui kipi kilichobanwa. Juzi juzi tuliambiwa kuna mtu katumwa India akatibiwe.

Kwa maana hio kutoka juni 30 2015 hadi juni 2016 zimetumika/kuongezeka tzs 2.2bn hapo Magu kabana?!!!
 
Kwa wale wataoenda kwa fedha zao binafsi,pia wanapaswa pia kuidhinishwa na jopo la maDk wa Muhimbili?..
 
Shangaa na wewe Mkuu. Sijui kipi kilichobanwa. Juzi juzi tuliambiwa kuna mtu katumwa India akatibiwe.
Kwani average annually ilikuwa kiasi gani? Tukijua hio ndio tutajua kama kubana kumefanya kazi.
 
16 bln mbona ndogo kama serikali inalipa huku imefumba macho.....

WAlipe aise...wale wanaoheshimika watatibiwa wapi lisipolipwa????
 
Deni matibabu India balaa
www.ippmedia.com/sw/habari/deni-matibabu-india-balaa

Januari 11, mwaka jana, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ikishirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ilitangaza masharti mapya kwa wafanyakazi na maofisa wa serikali kwenda kutibiwa nje ya nchi, ikifuta utaratibu uliokuwapo ambao ulikuwa rahisi kupata kibali cha kwenda kutibiwa ughaibuni.

Akitangaza masharti mapya siku hiyo, Msemaji wa Wizara wa Afya, Nsanchris Mwamwaja, alisema mtu atakayetaka kwenda kutibiwa nje ya nchi, atalazimika kuidhinishiwa safari yake na jopo la madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Alisema uamuzi huo umelenga kuondoa mwanya wa baadhi ya watumishi wa umma kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa maradhi ambayo yanaweza kutibiwa kirahisi katika hospitali zilizopo nchini.

Wakati serikali ikipambana kupungumza mzigo wa kugharamia matibabu ya Watanzania nje ya nchi, Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2015/16 imeonyesha kupaa kwa deni la serikali katika hospitali za rufani za India.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo ilikabidhiwa kwa Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam Machi 27 na baadaye kuwasilishwa bungeni mjini hapa Alhamisi iliyopita, hadi Juni 30, 2016, deni la serikali katika hospitali za rufani za India lilifikia Sh. bilioni 19.193.

Katika ripoti hiyo, CAG Prof. Mussa Assad, anasema, deni hilo limeongezeka kwa Sh. bilioni 2.252 kulinganishwa na lilivyokuwa Juni 30, 2015 ambapo Tanzania ilikuwa inadaiwa Sh. bilioni 16.94 na hospitali hiyo.

Katika mchanganuo wake, CAG Assad anazitaja hospitali za rufani za India zinazoidai Tanzania kuwa ni Ahmedabad Sh. bilioni 2.056, Bangalore Sh. milioni 548.323, Chennai Sh. bilioni 6.164, Madras Sh. milioni 5.274, Hyderabad Sh. bilioni 2.594 na New Delhi Sh. bilioni 7.824 zinazotengeza jumla ya Sh. bilioni 19.193.

Ripoti ya CAG kwa mwaka 2014/15 iliyowasilishwa bungeni Aprili 24, mwaka jana, ilionyesha kuwa mbali na kudaiwa Sh. bilioni 16.94 na hospitali za rufani za India, Tanzania pia ilikuwa inadaiwa Sh. milioni 448.144 kwa ajili ya malipo ya matibabu ya nje ya nchi ya maofisa wa balozi mbalimbali.

Serikali kupitia kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, imekuwa ikisisitiza kupunguza idadi ya Watanzania wanaopelekwa nje ya nchi kupata matibabu ili fedha zinazookolewa zitumike kuboresha huduma za kibingwa katika hospitali kubwa zilizopo nchini ikiwamo MNH, Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Zito Kabwe na Mbatia ndiyo walioliongeza Deni zaidi walienda kutibiwa Hugo!
 
Back
Top Bottom