Deni la taifa laongezeka triolion 21 ndani ya miezi 6

Deni la taifa laongezeka triolion 21 ndani ya miezi 6

uzio usio onekana

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2019
Posts
888
Reaction score
2,804
Screenshot_20221213_084656_Chrome.jpg

My take
Jamani hii ni hatari sana na hapa ndio nimeanza kumuelewa ndugai kwamba alikuwa yupo sahihi sana. na kinacho nisikitisha zaidi hizi pesa zilizokopwa ni nyingi sana na haziendani na kilicho fanyika kwenye maisha halisi ya watanzania.
 
Single ni ile ile, tunajenga madarasa na vituo vya afya......hapo usisahau matundu ya vyoo!
 
Ehh Mwenye Enzi Mungu
Lini itakuwa enough kwa hii nchi yetu Tanzania [emoji1241]?
Tutalia hadi lini? Machozi ya Watanzania hayaja jaa kwenye kikombe chako?
Ehh Mola wangu kumbuka damu za ndugu zetu zilizo mwagika ili tukomboe Africa nzima, hiyo ni hazina tosha ya Mbinguni na Duniani!
Ehh Rabuka tuokoe hii nchi kutoka kwenye makucha ya wezi wa nchi yetu Tanzania [emoji1241]
Nasema asante kwakuwa wewe unakumbuka ahadi zako zote na ni mwaminifu na mwenye rehema na neema!
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Aamina [emoji2972]
 
Mama angekuwa anakopa halafu pesa zinakuwa na impact ktk maisha ya mwananchi wa kawaida nisingeona tatizo, kwa hali ilivyo ni kama hizo pesa wanakula viongozi (kulamba asali?!) tuu na ndio maana wananchi wa kawaida hawamuelewi kbs rais!.
 
Hivi hayo mamikopo yanaenda wapi jamani maama km tozo ama kuleta nafuu kwetu huku sitimbi hatuoni ....
 
Ni kweli lakini watanzania maskini ndio chanzo Cha dharau ZAO walamba asali.

Vitu vinapanda Bei watu kimya wanaogopa kupigwa marungu na maskini wenzao wanaolipwa Kwa Kodi ZAO.
Watoto Wa maskini wanaongizwa kwenye deni la kitumwa Huku pesa hizo zikiishia Kwa Watoto na familia za wakubwa kuneemeka na kuanzisha NGO na kula pesa za misaada na Mikopo Toka Kwa mabeberu.

Gesi ipo tele lakini wanatuambia kuwa hakuna mvua ya kuzalisha umeme.
Ziwa Nyasa, Ziwa Viktoria, Ziwa Tanganyika ,na maziwa Mengi madogo kadogo karibu Kila mkoa lakini eti mvua haijaonyesha HIVYO hakuna huduma ya Maji wanachimba visima Kwa mamilioni vinatoka Maji Miaka miwili vinakauka au miundo mbinu inaharabika .

Watu Biashara za wanyonge zinafungwa kwa kukosa umeme lakini wao wanakwenda Nje na kujilipa Mapesa Huku wenye visaluni vyao wakikosa umeme na kukosa Hata pesa ya Kununua chakula. Wao inyeshe mvua liwake Jua watakula na kuvimbiwa lakini wenye stationary au wenye karakana za kuchomea vyuma hawawezi kula Bila umeme . Hilo hawajali. Anayeona hapati kitu ahamie Burundi.
Wanasubiri Mbowe awaambie kuwa waandamane Kudai kuwa umeme ni haki Yao mana waliwapiga watu mabomu Mtwara Ili umeme Wa gesi upatikane na mgao uwe historia.

Wanaoathiriwa na mgao Wa umeme,Maji, kupanda Bei Kwa vitu, Kodi KUBWA na tozo wangeungana nchi nzima mpaka vijijini Hao watu wangekaa na kutafuta uvumbuzi Wa kudumu Bila kujali matumbo Yao tu.

Watakopa sana mana hawataki kuwaza Wala kuumiza vichwa vyao mana muda wao utapita Kwa utulivu mkubwa kutokana na woga Wa wahanga .
Walisema hakuna MTU atakayegongewa Mpango Ili adaiwe deni la Taifa. Ni dharau KUBWA.
 
pesa zilizokopwa ni nyingi sana na haziendani na kilicho fanyika kwenye maisha halisi ya watanzania.
Hawakopi ili kuja kukuvisha na kukulisha. Wanakopa ili kujenga miundombinu pamoja na kuboresha huduma.

Ningekuelewa Kama ungesema haziendani na maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom