Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Deni la matibabu ya nje kwa baadhi ya wananchi wakiwamo vigogo katika hospitali mbalimbali nchini India limeongezeka kutoka Sh17 bilioni mwaka 2013/2014 hadi kufikia Sh28 bilioni.
Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) imebainisha ongezeko hilo katika kipindi cha mwaka 2014/15 ikilinganishwa na ukaguzi uliotangulia wa 2013/14. Matibabu nje ya nchi mara nyingi hufanywa kwa viongozi wa Serikali na wengine wanaopata vibali maalumu.
Ripoti hiyo imefafanua kwa kuzitaja hospitali zinazohusika na matibabu hayo na kiwango cha deni kinachodaiwa sasa ikilinganishwa na mwaka 2013/14. Katika Hospitali ya Apollo Hyderabad ambayo kwa mwaka 2013/2014 deni lilikuwa Sh2.7 bilioni sasa inadai Sh4.8 bilioni.
Hospitali nyingine ni Apollo Chennai pia ya India ambayo mwaka 2013/2014 deni lilikuwa Sh6.6 bilioni sasa limefika Sh8.7 bilioni. Kwa hospitali ya Apollo Bangalore, mwaka 2013/2014 deni lilikuwa Sh380 milioni na mwaka 2014/2015 likapanda kufikia Sh1.2 bilioni.
Hospitali ya Apollo Ahmedabad deni lilikuwa Sh582 milioni na likapanda hadi Sh2 bilioni, wakati Hospitali ya Apollo New Delhi deni lilikuwa Sh6 bilioni na sasa limefikia Sh10 bilioni na Hospitali ya Madras Medical Mission deni lilikuwa Sh562 milioni na sasa limefika Sh1 bilioni.
Kauli ya waziri Akizungumzia madeni hayo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema kuna mikakati inafanywa ili kukabiliana nalo.
"Hivi sasa deni ni zaidi ya Sh28 bilioni, hivyo tumedhamiria kujikita katika kujenga uwezo wa ndani kwa kusimika vifaatiba vya kisasa pamoja na kuongeza idadi madaktari bingwa ili huduma zitolewe nchini,"alisema.
Alisema, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete itawezeshwa ili vyumba vyake vya upasuaji vianze kufanya kazi katika mwaka wa fedha wa 2016/2017. fedha zimetengwa pia kwa ajili ya kusimika vifaatiba katika hospitali ya magonjwa ya saratani ya Ocean Road.
Alisema wizara yake inabana matumizi yasiyo ya lazima zikiwamo safari za nje ya nchi. "Zaidi ya asilimia 90 ya safari ninazoidhinisha kuombea kibali Ikulu hazilipiwi na Serikali. Ninaamini kwa mikakati hii tunaweza kupunguza deni la wizara kwa kiasi kikubwa," alisema.
Source: Mwananchi