Demu wangu kaniacha baada ya kusoma Post zangu JF

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Huu msala umenikuta muda si mrefu, Ni demu wangu ambae nilikuwa nadate nae na tulishakuwa na malengo na Moment nzuri sana,

Amenikata stimu muda huu baada ya kunipigia simu na kuniambia kuwa hawezi tena kuwa na mimi huku analia,
Kumuuliza nini chanzo ndio akaniambia kwamba Amesoma post zangu za JF na kujua yale niliyokuwa Namficha, (sikuwahi kujua kwamba anaijua JF japo ana simu kubwa huu ni Uzembe wangu)

Nikamuuliza tena Amesomaje na Simu yangu niko nae mimi mwenyewe akanijibu kwamba "kuna kisa cha demu Alikisoma Jamii forum baada ya kuunganisha doti ndio akajua kumbe ni ni yeye aliyekuwa anaelezewa kwa sababu matukio na Story nzima yalikuwa yanamuhusu yeye kwa Asilimia 100%"

Anasema Baada ya hapo akaingia kwenye ID ya mtoa mada akapitia post zake karibia zote za Nyuma,
Mpaka ile ya kumiliki kibanda cha chipsi,pia na ile ya safari ya kwenda Mwanza kupiga mishe ndio akapata mashaka juu yangu(Baadhi ya mambo yangu huwa namueleza kama mpenzi).

Baada ya kuwa na mashaka akaanza upelelezi wake kwa siri mimi bila kujua, "sasa leo mchana alikuja hapa kibandani kwangu na kunichangamkia fresh kama hakuna kitu chochote kile amehisi akaomba Chipsi kama kawa nikamuandalia,
Mimi bila kujua akaniuliza kama kwenye simu nina credit kuna mtu anataka awasiliane nae nikampa simu aisee kumbe ndio nilipolikoroga"

Kwa mujibu wa yeye ni kwamba nilipompa simu akapekua na kukutana na JF app kwenye simu yangu akaingia chap (si mnajua password inakuwa saved) akakutana na ID yangu ndio akajirizisha kwamba ndio mimi,

Kiufupi Mtoto kanipa fact tupu nimeshindwa kukataa ila kiume nikamwambia kwamba zile story sio za kweli mi nachangamsha genge tu

Mtoto kakataa kata kata kasema amekutana na Story nyingi tu za kweli na kuna mengi alishaanza kunihisi lakini alipokuwa anasoma Nyuzi zangu ndio akapata uhakika.

Bila ubishi nikakubaliana na maamuzi yake lakini Roho inaniuma sana,
Najua huu uzi atausoma pia na kunipigia simu.
"MPENZI WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWELI NI MIMI ILA KWA SASA NAKUHAIDI NITATULIA"
 
Back
Top Bottom