Demu myeyushaji

Ungeanza kwa kumpeleka chawote au zero pub sana sana angeanza kukuomba kama 20k or below. sasa m2 kaja na mdogo wake moven pick umeclear bill. Si ashakuona Bab kubwa hiyo laki kwako ni kama 10k tu. Ndo maana kaona kama unamyeyusha vile!! kwa kumnyims hiyo laki, au nimekosea jamani?

Dadangu nilitaka aenjoy mambo ya mji, sikujui... kesho nikikutana na mwingine nitampeleka chawote
 
Nanukuu

"Nilikutana nae kwa mshikaji, kaniambia walikuwa wanasoma pamoja

nikakutana nae mtaani, nikamnunulia msosi, tukabadilisha namba

tukaanza kuchati, mambo ya message usiku kucha, nikampeleka slipway mara mbili, movie mara moja

Kaniambia ananipenda, nami nikampenda tena kwa dhati

kaniomba vocha, nikamtumia, akanibeep nilipopiga, kasema ahsante

nikamwambia tutoke kideti Movenpeak, akaja na mdogo wake, nikalipia gharama

Baada ya wiki, akaniomba laki, nikwamwambia subiri, bado sipo freshi, sasa hajibu message na simu anakata

si miyeyusho au?"

jamni ulimpenda au ulipendezwa nae?maana navyojua mie kupenda ni kazi jamani lkn kupendezwa nae is so easy...Like ndo kupendezwa nae...
 
yaani we ni *****,
movenpick my foot.
sio kila msichana una m treat kwenye five au four star hotel...
ni kama ulijitangazia kuwa wewe ni buzi kwa hiyo kazi kwake kuchuna.
 
Anakuzungusha kila siku, anakupenda kweli?

Nazungumzia juu ya wale ambao wapo katika hatua za mwanzo za kutafuta mahali pa kupata pumziko la moyo! Umeshatoa hisia zako kwa muhusika lakini anakupiga chenga, haeleweki, hajulikani kama anakupenda au lah! Mwingine hazungumzi kitu, mwingine hutoa jibu la moja kwa moja, lakini kuna mwingine anakubali lakini mambo anayokufanyia hayana alama hata moja inayoonesha kweli anakupenda au vinginevyo!

Hili ni tatizo, lakini dawa yake imeshapatikana hapa katika Uwanja wa Huba. Tulianza kwa kuona jinsi ambavyo unatakiwa kumsogeza karibu yako mpenzi wako huyo ‘mtata’. Kwamba, ujumbe mfupi katika simu yake, waraka pepe na hata kumpigia simu sana kwa siku za awali za uchunguzi wako, inaweza kukupa msaada mkubwa sana kwako.

Kama kumbukumbu zako zitakuwa zipo sawa, utakumbuka nilisema kwamba, unatakiwa kuiongoza siku nzima ya mpenzi wako huyo huku manjonjo yakichukua nafasi kubwa kuliko kitu kingine chochote...uwe kiongozi wa siku yake!

Ukiwasiliana naye kila wakati, ataona unavyomjali na hata kama alikuwa na mpango wa kukutana na patina mwingine, nafsi humsuta, maana kila baada ya muda mfupi, simu yake huingiza sms kutoka kwako. Meseji ambazo bila shaka zitakuwa na ujumbe wa mapenzi, kutokana na hilo, siyo rahisi kuingiwa na hisia za kufanya kitu kibaya, vinginevyo atakuwa hakupendi!

Inashauriwa umpigie simu mara tano au zaidi kwa siku na kumtumia sms kumi au zaidi kwa siku, bila kusahau kuwa unapaswa kumtupia waraka pepe mara moja au zaidi kwa wiki!

Lengo ni kumfanya awe karibu na wewe kila wakati, apende asipende na hiyo ndiyo shabaha yako. Ninachomaanisha hapa ni kumfanya aone kuwa wewe ni sehemu ya maisha yake, sehemu ya siku yake, bila wewe siku haiwezi kukamilika. Fanya hivi kwa siku tatu mfulilizo.

(iii) Baada ya kuona mambo ya msingi ya kuzingatiwa kwa siku tatu mfululizo, sasa tugeukie katika siku tatu zingine. Katika muda huu wa siku tatu, unapaswa kumwekea mitego! Hapa namaanisha mitego ya kimapenzi. Kumbuka kuwa kwa siku tatu za mwanzo umeshamsogeza karibu yako, hafurukuti kwa lolote, umemfanya aishi unavyotaka wewe, ni kama hawezi kufanya kitu chochote kabla hujampa maelekezo, sasa mtege!

Hapa hutakiwi kufanya kitu chochote kwa nia ya kumwonyesha mapenzi, bali kaa kimya! Katika siku hizi tatu, hutakiwi kumwandikia sms, waraka pepe wala kumpigia simu, acha yeye afanye jambo hilo. Usithubutu kumfanyia kitu chochote, naomba hapo nieleweke vizuri. Hupaswi kufanya mawasiliano ya aina yoyote na yeye.

Bila shaka kimya chako kitamfanya akupigie simu, akuandikie waraka pepe au meseji, usijibu waraka pepe wala meseji zake lakini simu yake pokea. Hata hivyo, hutakiwi kabisa kutumia maneno kama, dear, sweetie, mpenzi na majina mengine yatakayoonesha lugha laini ya mapenzi.

Mshangaze katika hilo, labda kama akiomba umwite jina la kimapenzi ndiyo ufanye hivyo, lakini wewe kama wewe usithubutu kufanya hivyo. Akihitaji mkutane, kubali!

(iv) Hapa ndiyo mwisho wa mchezo, ukweli unajulikana katika kipengele hiki. Kama anakupenda kweli, kimya chako kitamfanya akutafute na wakati mwingine atahitaji mkutane kwa ajili ya mazungumzo ya faragha, hapo sasa ndipo atakapokueleza ukweli wa penzi lake, lakini kama hakupendi, hatashtuka na atakuacha, kwa sababu sms, waraka pepe na simu zako zilikuwa zinampotezea muda wake tu!

Jiulize, kama ulikuwa unamkera, kuna sababu gani ya kuwa na mtu ambaye hana mapenzi ya dhati kwako? Hapo ni mwanzo wa utumwa ambao mwisho wake ni mbaya. Bila shaka mpaka hapa, utaweza kugundua kama mwenzi wako alikuwa anakupenda au vinginevyo!
 
U said it ol!
senksi mkuu...!
 
Hakika uliingia choo cha kike toka haraka, Japo na wewe nahisi ulikuwa unataka kubofya tu

Heshima mbele mkuu!

Hiyo ID yako imenikumbusha meble sana. Tukiwa watoto wadogo tulikuwa tunatumia manati kuwinda ndege, na joloe ndiye alikuwa ndege mjanja kuliko wote, hapigiki kirahisi! :)
 
Nanukuu

"Nilikutana nae kwa mshikaji, kaniambia walikuwa wanasoma pamoja

nikakutana nae mtaani, nikamnunulia msosi, tukabadilisha namba

tukaanza kuchati, mambo ya message usiku kucha, nikampeleka slipway mara mbili, movie mara moja

Kaniambia ananipenda, nami nikampenda tena kwa dhati

kaniomba vocha, nikamtumia, akanibeep nilipopiga, kasema ahsante

nikamwambia tutoke kideti Movenpeak, akaja na mdogo wake, nikalipia gharama

Baada ya wiki, akaniomba laki, nikwamwambia subiri, bado sipo freshi, sasa hajibu message na simu anakata

si miyeyusho au?"

Haya mbona yamekaaa kama mashairi ya bongo fleva? Halafu wewe lazima ni mwanafunzi wa kidato fulani, maana mambo ya kwenda Slipway siku za Jumapili ni wanafunzi!
 
Huyo alikuwa tapeli tuu huyo hakukupenda wala nini, jaribu kumuepuka mapemaaa, maana mapenzi sio pesa ni kitu cha hiari na moyo msafi, sasa laki ndio hata simu anashindwa kupokea? Ni mapenzi gani hayo ulaghai au nini? **** makini ndugu yangu, dunia hii ina mitihani yake!
 
Ungeanza kwa kumpeleka chawote au zero pub sana sana angeanza kukuomba kama 20k or below.

Naona Chawote ni bab'kubwa mno angeanzia pale Billionare club pange mfaa zaidi hapana watu wengi angeweza hata kufanya matouching touching alafu akamaliza kabisa.
 
Hata hivyo kijana anaonekana bado mgeni kwenye gemu! :)
 
Back
Top Bottom