Demokrasia ya kweli itakuja tu baada ya serikali ya ccm kufa!

Demokrasia ya kweli itakuja tu baada ya serikali ya ccm kufa!

franklin12xx

Member
Joined
Sep 24, 2014
Posts
28
Reaction score
31
Tangia vugu vugu la uchaguzi uanze kumekuwa na mambo ya kustaajabisha sana!
Maana kama NEC ndiyo wasimamizi wa mambo ya uchaguzi, ila nayo inaonekana kutumika na chama tawala kwa mfano:
1. Mgombea urais kupitia ccm siku anazindua kampeni alipitisha zaidi ya nusu saa pamoja na lugha za matusi pale jangwani yaliyotolewa na viongozi waliopita lakini nec walikaa kimya bila kutoa tamko lolote, wakati lema alipopitisha dakika sita tu akasekwa ndani na polisi wakimtuhumu kuzidisha muda wa kampeni, hii inashangaza sana.

2. Mgombea urais wa ukawa alipokuwa kanisani anapoabudu aliongea tu kuwaomba waumini wake wamuombea na kumpigia kura, kesho yake ukaja mjadala mzito pamoja na tamko la nec. Hivi kauli za kibaguzi na lugha za matusi nec hawayoni kwa ccm bali ni upinzani tu ambao ndio dhahiri wanaenda kushika dola.

3. Waziri membe anapotoa tamko kwa waangalizi kuwa wasihudhurie vituo vya kupiga kura na wala wasihoji wananchi wakati wa kupiga kura, je hii ni demokrasia ya kweli au ndio goli la mkono? sasa hao waangalizi wamekuja kufanya nini maana hiyo ndiyo kazi yao.

4. Nikija kwenye hili la TCRA ni kwamba wao wenyewe wamekiuka utaratibu wa kuwasilisha onyo lao kwa vyombo vya habari kuhusiana na urushwaji wa moja kwa moja wa shughuli za uchaguzi huo.

Kwanza TCRA wanasema kwamba kanuni ya huduma za utangazaji sehemu ya 4 vifungu f h na I na kifungu cha 5 sehemu ya b d e na f ni vya sheria ya utangazaji ya mwaka 1993.


Hivyo basi juzi usiku TCRA wakakaa chini na kuongeza kifungu cha utangazaji wa uchaguzi wa vyama vya siasa ya mwaka 2015 je hiki kifungu kimetoka wapi?


Kama kifungu hiki kimetolewa baada ya askofu Gwajima kumchanachana Dr Slaa kwenye vyombo vya habari mapema wiki hii, basi ni kinyume cha sheria ukizingatia kwamba marekebisho yoyote ya sheria yanapaswa kupitishwa na bunge la JMT.


Na kama itathibitika kwamba kifungu hicho kimeongezwa kinyume cha sharia basi TCRA watapaswa kujitokeza na kukiri kuwa wanatumiwa katika kukandamiza hadi za msingi za kidemokrasia nchini na uhuru wa kupata na kupashana habari.

Maana hii siyo demokrasia ya kweli.

mimi naamini demokrasia ya kweli itakuja tu pale upinzani utakapochukua nchi, na kuna uwezekano mkubwa sana chadema kupitia ukawa kushika nchi, kwasababu vuguvugu la mabadiliko linaloonekana kila mahali na ari kubwa ya wananchi kuhitaji mabadiliko kutokana na kuchoshwa na ulaghai wa ccm ni wazi chama kitakachoshika dola hakitachezea tena haki za wananchi wake.
tusonge mbele na tulinde kadi zetu za kupigia kura ili tarehe 25 tufanye maamuzi sahihi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom