Demokrasia barani Afrika ni ya kuogopa kama ukoma, mwenye hoja ya kupinga aje ulingoni

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Messages
8,737
Points
2,000

Bila bila

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2016
8,737 2,000
Demokrasia ndani ya Afrika ni nyenzo ya ukoloni mamboleo. Hivi umeshawahi kujiuliza ni kwanini mabepari/ mabeberu hupenda sana kuona nchi za Afrika zikizingatia demokrasia na haki za binadamu? Na hawakupi msaada kama huzingatii demokrasia na haki za binadamu (wapinzani).

Jibu ni rahisi sana, demokrasia (upinzani) ni sauti ya mabeberu ndani ya nchi husika, hasa bungeni. Beberu hufanikiwa kupenyeza maslahi yake kwa kutumia sauti yake (wabunge wa upinzani) kwani wengi ni njaa na ni rahisi kununuliwa na kuwa vibaraka wa mabeberu, hupewa kila wanachohitaji kushinda chaguzi ili wakawe sauti ya bepari bungeni.
Hivyo basi kuminya upinzani na demokrasia kwa ujumla ni sawa na kuiminya sauti ya beberu kiasi cha kushindwa kupenyeza maslahi yake, hivyo ni lazima atakushinikiza uheshimu demokrasia kwa kukunyima misaada, sharti la ushoga ni decoy tu, lakini lengo kuu ni demokrasia ambayo ndio mlango wanaotumia kutikisa na kuingilia nchi za Afrika kwa mgongo wa upinzani, Kagame sio mjinga kuuona huu mtego.

Ilifikia hatua mbunge aliyekuwa anapigia kelele suala la mikataba mibovu ya madini, na kisha baada ya mikataba hiyo hiyo kufumuliwa anabadilisha gia angani na kusema eti tutashtakiwa MIGA sijui, kumbe ni mabeberu yanamtumia tu kama microphone kufikisha vitisho, halafu anatumika kuleta ujumbe wa blackmail kwamba tusiporuhusu makontena ya mchanga eti ndege yetu itakamatwa huko Canada, msaliti hana aibu!

Sasa hata ingekuwa wewe ndio bepari, usingeipenda demokrasia Afrika? Sasa unapoiminya demokrasia na kukiuka za haki za binadamu kwa kummiminia njugu kama mvua huyo msaliti ni lazima bepari apige kelele kwamba unavunja haki na demokrasia, hata msaada lazima akunyime kukushinikiza, na sisi tulivyo majinga tunaimba haki na demokrasia kama misukule!

Bepari akiona unambana mbavu kama jiwe anavyofanya, basi karata yake huwa ni kutumia upinzani kuendesha maandano ya 'amani' na kufanya mikutano ya kuwalisha sumu wananchi; sasa hata ingekuwa wewe ndio jiwe ungekubali kuona adui yako anaitumia demokrasia kama fimbo ya kukumaliza? Je, hutaivunjilia mbali hiyo fimbo?

Bepari siku zote anaangalia maslahi yake, ilifikia mahali akawa anahonga wafanyakazi wa mabwawa ya kuzalisha umeme ili wafungulie maji na kutengeneza uhaba wa umeme ili watukodisha ma-symbion na ma-aggeko yao ya kinyonyaji! Leo tunajenga stieglers gorge wapinzani wazito kama kabwe wanakuja kupaza sauti ya bepari eti tunaharibu mazingira?

Jiwe endelea kuminya demokrasia na kusigina haki za binadamu hadi mabeberu wajambe damu na kuharisha urojo mwekundu

===============================
UPDATE: 18/12/2018
Haya ndio majibu dhaifu ya Zitto juu ya uzi huu
A Joint Declaration by Leaders and Senior Members of Six Opposition Parties who met in Zanzibar on 16th - 18th December, 2018 to deliberate on the Sta - JamiiForums

================================
Update: 21/01/2019
Mabeberu wanajihami biashara yao ya Majenereta ya kufua umeme isije ikaota nyasi, kuna wabunge wanatumika vibaya kuhujumu maendeleo


===============================
Jinsi marekani na washirika wake wanapolazimika kutumia nguvu dhidi ya Nicholas Maduro - JamiiForums

==============================
Beberu anavyotumia demokrasia kuipindu aserikali ya Venezuela yenye utajiri wa mafuta duniani.Demokrasia nyoko!
=============================
09/02/2019
Rais Erdogan wa Uturukia awaaibisha mabeberu juu ya demokrasia na wanachokifanya Venezuela


Update: 22/06/2019
=================================
=================================
Ukute kwa upumbavu huu na wewe ni kiongozi serikalini.
 

Bongo bO

New Member
Joined
Nov 29, 2019
Messages
4
Points
45

Bongo bO

New Member
Joined Nov 29, 2019
4 45
kwahiyo wewe unasapoti kukandamizwa kwa upunzani afrika na Tanzania?

baada ya kubana demokrasia watatawala miaka mingapi?

Tanzania imeongozwa na chama gani miaka hamsini nini cha maana wamefanya?

mikataba mibovu inapitiswaga na upinzani?
Wapinzania nguvu ya ni kufanya uongo uwe ukweli na ukweli uwe uongo na aslimia kubwa sisi watz bendera fuata upepo. Haina budi na sisi tukafunguka na kuangalia mambo yanayoendelea kwa wenzetu haswa Hong Kong wanafanya maandamano na bendera za usa na uk zikiwa hewani, hapo lazima tujifikirie kwamba tunataka nini. kama tumekubarii mabadiriko ni bora tukubari. nb nabii hakubaliki kwao
 

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Messages
17,674
Points
2,000

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2013
17,674 2,000
Hivi
Beberu
Ni nini maana hasa
Sent from my 4034X using JamiiForums mobile app
Beberu ni mbuzi dume. Ubeberu unaozungumziwa hapa ni hali/ tabia ya ubabe wa mataifa ya magharibi inayoshabihiana na tabia ya ubabe ya mbuzi dume, ndio maana huita mabeberu.
 

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Messages
17,674
Points
2,000

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2013
17,674 2,000
 

nduza

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2019
Messages
373
Points
500

nduza

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2019
373 500
Beberu ni mbuzi dume. Ubeberu unaozungumziwa hapa ni hali/ tabia ya ubabe wa mataifa ya magharibi inayoshabihiana na tabia ya ubabe ya mbuzi dume, ndio maana huita mabeberu.
So sisi tunaplay kama mbuzi wa kike kwenye huu msemo?
 

Forum statistics

Threads 1,367,633
Members 521,789
Posts 33,405,666
Top