Demokrasia barani Afrika ni ya kuogopa kama ukoma, mwenye hoja ya kupinga aje ulingoni

FRANCIS DA DON, Kwa jinsi unavyo present hoja zako inaonekana ni mmoja wa watu ambao aidha wanafaidika na yanayoendelea au unauhusika katika kuyatekeleza haya yanayoendekea.

Naomba nikukumbushe tafsiri ya Mwalimu Nyerere kuhusu maendeleo 'People centered development' kama unafahamu nini Mwalimu aliongea katika hii dhana yake usingebeza dhana ya demokrasia. Huwezi kuminya watu ukaindoa democracy eti kwa kuwa mabepari wataitumia kukupinga, sasa hivyo vitu unavyovifanya unavifanya kwa ajili ya nani? Kama unavifanya kwa ajili ya watu alafu watu hao hawana furaha haina maana bora watu wabaki na umaskini wao huku wana amani. Vyote viwili yaani democracy na maendeleo havina budi kwenda sambamba.

Siku zote tunapozungumzia demokrasia katika Serikali maana yake kwa kifupi ni 'ushirikishwaji' kwamba watu wapo huru kuchangia katika maendeleo ya nchi yao aidha kwa Maamuzi, hoja, nguvu Kazi, au rasilimali zao. Sasa wewe unapopinga democracy maanake unakubaliana na mfumo wa mtu mmoja kuhodhi madaraka ya kuamua kwa ajili ya wengi kwa kila kitu. Mtu mmoja peke yake hawezi kuwa perfect katika maamuzi ya kila kitu lazima ashirikishe wenzie kuamua kwa pamoja.

Sina uhakika kama unamfahamu masuala ya fedha, nimeona point yako sehemu I am sorry kama nitakuwa nimekuelewa vibaya, umesema kuwa ugumu wa maisha unaoendelea umechochewa na mabeberu ili kuwafanya wananchi kuichukia Serikali yao ili mabeberu wapate nafasi. Kwangu Mimi sikubaliani na wewe, ninachoamini hali hii imetokana na mtu mmoja kufanya maamuzi ya kiuchumi peke yake bila kushirikisha wataalam wa uchumi.

Amezuia treasury bill na government bond, ametoa fedha za Serikali katika commercial banks ghafla, amezuia Serikali kufanya biashara na private sector, anafanya miradi mikubwa ya maendeleo by cash kwa wakati mmoja kwa kutumia makampuni ya nje pesa zinaenda nje, lakini wakati huo huo kodi anaongeza na mishahara ya watumishi haongezi.

Mambo haya yote kwa ujumla yanapunguza mzunguko wa pesa ktk jamii na kupunguza purchasing power ya jamii. Sasa kama kungekuwa na ushirikishwaji/democracy haya yasingetokea. Alishauliwa 40% for capital budget kwa nchi yetu itatuathiri akagoma kwasababu hataki democracy/ushirikishaji matokeo yake ndo haya tunayaona.
 
Ebe,
Sijasema Democracy sio nzuri, ila kwa Afrika panapokua na manipulation ya beberu, infact katika awamu za kibepari za benjamini na mkwere demokrasia ya upinzani ilisaidia sana kuibua madudu ya mabapari waliokuwa wameishika serikali, ila kwa awamu hii ya serikali madhubuti bepari amehamia kuinfiltrate upinzani. Chakula hata kiwe kitamu vipi, kikishaingia sumu ni hatari na hakifai.

Kuhusu hiyo maisha kuwa magumu kutokana na heavy capital investments imesababishwa na underinvestment katika awamu za kibeberu, hivyo inabidi tufidie kwani tumechelewa sana! No pain No gain, ila utamu tutauona pale bwawa la Stiegler's litakapokamilika na umeme kuwa wa bei nafuu na wa uhakika na kuchagiza ukuaji wa viwanda,ajira na uchumia kwa ujumla.
 
Utter nonsense

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Bepari anatapatapa tu muda huu, elaborate in what way is it nonsense?

 
Kesi kwa ufadhili wa beberu

 
Update: 21/01/2019
Mabeberu wanajihami biashara yao ya Majenereta ya kufua umeme isije ikaota nyasi, kuna wabunge wanatumika vibaya kuhujumu maendeleo

 
Beberu anavyotumia demokrasia kuipindu aserikali ya Venezuela yenye utajiri wa mafuta duniani. Demokrasia hatari!
 
Back
Top Bottom