Demokrasia barani Afrika ni ya kuogopa kama ukoma, mwenye hoja ya kupinga aje ulingoni

Nilicho gundua ni kuwa wa Tanzania wanao tetea sana jiwe wengi wanafaidika na huu utawala yaan akina bashite,mnyeti ,musiba na wengineo na ndo hawa tunawaona hapa kwa id's fake wakijifanya wao ni wazalendo sana ....lakn kiuhalisia kabisa utawala huu una mengi ya kukemewa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa Uhuru na usalama wa maisha,kudhulumu wakulima,ongezeko la kodi kwa mafanyabiashara ,kutaifisha mafao ya wasitaafu,double standards mfano bashite kuendelea kuwa madarakani ..na mengine mengi ya hovyo!
Mzee baba mimi umeniumiza sana kumtaja Bashite huwa nakwazika sana kumuona huyo mkwepa kodi bado yupo on top
 
FRANCIS DA DON, safi saana kamanda

nimeona unadai hamtolegeza kamba (kukubali demokrasia) na mnajua hujuma zote na mtazipangua
sasa mkuu mtapambana vipi na mabepari aliyakuwa mnatunyima elimu?

atakaepambana na Mabepari ni nani wewe (tabaka la juu) au mimi slum dweller?

huo mpambano na mabepari ni wa aina gani?

unadhani bidhaa zikiadimika mtaani mimi nitafanya nini kama sio kuingia road na kutoa Jiwe kuu


mwambie Jiwe atoe fursa zaidi kwenye elimu (yeye pia alisoma ulaya)

pia awekeze kwenye kilimo ukiweza mwambie pia Bashite cheo kinamzidi uwezo
 
Richard irakunda,
1.) Anaekunyima elimu ni huyu anaetoa elimu ya msingi bure nchi nzima tena hata michango hakuna tena. Anaekunyima elimu ni huyu anaetoa matrillion kwa ajili ya bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu? Au yupi unaemzungumzia?

2.) WaTanzania wote tutapambana na bepari, unataka au hutaki habari ndio hiyo.

3.)Kuna nchi ambazo bidhaa muhimu kama mahindi, mchele na ngano huadimika baada ya beberu kukaza kamba, hii ni kwa sababu chini ya asilimia 5 ya wanachi ndio hujishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na hivyo hutegemea kuagiza chakula toka nje, hii hupelekea wananchi kuandamana na kuipindua serikali, lakini kwa hapa bongo over 75% ni wakulima tena asilimia kubwa ni wa mazao ya chakula, hivyo hilo la kuadimika bidhaa muhimu halipo.Na ndio maana bepari alitaka kuleta teknolojia ya GMO ili mbegu zetu za asili zipotee halafu tuwe tunategemea mbegu za GMO toka kwao na hivyo tungeingia kwenye mtego wa utumwa wa chakula na beberu angetuchezesha ngoma anayotaka kama vikaragosi, jiwe alishtukia mtego huu kwa msaada wa mwanazuoni mzalendo na akapiga marufuku GMO

4.) Fursa gani zaidi unazotaka kwenye elimu zaidi ya hizo kwenye point namba 1? Na uwekezaji kwenye kilimo unafanyika sana kwa kuwapa wakulima stakabadhi za pembejeo na mbegu, na hata uanzishwaji wa kiwanda cha matrekta kilichopo Kibaha ni juhudi za kukuza kilimo.

TUPO VIZURI, demokrasia na haki za binadamu ndio upenyo pekee wa bepari uliobakia, lazima tuuminye tu.
 
FRANCIS DA DON, pote nakubali ila apo kwenye elimu mbona wanafunzi waliosomea shule binafsi wananyiimwa mikopo?

kipiindi cha Mzee Kikwete wanafunzi waliofanya vizuri walikuwa wanapelekwa ulaya kusoma now day hataki?

viongozi wakubwa hii nchi wanahistoria ya kusomea ulaya hataki watu waelimike ili atawale milele?
 
Richard irakunda,
Sasa kwa akili za haraka haraka tu, mtu aliyesoma IST ambapo ada ni milioni 40 kwa mwaka ana asilimia ndogo sana ya kufeli, maana kila kitu wanapata, hivyo most likely atafaulu tu! Sasa umpe mkopo mtu aliemudu kulipa ada ya 40mil+ kwa mwaka na akapata div.1 halafu tumnyime aliesomea chini ya mti akapata div.2 kweli, huyu wa chini ya mti angepewa fursa sawa angepata div.1 bila shaka, hivyo lazima apewe kipaumbele!
 
Sasa kwa akili za haraka haraka tu, mtu aliyesoma IST ambapo ada ni milioni 40 kwa mwaka ana asilimia ndogo sana ya kufeli, maana kila kitu wanapata, hivyo most likely atafaulu tu! Sasa umpe mkopo mtu aliemudu kulipa ada ya 40mil+ kwa mwaka na akapata div.1 halafu tumnyime aliesomea chini ya mti akapata div.2 kweli, huyu wa chini ya mti angepewa fursa sawa angepata div.1 bila shaka, hivyo lazima apewe kipaumbele!
kwahiyo shule zote binafsi Tanzania ni milion 40 ada yake?

Kigoma kuna shule binafsi ada mpaka laki tatu kwa mwaka mfano ujiji secondari na jihad sec

Vipi mtu aliyesomeshwa shule binafsi na kanisa?

Vipi aliyesomeshwa na wazazi alafu wazazi wakapoteza ajira au kufilisika?

Mwambie jiwe Boko Haram ilianza kwa kupinga kofia ngumu (helment)
 
Afrika maana ya demokrasia ni kubadilishana ikulu baada ya hapo mchezo ni ule ule si wote tunamkumbuka Chiluba ?
 

Zitto aliesema tunaharibu mazingira alitumwa na beberu, demokrasia inalawitiwa na wapinzani. TUPO VIZURI
 
MABEBERU NI JANGA KUU LA TAIFA.
Walipitisha mikataba ya gesi na mafuta kama hati ya dharura tena usiku bungeni.
Walisaini mikataba mibovu ya madini
Walisaini mikataba ya IPTL
Walikwiba hela za EPA
Walikwiba hela za Tegeta ESCROW akaunti
Mikataba ya Simbion walisaini wao na chama chao nk
Mwisho wanatuambia wanawaogopa sana ma beberu,sijui wao siyo ccm ni mbuzi jike?
 
Naunga mkono mtoa mada. Kama siyo CCM sijui ingekuwaje..mbowe ,mtei na lissu waliuza migodi hiyo kwa Mabeberu, wakauza mashirika ya umma kwa mabeberu ila chama cha wanyonge kikayarudisha mikononi mwetu,wakati Lissu anakula bata na kusaini mikataba ya Buzwagi pale Hotelini Londoni, kina Job Ndugai walikuwa kule Nyamongo wanahangaika na wananchi waliomwagiwa sumu kwenye mto, wakati Mbowe anasema mtakula nyasi lazima ndege ya rais inunuliwe kina Chenge walikuwa wanapambana kutetea wanyonge, sitakaa nisahau kina Lissu walivyoamuru wachimbaji wadogo kufukiwa hai kule Bulyanhulu ili Mabeberu yachukue mgodi. CCM oyeeee
 
Back
Top Bottom