Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,188
- 3,379
Nikiri tu wazi,
naupenda sana uoga wa Democrats, una ladha tamu sana kwa republicans, Democrats wamejawa chuki zinazowafanya wawe na hofu na wasiwasi kwa chochote anachofanya au wanachodhani atakifanya trump.
kila muda dems wanavyodhani wamekula kete moja, Trump anawasomba kwa kingi.
Democrats wamekazia hoja kwamba trump kaidhalilisha marekani na katiba wakati hawawezi kuonyesha facts, ushahidi, yani hakuna kitu. na ndio maana hata hii kesi iliyofanywa kwa spidi ya haraka imelenga msemo "haraka haraka haina baraka", cha kushangaza kesi ni dhaifu kiasi kwamba kiongozi wa democrats huko senate amebembelezamashahidi waongezeke kwa sababu anajua kabisa kesi haina mashiko, ombi hili lilikataliwa na republicans wa senate kwa kumjibu senatwe sio mahali pa kufanyia homework walizoshindwa democrats.
sio hivyo tu hata raisi wa ukraine ambaye alikua anaongea na trump kwenye simu kakiri mara mbili trump hajafanya chocjote kibaya, pia nimesoma transcripy ya maongezi yao nimegundua hakuna baya lolote.
Ni dhahiri kabisa democrats wanafanya kila mbinu ili wamuondoe trump (kitu kisichowezekana) kwa sababu hakuna democrat anayeweza kufanya anayofanya huyu mzee na yeyote ataegombea uraisi kwa tiketi ya democrats anajua kabisa ni ndoto kumshinda mzee.
Media za marekani nyingi sana kuanzia cnn, msnbc, abc, n.k zipo upande wa democrats na kazi yao ni kumchafua trumop kiasi cha kutunga habari feki *fake news), kwa mfano hizi news zimeaminisha watu wengi kwamba trump kafukuzwa uraisi ama anasubiria kufukuzwa bila kuelezea hatua ambazo mtu akizifahamu na kupata maarifa basi ni wazi kabisa trump hatoki na watu pekee waliopiga kura za kumtoa ni baadhi ya democrats (sio wote) ila waliopinga ni republicans wote na baadhi ya democrats, kwa harakaharaka unaona kabisa hii kitu imekaa kichama zaidi kuliko kitaifa.
mfano mzuri ni hapa hapa tz tena humu humu j.f ukiingia nyuzi ya trump kuwa impeached unaona kabisa 80% ya wachangiaji wamekuwa brain washed na fake news zinazoaminisha uongo kwamba trump kang;oka madarakani.
Trump anataka kuuweka wazi uchafu na madudu ya democrats enzi hadi enzi jinsi yalivyoichafua na kuendelea kuichafua marekani, Joe Biden ambaye aliwahi kuwa makamu wa raisi kipindi cha obama aliwahi kuwatisha ukraide hataruhusu marekani kutoa msaada wa kifedha ukraine kama hawatamsimamisha kazi mpelelezi wa ukraine aliekua akimchunguza mtoto wake aliekuwa akitakatisha fedha, kitendo cha trump kuomba ushirikiano na raisi wa ukraine kufichua uovu huu ndio chanzo kikubwa kilichowafanya democrats waanzishe kesi ya kumtoa ambayo hadi sasa ni dhahiri haitazaa matunfa, ikumbukwe kwamba biden ndie anategemewa kuwakilisha denocrats kuwania urais 2020
Kwa sasa chama cha democrats kimejiharibu sana hasa ukiangalia uso wa chama ni kina ilhan omar wanaotania tukio la kigaidi la 2001, alexandra cotez mwenye matatizo ya kiakili, rashida talib asie na ustaarabu na nancy pelosi ambae chuki imemzidi kuliko reasoning.