Deluxe Pub Iringa Mjirekebishe

Ngusho

Member
Jul 12, 2012
78
131
Mmiliki wa hii Pub hapa Iringa ana kazi kubwa ya kufanya. Niko hapa saa hii, huduma ni Mbovu ajabu, wahudumu wana lugha za ajabu na dharau hadi unashangaa.

Kama ilivyo kwa Liquor store nyingi, wameweka muziki wa Bluetooth, ila wanashindwa ku-control. Yaani mteja kwa sababu kaja pub mapema amepewa access apige muziki yeye tu sasa kalewa, anapiga muziki unafika nusu anakata na kuweka mwingine anaotaka. Yaani ni shidaaa tupu.

USHAURI: Pub yenu nzuri rekebisheni issue ya muziki. Either Muwe na DJ au mruhusu wateja kupokezana kupiga muziki, otherwise mnawakwaza wateja wengine na yawezekana in few weeks to come msiwaone tena hapo. Pia, Wahudumu wajifunze lugha nzuri!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom