Dell Vostro 1500: Msaada wa Kiufundi

AljuniorTz

JF-Expert Member
Jan 6, 2009
544
17
Wakuu ktk nyanja ya kiteknolojia; wiki hii nimeletewa Laptop Dell Vostro 1500 ina tatizo lifuatalo: -

Ukiiwasha baada ya kuload kila kitu na ku-login ktk profile husika inaingia moja kwa moja ktk my documents. Desktop items zoote hakuna na wala ile baa ya chini (start bar) hakuna; inshort - desktop disabled.
Through my documents naweza kufanya mambo yangu yoote; kuzima PC lazima nitue Alt+Ctrl+Delete then naselect shut down option (mtumiaji alikuwa anazima km kibatari ( anabonyeza switch hadi izimike)

Nilimdadisi chanzo akaniambia alitumia ktk net (TTCL) alipomaliza kazi zake akazima laptop akaenda zake kulala. Alipoenda nayo kazini kuiwasha ndio akaona hivyo.

NILICHOFANYA
step: 1. Nilienda ktk safe mode, nika-restore hadi tarehe/siku before tatizo lililotokea; ika-restart, kurudi ni yaleyale.
step: 2. Nikaenda tena ktk safe mode without system restore; nikatengeneza PROFILE MPYA, then nika-restart PC. Ilipoamka nikaingia ktk profile mpya; but game ni ileile na profile hiyo hupati kitu chochote (my documents ipo empty na hata zile options nyenginezo ambazo ktk old profile nazipata (km control panel, my computer n.k) huku sizipati.
step: 3. Nikafanya utundu mwengine wa kufuta baadhi ya programs n.k but tatizo lipo pale pale. Pia niliingia ktk FORUM ya Dell but sijapata majibu yenye kuridhisha zaidi ni procedure amabazo nishazifanya.

Je yupo ambae ameshakutana na tatizo km hili?? au mwenye clue???

CPU: Core Duo
OS: Windows Vista Business
RAM: 2 GB
HDD: I60 GB

Tusaidiane mbinu na mawazo.

Nawasilisha
 
Jaribu kufanya hivi. Right click desk top kisha nenda arrange Icon by then click show desktop Icon. Kama nimekuelewa tatizo lako.
 
MKUU,bado hujamuelewa, sio kwamba hakuna kitu kwenye desktop tu bali hata start bar haipo.
 
AljuniorTz,

Jaribu alichoelekeza Tukufu

Unaposema "umetengeneza profile mpya" unazungumzia "computer account mpya" (new login name and password)?
Nilimdadisi chanzo akaniambia alitumia ktk net (TTCL) alipomaliza kazi zake akazima laptop akaenda zake kulala. Alipoenda nayo kazini kuiwasha ndio akaona hivyo.
Kama sio virus basi huyo jamaa hakukueleza yote.

Task bar yenye START button huenda imefichwa kwa bahati mbaya. Move your cursor kuelekea chini hadi ifike mwisho ambapo itabadilika shape kuwa nyeusi yenye mshale. Left click and hold, then move it up a little and release cursor.

Task bar utaiona inachungulia (like 1 or 2 milliliters), chini, juu, kushoto au kulia pembezoni mwa screen.
 
Last edited:
Nakushauri Ujaribu kufanya alivyosema Lazydog kuhusu task Bar,tatizo likiendelea kuwepo basi bila shaka ni Virus na katika hali kama hiyo huwezi ku-install Antivirus(kama ni kweli kuna virus). Hamisha Mafile yako ya muhimu kwenye External HDD,Format machine yako,Install Antivirus yenye akili kama Kapersky,connect your External HDD,Do Full scan,rudisha ma-file yako. You'll be happy again with Your Dell.
 
Ukiiwasha baada ya kuload kila kitu na ku-login ktk profile husika inaingia moja kwa moja ktk my documents. Desktop items zoote hakuna na wala ile baa ya chini (start bar) hakuna; inshort - desktop disabled.

Naomba muelewe; SWALI: Kwa nini ikisha log in ianze kufungua my documents folder wakati before haikuwa hivyo???:confused:

Jaribu kufanya hivi. Right click desk top kisha nenda arrange Icon by then click show desktop Icon. Kama nimekuelewa tatizo lako.

Hayo yote nilishafanya na bado hakuna kipya kilichotokea; maelekezo yako hayahusiani na tatizo lililopo

AljuniorTz,

Jaribu alichoelekeza Tukufu

Unaposema "umetengeneza profile mpya" unazungumzia "computer account mpya" (new login name and password)?Kama sio virus basi huyo jamaa hakukueleza yote.

Task bar yenye START button huenda imefichwa kwa bahati mbaya. Move your cursor kuelekea chini hadi ifike mwisho ambapo itabadilika shape kuwa nyeusi yenye mshale. Left click and hold, then move it up a little and release cursor.
Task bar utaiona inachungulia (like 1 or 2 milliliters), chini, juu, kushoto au kulia pembezoni mwa screen.

Nimetengeneza profile mpya (account mpya yenye username na password); hayo yote unayosema nilishajaribu.

Nakushauri Ujaribu kufanya alivyosema Lazydog kuhusu task Bar,tatizo likiendelea kuwepo basi bila shaka ni Virus na katika hali kama hiyo huwezi ku-install Antivirus(kama ni kweli kuna virus). Hamisha Mafile yako ya muhimu kwenye External HDD,Format machine yako,Install Antivirus yenye akili kama Kapersky,connect your External HDD,Do Full scan,rudisha ma-file yako. You'll be happy again with Your Dell.

Mkuu afkombo;
kwangu ku-format PC huwa ni option ya mwisho kabisa km kila kitu kimeshindikana. Maana kila pc ikiwa na virus au windows inaleta uzushi unafomati; unakuwa hujifunzi kitu kipya.
 
Mkuu afkombo;
kwangu ku-format PC huwa ni option ya mwisho kabisa km kila kitu kimeshindikana. Maana kila pc ikiwa na virus au windows inaleta uzushi unafomati; unakuwa hujifunzi kitu kipya.
Good! Now we know what is not the problem.

Humu jamvini kuna discussion ya tools hizi mbili,
HijackThis and ComboFix

Try them

Anti-virus gani unatumia?
 
Look My Documents open at startup

Do your desktop icons show up? Look in processes in task manager to see if explorer.exe is running. To open up the registry editor in task manager click file > new task > regedit > now you can continue with the this link My Documents open at startup

Nishajibu tangu huko mwanzoni; Desktop Icons hazipo; naweza ku-access desktop icons through my documents (through drop down menu ktk hilo folder).

Explorer.exe ipo ktk process

Good! Now we know what is not the problem.

Humu jamvini kuna discussion ya tools hizi mbili,
HijackThis and ComboFix

Try them

Anti-virus gani unatumia?

Ilikuwa ina McAfee alipoinunua; ktk ku-try and error nilimuwekea Kaspersky but haikuona chochote.
HijackThis nimeijaribu hakuona ndani; nitaijaribu hiyo ComboFix maelezo yake yamenivutia kuijaribu.
 
Tukufu kwenye post number 8 aliweka link ambayo ingeweza kutatua tatizo la My Document kufunguka upon boot. Ku-fix kimoja kimoja kwa utaratibu huu ni gharama.
Link nyingine hii hapa: http://support.microsoft.com/?kbid=899865
Au tumia hii: Fix (download and run/merge)
 
Hiyo option sijaifanya bado; nahitaji kujua chanzo cha tatizo kwanza kuliko kuanza kutafuta solution. Naweza kufanya Backup and Restore but then tatizo likajirudia tena.

Nilikuwa namaanisha Operating System backup. That is, making an image of your Windows to an external storage media such as DVD or external HDD. Ikiwa unayo CD ya Windows Vista, this may not be such a big deal of a thing to do at this point.
 
Ukishalogin jaribu bonyeza ALT+CTRL+DELETE then nenda kwenye task manager. ukifika hapo click "new task", halafu andika explorer.exe. Je unapata nini?

Pia jaribu kufanya hivi halafu utupatie majibu.

Fanya kama hapo juu then kwenye "new task" andika "regedit" bila ya hizo quotes.

Regedit ikifunguka nenda kwenye location hii;

HKEY_LOCAL_MACHINE\SOFTWARE\Microsoft\Windows NT\CurrentVersion\Winlogon

Then kwenye upande wa kulia wa registry editor baada ya ku-click Winlogon utaona vitu(value) kadhaa. Tafuta value inayoitwa "Shell" then double-click kwenye hiyo Shell halafu tuambie hiyo Shell imeandikwa value gani?

Waiting for your reply.
 
Last edited:
Nashkuru wanajamii wenzangu tatizo nilimaliza tangu jana mchana; nilipitia mtandao huu hapa ambao nilipata msaada wa ku- restore explorer.exe; No Icons on my PC only Desktop Background

Ile profile mpya niliyotengeneza ilipokuwa na tatizo lile lile kama profile ya zamani nikajua tatizo lipo ktk explorer; nikafanya task manager na ku-run explorer.exe; kila kitu kikarudi kama mwanzo. Tatizo likaja niki-log off au ku-restart pc tatizo linarudi km mwanzo. Ndio nikaanza kutafuta ufumbuzi wa kudumu.

Katika ku-search ndio nikapata clue kutoka kwa hao jamaa wa kioskea.net (thanx 2 them na bwax {mchango wake nimeuona asubuhi hii}). Nikarekebisha kule kwenye Registry; nika-restart. Kurudi juu nikaingia ktk ile profile mpya ikawa mswano; niswitch to old nayo iko bomba.
Then nika-update Kaspersky Antivirus; kumaliza matatizo yaliyobaki.

Sasa hii mbinu haitanitoka kumkichwa abadan; kuliko ninge restore au kuformat.

Naomba tufunge mjadala

Again thanx to all of you.
 
You are welcome. Am glad umefanikiwa kulitatua coz tatizo lilichukua muda kidogo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom