Asante sana kwa maelezo, na kuna mdau Mlamoto amemaliza kabisa kwa kusema haiwezi kujaa.
Msinichoke bado mgeni kwenye hayo mambo:
Kama ndiyo hivyo ni kama hakuna limit (ukiacha lifespan), vipi kuhusu hizi capacity unaambiwa Hard disk gb5, Ram and Hdd so on hiyo haimaanishi kwamba kuna limit kuhifadhi data? ndiyo maana sisi bila kujua tuna-delete tukidhani tunameondoa kila kitu ili kupata space kubwa (hasa tunapoona computer inakuwa slow), kwa maelezo mengine hiyo HDD ukiacha life span haiwezi kujaa kabisa na kutoruhusu trash kutoka recyclebin ziingie?
maelezo yako unapata 98%
Limit ya kuhifadhi data ipo kama hautafuta mafaili. kwa ufahamu wako Hdd za sasa hivi ni kubwa mno Hakuna 5gb tena!
hard disk lifespan yake ni wastani wa miaka 5.
kwa hivyo usinunue hard disk used kamwe.
hard disks zina motor ambazo zinazunguka kama mara 5400, 7200, 15000 kwa dakika. Hivyo baada ya muda zinachoka.
kuna aina mpya ya storage inaitwa SSD. Solid state disk. inatumia technology ya flash disk kutunza data, ndo nzuri kwa sasa, haichoki mapema na inahimili mikimiki, haitumii motor
kuwa slow kwa computer yako haisababishwi kujaza vitu Kwenye computer.! No!
inasababishwa na program zinazojaza RAM yako na zile zinazo ifanya processor iwe bize muda mrefu.
huwa zinaingia pamoja na program unazoweka. nyingi zina autostart. Nyingi ni za kidaku... huku zikijinadi kuwa zinafanya auto-update. ukweli ni kuwa zinapeleka information kadhaa kwa walio zitengeneza na hata kwengineko.... watch out!!!!
Mkuu malizia basi hzo asilimia 2 alizobakisha
Maelezo mafupi na rahisi ni haya;
utunzaji wa mafaili Kwenye Hdd ni kama uandishi wa kitabu. kuna ukurasa unaitwa yaliyomo (hizi ni references tu)
na kurasa mbali mbali zinafuatia.Ukitaka Habari kihusu jambo fulani unakwenda Kwenye yaliyomo. yaliyomo inakuelekeza ni ukurasa upi.
Ndivyo na Computer ilivyo. computer inakuonyesha yaliyomo kama mafaili ma mafolder.
Kwenye Computer katika kufuta mafaili; maelekezo ( references tu) yaliyo kwenye yaliyomo ndo yanaondolewa na ukurasa unabaki kama ulivyo, japo computer inaweza kuandika tena katika ule ukurasa na kuuingiza kwenye listi ya yaliyomo tena!
umeona pekundu hapo chini? Haikwepi kuandika data katika sector hiyo...
except inategemea na mzigo ulionao computer kwa muda huo(processes), position of the hard disk head and the closest free space iliyopo.. hata kama itakuwa ndo hiyo ambayo imefutwa hiyo hiyo sekunde
By CYBERTEQ
Lol! Unapofuta file haliondoki katika sector lilipohifadhiwa, kinachobadilika ni entry tu, OS yako inabadili anuani kutoka say "my documents" kwenda "trash",
hivyo sector ya hdd lilipohifadhiwa hilo file inakuwa bado na kitu kilekile kama kilivyohifadhiwa kuondoa anuani tu. Hivyo basi, uki-empty recycle bin yako unafuta hata hiyo anuani ya pili "recycle bin" hivyo inakuwa ngumu kulitrace file lako kiurahisi,
lakini si kwamba file limetoweka kabisa, linabaki palepale kwenye sector ileile, na computer ita-asign jina maalum katika file lako, computer itakwepa kwa kadri iwezekanavyo kuandika data nyingine katika sector hiyo,
hivyo katika muda huo ukitumia software maalum inalocate file lako na inaweza kulirejesha kwa kulipa anuani nyingine!
vipi kuhusu Simu hizi msg tunazofuta nazo zinaenda wapi?
Mkuu sijui nini, nafikiri kuwa neno 'DELETE' kwa maana ya 'futa' ukihusisha majibu mbali mbali yaliyotolewa ktk thread hii si sawa kutumika; neno zuri labda lingekuwa 'MOVE' kwa maana ya kuhamisha file kutoka sehemu lilipo kwenda ktk 'trash can'. Nasema hivi kutokana na sababu kuwa, unaweza kutumia a special program kupata tena file lako lililopelekwa ktk 'pipa la uchafu'.
Asanteni sana wataalam coz hadi sasa naendelea kulicover mafile yangu. Nashukuru sana JF nitawapa matokeo
Asante sana kwa maelezo, na kuna mdau Mlamoto amemaliza kabisa kwa kusema haiwezi kujaa.
Msinichoke bado mgeni kwenye hayo mambo:
Kama ndiyo hivyo ni kama hakuna limit (ukiacha lifespan), vipi kuhusu hizi capacity unaambiwa Hard disk gb5, Ram and Hdd so on hiyo haimaanishi kwamba kuna limit kuhifadhi data?
ndiyo maana sisi bila kujua tuna-delete tukidhani tunameondoa kila kitu ili kupata space kubwa (hasa tunapoona computer inakuwa slow), kwa maelezo mengine hiyo HDD ukiacha life span haiwezi kujaa kabisa na kutoruhusu trash kutoka recyclebin ziingie?
Mkuu sijui nini, nafikiri kuwa neno 'DELETE' kwa maana ya 'futa' ukihusisha majibu mbali mbali yaliyotolewa ktk thread hii si sawa kutumika; neno zuri labda lingekuwa 'MOVE' kwa maana ya kuhamisha file kutoka sehemu lilipo kwenda ktk 'trash can'. Nasema hivi kutokana na sababu kuwa, unaweza kutumia a special program kupata tena file lako lililopelekwa ktk 'pipa la uchafu'.
mkuu, maelezo unayosema ni rahisi ndio magumu zaidi, yaani no mtiririko wala collocation na hiyo mifano ni irrelevant kabisa naomba huyo uliempa 98% umpe 100% na wewe ujipe 05% kwani umetuchanganya zaidi!
Unapo empty trash nini hutokea.