Ded - aliyetoa machozi kishapu aagizwa na bosi wake!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ded - aliyetoa machozi kishapu aagizwa na bosi wake!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SpK, Feb 3, 2009.

 1. S

  SpK Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Bw. Mlaki ametakiwa kuheshimu mamlaka ya madiwani

  2009-02-03 12:31:28
  Na ITV Habari


  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Brigedia Jenerali mstaafu Dkt. Yohana Balele amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Bw. Jesse Mlaki kuheshimu mamlaka ya madiwani.

  Dkt. Balele ametoa agizo hilo katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo baada ya kupata malalamiko kutoka miongoni mwa madiwani hao kuwa mkurugenzi huyo amekuwa akikiuka utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya baraza lao.

  Amesema madiwani ndiyo wawakilishi wa wananchi katika halmashauri hiyo hivyo mkurugenzi hana budi kuwaheshimu, kufanyia kazi na kutekeleza maamuzi yote ya vikao vyao ambapo pia amemtaka awe akiwapatia taarifa za fedha zinazoingia katika halmashauri hiyo kutoka serikalini na kuwasomea mapato na matumizi wanapoyahitaji.

  SOURCE: ITV
   
Loading...