Naona ili tuwe salama mbele ya safari, tuandae viongozi wengine waadilifu. Huyu bwana watu wanavyomuchukulia itakuwa ngumu sana kuwa kiongozi tena TZ.Tunao watu wenye uwezo wa kuongoza. Tuanze kuachana sasa na haya majina yasiobadilika toka enzi zile na hakuna lolote linalofanyikaKwa taarifa, sijamsafisha Lowassa kwa alichotuhumiwa au nilichokisema. Nimeainisha baadhi ya vitu vya kiutendaji ambavyo alivifanya pamoja na bugudha niliyokuwa nayo ya kuona alichokuwa akikifanya ni batili kabisa.
Lowasa atarudi madarakani muda si mrefu na anategemewa kuchukua uraisi hapo baadaye.
Kumbukeni Mwalimu Nyerere aliwakataa Kikwete na Lowasa kugombea nafasi hizo kubwa. Hawa jamaa kwa pamoja waliamua kung'ang'ania na kusaidiana kwa hali na mali hadi wakapata nafasi hizo kwa makubaliano ya kuachiana kiti cha uraisi. Hivyo Lowasa anajua kabisa kwamba ni lazima arudi madarakani haraka kadri iwezekanavyo ili iwe rahisi kwake kuwa raisi wa Tanzania.
Alichokuwa anafanya Lowasa katika nafasi ya uwaziri mkuu ni kukusanya pesa kwa kila namna ambazo zingemsaidia katika kampeni yake ya kwenda ikulu. Huo mradi wa Richmond ilikuwa ni moja kati ya njia za kukusanya pesa. Alikuwa ana mipango kabambe kabisa ya kuuza Bandari ili kukusanya pesa za kampeni.
Pamoja na makelele yetu yote bado Lowasa atarudi serikalini na kuchukua madaraka makubwa katika nchi hii.
Tanzania inamilikiwa na watu wachache sana na Lowasa ni moja kati yao.
What kind of question is this? That you are at all able to entertain this kind of idea shows how seriously you must be underestimating the intelligence of ordinary Tanzanian people. Stop peddling this kind of nonsense and get real!
Kwa taarifa, sijamsafisha Lowassa kwa alichotuhumiwa au nilichokisema. Nimeainisha baadhi ya vitu vya kiutendaji ambavyo alivifanya pamoja na bugudha niliyokuwa nayo ya kuona alichokuwa akikifanya ni batili kabisa.
MWISHO WA TOLEO LA KWANZA LA MAFISADI WA ELIMU.
I AM READY FOR ANY CHALLENGE.