Debate on what happened during latest CCM-NEC meeting:

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
Debate on what happened during latest CCM-NEC meeting:

THIS DAY


AT least one topmost official of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) has openly confirmed a brazen party bid to silence once and for all some of its more vocally anti-corruption MPs, including National Assembly Speaker Samwel Sitta, during last month’s CCM national executive committee (NEC) convention in Dodoma.

In his written treatise believed to have been distributed to various diplomatic missions in the country, CCM vice-chairman Pius Msekwa acknowledged that Sitta and a number of CCM legislators were collectively criticized for their lack of party loyalty and discipline, but insisted that this was done for a good cause.

The Speaker was criticized primarily for his failure, while guiding the deliberations of the House, to observe the parliamentary conventions governing the exercise by parliament of its control function over the government, Msekwa said.

The document is understood to have been circulated amongst members of the diplomatic community in Tanzania, to explain CCM’s position in the wake of the social and political debate now simmering across the country regarding what precisely transpired during that NEC meeting in Dodoma.

Msekwa, Sitta’s predecessor as National Assembly Speaker, is now a member of the three-man team picked during the meeting to oversee efforts to restore party unity and fix CCM’s growing image problems.

The team is led by ex-president Ali Hassan Mwinyi, and also includes former Speaker of the East African Legislative Assembly, Abdulrahman Kinana. Its primary task has been described as to seek ways of healing an apparent deep rift between a growing number of CCM legislators and the central party establishment itself.

All three members are sitting members of the all-powerful CCM central committee.

In general, Msekwa’s remarks contained in the new document, a copy of which has been obtained by THISDAY, appear to contradict earlier statements by various CCM senior functionaries which vehemently sought to deny all reports of any kind of friction during the Dodoma NEC meeting.

Some of the key CCM officials who have been in such denial so far include secretary general Yusuf Makamba, publicity secretary John Chiligati, and self-styled propaganda specialist Richard [?]Tambwe Hiza.

But according to Msekwa: Particular reference was made to certain unacceptable utterances which have been made by members of parliament and the Zanzibar House of Representatives in their respective Houses, as well as the conduct of Speaker Samuel Sitta.

He sought to deny media reports quoting various legal experts saying the NEC meeting deliberations had contravened Article 100 of the national Constitution in trying to curb ruling party legislators from exercising their democratic right to debate issues freely in the House, but insisted on the importance of maintaining party organization and discipline during this era of political pluralism.

He said since competition between political parties does not terminate with elections, but only shifts to the floor of parliament, appropriate rules of competition are also required at this new stage of competition within the House.

�This emphasizes the importance as well as the high value of the CCM parliamentary party caucus rules, and the need to adhere to them, for the smooth operations of parliament,� he added.

Amongst senior diplomats in the country who are understood to have made clear their alarm at the reports of what transpired during the latest CCM top-level meetings was the Swedish Ambassador, Steffan Herrstrom, for one.

It is understood that during the highly-charged Dodoma meeting, more than 40 NEC members launched direct attacks on Sitta and other ”rebel” MPs for speaking out against high-level corruption in government.

They accused the Speaker of ”embarrassing” the government by allowing MPs during the recent parliamentary budget session to openly criticize senior public leaders, both past and present, and there were several calls for Sitta’s immediate expulsion from the party and replacement as House Speaker.

An official CCM statement issued after the meeting said merely that all ruling party cadres - particularly MPs � had been banned forthwith from speaking out on widespread corruption and abuse of office allegations against ex-president Benjamin Mkapa. Nothing else was said.

 
lC.gif
Mwandishi Wetu

Raia Mwema
Septemba 16, 2009


rC.jpg

bul2.gif
Wa Sweden aenda hadi ofisi za CCM


bul2.gif
Msekwa aziandikia waraka kuzipoza



bul2.gif
Akiri NEC ilikosea taratibu




BAADHI ya balozi nchini zimefuatilia taarifa za kikao kilichopita cha Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichotafsiriwa kuwa kililenga kuziba midomo ya wabunge, ili kujiridhisha na usalama wa fedha zao zinazokuja Tanzania kwa njia ya msaada wa kibajeti, Raia Mwema imeambiwa.
Hatua hiyo ya ufuatiliaji, taarifa zinasema, imechagizwa na hoja kwamba kama ni kweli kwamba chama tawala kiliwaonya wabunge wake wapunguze kelele dhidi ya Serikali na hivyo kuua uhuru wa Bunge na mbunge mmoja mmoja wa kuikosoa, basi kazi muhimu ya Bunge na wabunge ya kuisimamia Serikali, itakuwa hatarini.
Taarifa kutoka kwa maofisa wasaidizi wa baadhi ya balozi hizo, zinaeleza ya kuwa baadhi ya mabalozi wamepelekewa waraka maalumu ulioandikwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, kwa lengo la kueleza kwa ufasaha kile kilichojiri katika kikao cha NEC cha mwezi uliopita mjini Dodoma.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa mmoja wa balozi zilizopelekewa waraka huo wa Msekwa ni wa Sweden, ambao Balozi wake alifika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo hayo na masuala mengine ya kisiasa, hatua ambayo imethibitishwa na ubalozi wa Sweden nchini, ingawa pia ubalozi huo umesisitiza kuwa hayo yalikuwa mazungumzo ya kawaida kuhusu masuala ya kisiasa nchini. '‘Ni kweli (Balozi Staffan Herrstrˆm) alikwenda CCM Lumumba. Na walifanya mazungumzo kuhusu masuala ya kisiasa. Huu ni utaratibu wa kawaida,'' alisema katibu muhtasi Doris Lema, akikariri majibu ya Balozi kwa maswali ya Raia Mwema juu ya safari yake ya ofisi za CCM.
Katika hatua nyingine, Raia Mwema imefanikiwa kupata nakala ya waraka wa Msekwa kwa balozi kadhaa zinazoifadhili Tanzania ambao, pamoja na mambo mengine, unazungumzia yaliyojitokeza katika kikao hicho cha NEC, akionyesha upungufu katika taratibu za kumjadili Spika Samuel Sitta na kasoro miongoni mwa wabunge wa CCM wanaojitambulisha kuwa ni wapambanaji wa vita dhidi ya ufisadi.
Katika maelezo yake, Msekwa anatoa ufafanuzi katika maeneo makuu matatu aliyoyaweka kwenye mtindo wa maswali, jambo la kwanza likiwa ni "Mjadala kwenye NEC umehoji uendeshaji wa Bunge, hatua ambayo ni uvunjaji wa kifungu cha 100 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?"
Jambo la pili: "Ni sahihi kwa NEC-CCM kujadili mwenendo wa wabunge wake ndani ya Bunge, akiwamo Spika? Kwa maneno mengine, kitendo hicho kinavunja sheria ya mamlaka na haki za Bunge? Pili: "Spika amekabwa kwenye kikao hicho kwa sababu ya kuwa mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya mafisadi? Kabla ya kutoa ufafanuzi wa kina katika maeneo hayo, Msekwa anaeleza; " jibu kwa kila swali ni hapana."
Anasema katika waraka huo ya kuwa NEC ina wajibu wa kujadili mwenendo wa viongozi wake ingawa katika kikao cha Dodoma utaratibu wa chama hicho kumlalamikia kiongozi au mwanachama mwingine yeyote haukuzingatiwa.
"Kifungu cha 108 cha Katiba ya CCM kinaeleza majukumu ya jumla ya mikutano ya NEC, na kifungu kidogo chake cha nane kinaeleza kudumisha uangalizi juu ya vitendo vya wanachama na viongozi wa CCM, hii maana yeke ni kudhibiti mwenendo na vitendo vya wanachama na viongozi wake.
"Kuingilia mambo ya Bunge ni makosa, lakini umma unajua kuwa kumekuwa na makundi hasimu miongoni mwa wabunge kuhusu vita dhidi ya ufisadi, wapo wanaopinga ufisadi na wengine wanaopuuza vita hiyo. Spika alikosolewa kwa kushindwa kuendesha mijadala bila kuzingatia maslahi ya chama, na wabunge wamekosolewa kwa kushindwa kutumia kamati ya wabunge wa CCM," anasema Msekwa.
Hata hivyo, pamoja na kuonyesha kuamini kuwa kulikuwa na nafasi kwa Spika kuendesha mijadala kwa kutazama maslahi ya chama na pia NEC kuwa na wajibu kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho kufuatilia na kuhoji mienendo na vitendo vya wanachama na viongozi wake, Msekwa anasema makosa yalifanyika ndani ya NEC.
"Kitendo hicho cha NEC kinaweza kuwa ni makosa. Ingawa kujadili mwenendo wa Spika na baadhi ya wabunge wengine wa CCM kinaweza kutetewa kwa mujibu wa Katiba ya CCM, lakini pia kuna makosa yamefanyika na hasa kwa upande wa kuzingatia taratibu na kanuni za chama.
"CCM imekuwa na utaratibu na kanuni nzuri kwa viongozi wake wanaolalamikiwa mwenendo wao kwamba wamekiuka kanuni na maadili ya chama. Sheria na kanuni hizo zinaeleza kuwa kiongozi anayetuhumiwa anapaswa kupelekewa orodha ya tuhuma zake na kupewa fursa ya kuzijibu.
"Na baada ya hapo, Kamati ya Maadili ya CCM inakutana kwa ajili ya kuchambua suala hilo na kufanya uamuzi na pia kutoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu (NEC). Kwa hiyo inaridhiwa kuwa taratibu za kisheria hazikufuatwa katika suala hili," anaeleza Msekwa katika waraka wake huo wenye kurasa 11.
Anaongeza:"Ni vizuri ikaeleweka kwamba katika utamaduni wa siasa za vyama vingi umuhimu ni lazima uwekwe na kudhibitiwa ndani ya chama cha siasa, hususan suala la nidhamu. Na uhai wa chama chochote cha siasa ni umoja na nidhamu.''
Katika hatua nyingine, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alain Noudehou, amewasifu Rais Jakaya Kikwete na Spika Sitta kwa kazi nzuri ya Rais Kikwete kuruhusu uhuru wa kuzungumza ikiwa ni pamoja na kutoa fursa kwa Watanzania kumuuliza maswali ya papo kwa papo.
Akizungumza, jana, Jumanne, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Mwakilishi huyo wa UN alimsifia Sitta kwa mpango wake wa kuendesha Bunge vyema katika wajibu wake wa usimamizi wa Serikali.
 
Huko CCM ni hovyo kabisa! Yaani mpaka Mabalozi wa nje waje juu ndiyo wanagundua kwamba kulikuwa na makosa kwenye Kikao cha NEC kilichopita! Kweli hiki ni chama cha mafisadi! Nani wa kuwajibishwa kutokana na makosa hayo!? Mwenyekiti wa Chama, Naibu Mwenyekiti au Katibu Mkuu!? Chama cha mafisadi kilichoshindwa kuwafukuza chamani mafisadi mbali mbali akina Mkapa, Chenge, Lowassa, Mramba, Makamba, Rostam na wengineo wengi tu, hakuna atakayewajibishwa kwa makosa hayo ya kuvunja katiba ya nchi.
 
Haya wadau sikilizeni clip hii. Bofyeni ili mpate uondo kuhusu mafisadi:
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=rudsvrKu5Bc[/ame]
 
Back
Top Bottom