Mrs Bishanga
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 1,002
- 2,293
Sisi ambao tulikimbiwa na mama zetu, hii mada imetupita kushoto..
Ni kweli Mrs ila pia kumbuka mama ako alikua mke wa mtu nakasha wahi kuumiza huyu mtu vibaya.......kwa kiasi watu wengine kuhukumu kwamba wanawake hawako katika jamii ya binaadamu, kwa vitimbi vyao kwa wanaummeIkiwa bado siku chache kumaliza mwaka 2019 nimetafakari sana mambo ambayo mama anayafanya katika maisha ya mtoto wake.
mbali na kuwa nimekuwa mtu mzima ambaye najitegemea kwa kiasi kikubwa bado mama yangu amekuwa na mchango mkubwa katika maisha yangu. Nikiwa nimezongwa na mawazo ya maisha kimbilio ni Kwa mama yangu....nikisikia sauti yake tu ninapona na kujiona mpya kuweza kuikabili changamoto iliyo mbele yangu.
Hivi Hawa wamama wameumbwa na roho za aina gani? Wao yawe mazuri au mabaya huyabeba bila lawama.
Wana upendo wa kujitoa .....Yani hapendi kuniona ninasononeka? Yani hata awe na Akiba yake akiniona Nina mawazo ya kutatua ishu flani ya hela Basi Mara moja tukimaliza tu maongezi nitaona muamala wa tigopesa unasoma....kucheki mama ashaziba shimo...
Hata nikosee vipi huwa hahukumu Kama walivyo wababa. Huyu mama huwa namkosea weeeee lakini siku zote amebaki kuwa mtulivu na wa kusamehe bure bila hata kuombwa msamaha.
Mama ameweza kutoa Vingi ili kuniona ninatimiza ndoto zangu na ninakuwa mtu wa furaha bila kujali malipo.
Ee Mungu nijalie siku moja na Mimi niweze kumfurahisha mama yangu hadi asahau taabu zote alizopitia Kwa ajili yangu.
Ee mama nakuombea maisha marefu katika dunia hii.
Mpende mama yako bila kujali Hali yake.....mama Ndio mtu pekee duniani hapa ambaye hata dunia yote ikuzomee bado atabaki amesimama na wewe mpaka dakika ya mwisho.
Kama unamuombea mama yako heri Basi usipite bila kutia neno.
Hapo ndo siwaelewagi wanawake au wamama.... yaani wao huwa hawakosei, na ikitokea wakakosea, basi mwanaume au baba ndo kasababisha..!!Ukiona hivyo chanzo kilikuwa baba. Chunguza vizuri utakuja kujua
Tehtehteh..... unataka uwaelewe mkuu?Hapo ndo siwaelewagi wanawake au wamama.... yaani wao huwa hawakosei, na ikitokea wakakosea, basi mwanaume au baba ndo kasababisha..!!
Mama ni mama....hakuna mtu mwenye huruma kama anayeitwa mama...ata watu wakutenge kiasi gani bd atabaki na wewe, ata uwe umefanyaje jambo gani la kukera bd atakusamehe tu,
Upendo wa mama kwa mtoto wake ni mkubwa sana, hakika tuwajali mama zetu kwa kiasi kikubwa hapa ulimwenguni.
Binafsi nampenda sana mama yangu, kwn ndy msiri wang, rfk yng, shogha yng, kila kitu kwangu.
Hapo ndo siwaelewagi wanawake au wamama.... yaani wao huwa hawakosei, na ikitokea wakakosea, basi mwanaume au baba ndo kasababisha..!!
Aisee
Imani za ajabu sanaNyie ndo mnadanganywa na waganga kwamba mama zenu wanaweza kuwaloga. Kwanini alikuzaa Kwa uchungu ili aje akukoge ukubwani ? Kwa nini asingekutoa mimba tu? Msiendekeze waganga
umeandika mada nzuri unakuja kuharibu kwenye reply [emoji41]Ukiona hivyo chanzo kilikuwa baba. Chunguza vizuri utakuja kujua
Ata Mimi nashangaa ,kwanini akunitupa kwenye mtalo, Ila ukubwani ananichawiaNyie ndo mnadanganywa na waganga kwamba mama zenu wanaweza kuwaloga. Kwanini alikuzaa Kwa uchungu ili aje akukoge ukubwani ? Kwa nini asingekutoa mimba tu? Msiendekeze waganga