Magulumangu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 3,047
- 455
- Thread starter
-
- #61
Naona mwanisifia, tungo mwazifurahia
Mwasema ziko sawia, na tena mmeridhia
Vina mwaniambia, hakika vinatishia
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
Kutunga nilitamani, toka zama za zamani
Labda sikujiamini, ningeanzaje jamani
Leo nipo furahani, najaribu hii fani
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
Ni kweli sijakomaa, ningali ni mwanafunzi
sitokata na tamaa, nipate mwingi ujuzi
Mola nipe shufaa, ili niwe mkufunzi
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
Msaada mnipatie, enyi mliobobea
Msiniache nikimbie, bahari kuogelea
Kweli mnisaidie, tungo zisije pelea
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
kwanini nimeingia kusoma hili shairi!!!
Malenga bado mpo kumbe....
Ngoja nikakariri kamusi kwanza
Naona mwanisifia, tungo mwazifurahia
Mwasema ziko sawia, na tena mmeridhia
Vina mwaniambia, hakika vinatishia
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
Kutunga nilitamani, toka zama za zamani
Labda sikujiamini, ningeanzaje jamani
Leo nipo furahani, najaribu hii fani
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
Ni kweli sijakomaa, ningali ni mwanafunzi
sitokata na tamaa, nipate mwingi ujuzi
Mola nipe shufaa, ili niwe mkufunzi
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
Msaada mnipatie, enyi mliobobea
Msiniache nikimbie, bahari kuogelea
Kweli mnisaidie, tungo zisije pelea
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
shuka mwana wewe shuka,tungo zako zi sawia,
kamwe hutoteremka,hapo ulipo kawia,
si wote tu mauruka,sifazo kukusifia,
mkuu yakuonea,wewe mwana upo juu,
muite klorokwini,aspirini na mangu,
mwanakijiji hayani,kamwe hao ndio mwangu,
lizi aso kibindoni,judi asiye kiwingu,
Mkuu yakuonea,wewe mwana upo juu,
sijakutembo mkuu,nisje litia maji,
mweka we mpaka majuu,malenga wetu si maji,
lijua neno kajuu,malenga ndio mtaji,
Mkuu yakuonea,wewe mwana upo juu....
Karibu upite ndani, ewe ndungu wa fani
Sasa umo hesabuni, jiskie wa nyumbani
Tujumuike kundini , JF furahani
Wala sijione duni, huna hata mpinzani
Changamoto ninakupa, tena usiipuuze
Sredi moja ungetupa, nasi tuiendeleze
Hapa tuchape lapa , sifa za mama tutunze
Ombi usijelikwepa, twaomba utekeleze
Chagua mada yoyote, igusayo moyo wako
Wakijiji umchote , ajibu mapigo yako
Magulumangu atete, nitaweka kiitiko
Aspirin avue pete , tukuvike taji lako
Uzi tunausubiri , mimi na Judith pia
Lizzy nae ni mahiri, hakika atachangia
Shossi nae ni hatari, hii fani kabobea
Nawe wako ujasiri , kofia nakuvulia
hehehe Yakuonea sasa tunaomba sredi yako ya mistari
Wakuu ninasimama, heshima kuwapatia
Napenda zenu hekima, lengo kunisaidia
Na kila nikitazama, siwezi kuwafikia
Changamoto nimepata
Mimi bado maamuma, kutembea sijaweza
Si kama narudi nyuma, Uzi kweli nitaweza?
Ndugu zangu sijagoma, ila sitaki jikweza
Changamoto nimepata
Ukaidi sijafanya, naomba mnielewe
Mwaweza hata nikanya, tusigombane wenyewe
Kifani sijachanganya, nitarusha vipi mawe
Changamoto nimepata
Muda ukifikia, uzi nitawatumia
Msije acha changia, mawazo yenu kutia
Kweli nimeweka nia, kloro fuatilia
Changamoto nimepata
Wala tena usihofu
Ombi sio msahafu
Muhimu usistaafu
Komaa na uzoefu
Ukitoa tutajibu
Ila hiyo si wajibu
Lakini ukijaribu
Utakifunga kitabu
Ukisubiri tuanze sisi
Wengi wetu ni waasi
Uzi kuanzisha si rahisi
Ni kaskazi hadi kusi
Lakini tupo pamoja
Japo tunajikongoja
Ipo siku itakuja
Tutaja kuvika koja
Nimeangalia watu wengi ambao wako kwenye fani ya ushairi nimeona wanamajina ya ushairi, mfano mzuri ni klorokwini na wengine wengi, hivyo na mimi kama mpenda mashairi nimeamua nitafute jina la kiushairi, na jina nitakalo tumia ni SINDANO YA GANZI, ninahisi labda klorokwini wewe ni mtu ambae uko kwenye fani ya madawa (sina uhakika na hili) na unaelewa vizuri umuhimu wa sindano ya ganzi,hivyo basi kwa wale wasio elewa undani wa sindano ya ganzi naweza kuandika mistari michache kuelezea umuhimu wake na kwa nini nimeamua kujipa jina hilo, labda siku za usoni naweza kuja kuandika kama kuna uhusiano wowote kati yangu na sindano ya ganzi kiuhalisia
Tunaisubiria mistari mkuu, jina limetulia kabisa. Magulumangu akiwapa dozi ya sindano ya ganzi, klorokwini na aspirin. kwisha habari yao! lol
JINA LA KISHAIRI
Mwenzenu nimefikiri, jina kujitafutia
Kwenye fani ushairi, niweze kulitumia
Pokeeni mistari, jina nawafunulia
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi
Sindano ile ya ganzi, sisi sote twaijua
Inafanya nyingi kazi, nani asiyetambua
Kupasua hauanzi, bila ganzi kupatiwa
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi
Ganzi itakufariji, pindi upasuliwapo
Utasikia baridi, tena hapo kwa papo
kutumima inabidi,hakuna njia mkato
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi
Maumivu utasikia, ganzi isipo tumika
Utaishia kulia, tena na kufadhaika
Ganzi yatusaidia, yabidi kuheshimika
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi
Sitaki tena fikiri, vipi isingekuwepo
Upasuaji nakiri, leo ungekuwa ndoto
Uliza madaktari, ganzi kweli kiboko
Jina langu kishairi, sindano mwana wa ganzi
Mshairi wenu
Sindano ya ganzi
Jina tumelipokea, na hati miliki yake
Limetulia!
Baraka twalimwagia, hii fani liiteke
Si nakwambia!
Maelezo umetowa, sababu ya kuchagua!
Imenoga!
Wa ganzi umekuwa, sindano isiyouwa
Umewakoga!
Sasa dozi wapatie, kutwa 2 mara tatu
Watapona!
Butwaa wakushangae, huyu ndie ganzi wetu?
Utawakuna!

Kloro ninashukuru, kwa jina kuliridhia
Wewe ni mwanga na nuru, mengi menisaidia
Tena hujui kufuru, na sasa tu ndugu pia
Sindano nakushukuru, mimi ndo mwana wa ganzi
Sijui ingekuwaje, jina ungelichukia
Jingine ningepataje, ganzi ningelililia
Ni furaha ilioje, kweli nalifurahia
Sindano nakushukuru, mimi ndo mwana wa ganzi
Kloro tukamatane, na mengi sasa tufanye
kwenye vita tupigane, ole wao mabwanyenye
Na tuwe kama mashine, ili tuwafinye finye
Sindano nakushukuru, mimi ndo mwana wa ganzi
Sindano ya Ganzi