De Gea wa Man United ni mshamba sana

De Gea wa Man United ni mshamba sana

Haina guarantee kwamba atafanikiwa. Akumbuke siku za mwanzo Man U walimvumilia ndiyo maana kafika alipo.
Real Madrid akiboronga mechi tatu ndiyo mwisho wa soka lake. Hawana msamaha wala uvumilivu aliopata Man U siku za mwanzo.

Hakika Mkuu. Wanakununua kW rate yyt na wanakufuky ukiboronga. Ref. bale, nakumbuka mchezaji wa kiingeleza alibironga ikawa mwsho wa maish yke. simkumbuk jina.
 
Anapata nafasi ya kurudi nyumbani, mji aliozaliwa na kukulia, marafiki na familia watamshangilia kwa karibu na urahisi zaidi week in week out. Kila mtu kwenye viatu vya De Gea angefanya hivyo, hutajua unapapenda nyumbani kiasi gani mpaka utakapoondoka na kwenda sehemu yenye watu tofauti, na tamaduni tofauti.

Na kikubwa zaidi, anapata nafasi ya kutoka hadhi ya Antonov-124 kwenda An-225, Imagine that. Kama huu ni ushamba, ningeongeza Mshamba katika majina yangu kwenye vyeti.

yaan Mkuu kama unasahau aliekutoa tongo. itafaa sana uwe balotel.

Nitoe tongotongo antonov ni nini. 225 je
 
yaan Mkuu kama unasahau aliekutoa tongo. itafaa sana uwe balotel.

Nitoe tongotongo antonov ni nini. 225 je
De Gea alikuwa kipa bora na kwenye ramani ya dunia tangu Atletico Madrid, ndio maana United walitoa fungu walilotoa kumsajili. Haya ya kumvumilia na nini, ni kwa sababu walijua uwezo wake.

Antonov 124, na 225 ndio ndege kubwa zaidi duniani, zilitengenezwa kipindi bado USSR haijavunjika kama ushindani baina yao na wamarekani. Ni ndege za mizigo na kwa sasa zinamilikiwa na Ukrain. An-225 ambayo ndio kubwa zaidi, ukiiweka OT pale inavuka goli mpaka goli, na kama ingekuwa modified ibebe abiria, ingechukua mpaka watu 1500, wakati ndege inayobeba abiria wengi mpaka sasa hawazidi 800. Kuna documentaries zake unaweza kutafuta kama ukihitaji kujua zaidi.
 
Kinachomfanya aione man utd haifai najua ni wakala wake, lakin ole wake

hata huyo aliyeko pale Madrid sasa alikuwa mkali, atakuja juta.

Hivi watu wengine hawaigi kustaafu soka kwa heshima kama Van de sar? Hiki Kizaz cha enzi za Kikwete hatari sana

View attachment 252292

Umenifanya nikuone wewe ni mtu wa aina gani. Kwa taarifa yako kizazi cha kina kikwete ni hao makocha kina van gaal, mourinho na wengineo. Huyo De gea ni kizazi chenu ndiyo maana akili zinafanana. Yaani hapo ulichomaanisha kama de gea ana matatizo basi na wewe una matatizo unless kama umezaliwa enzi za nyerere au uko katika kizazi cha mzee mwinyi.
 
yaan Mkuu kama unasahau aliekutoa tongo. itafaa sana uwe balotel.

Nitoe tongotongo antonov ni nini. 225 je

Kwahiyo unamaanisha kila uliyemtoa bikra lazima umuoe au? Kwakuwa akienda kuolewa na wengine basi hafai anasaliti
 
washabiki wa man u mnachekesha sana De gea amefanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi kusema hatatamba mnajisumbua kwani alianza kuwika akiwa hispania badala ya kumlaani mnatakiwa kutafuta makipa wengine bora mbona mnataka kumchukua mshambuliaji wa toteham au nyie mnaona sawa kuchukua vya wenzenu ila nyie kutoa hamtaki
 
Wachezaji wa Kihispaniola waliokuzwa katika miji ya Barcelona au Madrid huwa hawapendi sana kukaa nje ya nchi yao Spain...

Hilo lipo pia kwa wachezaji wa Kijerumani...

Uingereza ndio usiseme. Hata tanzania pia.

Ila de gea kama hataondoka nitamshangaa sana tumemvumilia sana toka kipindi kile cha babu Fergie alikuwa na makosa mengi mno.
 
Yaani huyu dogo sina hamu naye, enzi zile amesajiriwa alikuwa anatufungisha magoli mengi kweli yakipuuzi, hadi washabiki wakawa wanamuona kama ferg anahujumu timu kwanini asimutimue, akamvumilia leo ameweza imekuwa shida, anakuwa na majipu!!!! ila kwa msimu huu ametuokoa sana!!

valdes yuko vizuri kumshinda De Gea
 
Bahati mbaya sijawahi kumkubali kama ni kipa bora. Uwa anafungwa magoli ya kijinga sana.

Tiba

Ni kipa bora sana, magoli mengi anayofungwa ni yanakuwa deflected, kama imeshawahi ku notice, anafata mpira lakini unamgonga beki na kuingia
 
Ni kipa bora sana, magoli mengi anayofungwa ni yanakuwa deflected, kama imeshawahi ku notice, anafata mpira lakini unamgonga beki na kuingia

Kipa mzuri inabidi awe flexible Bwana!!!! Halafu anafungwa magoli ya direct kick ovyo ovyo.

Tiba
 
Back
Top Bottom