DCEA yatoa pendekezo wauza dawa za kulevya kunyongwa

DCEA yatoa pendekezo wauza dawa za kulevya kunyongwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeeleza kuwa ipo tayari kushauri mamlaka husika kutunga sheria itakayoruhusu wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya nchini kunyongwa.

Pamoja na pendekezo hilo, mamlaka imewataka watu wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya kujisalimisha na kuwaomba radhi Watanzania kwa kosa hilo.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema mamlaka iko tayari kuwasamehe watakaofanya hivyo kwa hiari na kutoa ushirikiano wa dhati.

"Yeyote anayetaka kujisalimisha afike ofisi za mamlaka au apige namba 119 ili apatiwe maelekezo zaidi. Mamlaka haitawachukulia hatua za kisheria watakaojitokeza na kuwaomba radhi wananchi," alisema Kamishna Lyimo.

Aliesema dawa za kulevya zina athari kubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla, ikiwemo kuchochea uhalifu unaofanywa na waraibu na kuharibu miundombinu ya maendeleo ambayo imegharimu fedha nyingi za umma.

Aliongeza kuwa wauzaji wa dawa hizo wanapaswa kuwaomba radhi Watanzania kwa madhara makubwa waliyosababisha.

"Wapo walioko mafichoni ndani ya nchi nawaomba wajitokeze. Kwa wale waliokimbilia mataifa jirani, tunafahamu wapo nchi zipi na tunaendelea kushirikiana na nchi hizo ili kuwapata na kuwachukulia hatua za kisheria," alisema Kamishna Lyimo.

Kamishna Lyimo alitoa kauli hiyo wakati wa zoezi la uteketezaji wa dawa za kulevya zenye uzito wa jumla ya kilogramu 4,402.02 za aina mbalimbali zilizokamatwa nchini. Zoezi hilo lilifanyika katika kiwanda cha saruji cha Twinga kilichopo Wazo, jijini Dar es Salaam.
 
Ukweli wanaujua, na hao wanaoandaliwa kunyongwa ni sadaka ili biashara iende vizuri, hakuna biashara inafanikiwa bila sadaka.
 
Picha imeanza au bado ni trela
Wakijisalimisha watawaomba radhi watanzania kwa njia gani
 
Back
Top Bottom