Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Bw. Mwanga amempeleka polisi mtumishi wa halmashauri Bw. Mohamedi Semkamba kwa kosa la kuchelewa kuondoa vifaa vya mwenge. DC alikasirishwa na kitendo cha Bw. Mohamedi kuchelewa kuchukua vifaa vya mwenge, ingawa Mohamedi alichelewa sehemu ya tukio kwa vile alikuwa anaokoa gari la serikali lililotaka kuungua moto. Mara alipofika pamoja na utetezi wote, DC aliita askari wa polisi na kutoa amri ya kumweka chini ya ulizni wa polisi hadi atapotoa amri nyingine.
DC huyu tangu afike Lushoto amekuwa ni mbabe anayependa kutukuzwa na wafanyakazi wote wa serikali wilayani Lushoto; tukio hili ji mwendelezo wa uvunjwaji wa UTAWALA BORA, SHERIA na matumizi mabaya ya madaraka kwa mfano ni yeye DC kwa ushirikiano na RC Chiku Galawa siku za karibuni walimweka lupango DMO kwa kosa la kunywa maji ya chupa mbele yao. wakidai ni kitendo cha dharau kwa viongozi wake. Pia DC amewahi kujaribu kumweka Lupango, DED na Mwanasheria wa Halmashauri ya Lushoto.