DC wa Bagamoyo awaonya mgambo wanaojifanya trafiki

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,721
2,000

MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, amewapiga marufuku askari mgambo wilayani hapa wanaokamata pikipiki zinazobeba abiria, maarufu kama bodaboda na kuonya kuwa hiyo si kazi yao.

Mwanga alitoa onyo hilo juzi alipokuwa katika ziara ya kusikiliza kero mbalimbali zikiwamo za maji na umeme zinazowakabili wananchi wa Kata ya Lugoba, Halmashauri ya Chalinze.

Alhaji Mwanga alisema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusiana na vitendo vya mgambo kukamata bodaboda.

Alisema mgambo ambao ni askari wa akiba. Hivyo hawaruhusiwi kukamata bodaboda kutokana na kwamba si askari waliopewa jukumu hilo.

"Askari mgambo ambao ni askari wetu wa akiba hamruhusiwi kukamata bodaboda kwani si askari mliopewa jukumu hilo. Kwa kufanya hivyo mnakwenda kinyume cha sheria, " alisema Mwanga.

Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Uzalishaji Maji katika Mto Wami, Mhandisi Christina Mchomba, akizungumzia kero ya maji, alisema utafiti walioufanya katika mto huo umebaini uwapo wa tope kubwa.

Kutokana na kero hiyo, alisema wanaendelea na mradi huo kwa kufanya upanuzi wa mitambo ambayo inaenda sambamba na ujenzi wa matangi 19 ambayo yatasaidia kuhifadhi maji.

Mchomba alisema moja ya matangi hayo linajengwa katika kijiji cha Mazizi lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni mbili, litasaidia kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho.
 

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
Hawa mgambo wamekuwa wapuuzi sana kuingilia mpaka majukumu yao nje mipaka yao ya kazi. Nikiwa likizo Mwanza siku niliwahi kuvunja jino mgambo kwa uonevu alikuwa anampigia mmachinga mateke bila kuwa na kosa.
 

chilubi

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
7,890
2,000
Mimi naomba kujua sheri inasemaje kwa ujumla? maana naona hata FFU wamekuwa wanafanya kazi za traffic sifahamu kabisa. Mwenye link ya haya masuala ya nani ana haki ya kukudai leseni ama kukushtaki kwa makosa ya barabarani aniletee
 

South

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
3,494
2,000
Sio kwamba hawajui ila ndio hali halisi ilivyo sasa maana hata humu JF tunaona baadhi ya members wakiamlisha polisi wamkamate nani kwa sababu zao
 

marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
14,829
2,000
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, amewapiga marufuku askari mgambo wilayani hapa wanaokamata pikipiki zinazobeba abiria, maarufu kama bodaboda na kuonya kuwa hiyo si kazi yao.


Kwani wakati wanawaajiri hawakuwapa maelekezo ya majukumu yao? na kwanini wasiwachukulie hatua kwa kufanya makosa hayo kama kweli hawakuelekezwa kufanya hivyo?
 

Africa Tanzania

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
1,429
2,000
Sheria inapovunjwa mtu yeyote anaruhusiwa kuisimamia! Mie Nadhani kakosea..... Wenye Elimu ya juu mnisaidie hili
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom