DC Tarime azuia Mashindano ya Mbunge Esther Matiko, Bukombe na Babati yaendelea

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Tusome UZI tafadhali. MKUU WA WILAYA TARIME anazuia mashindano ya #EstherMatikoRisingStar

Mkuu wa wilaya ya Tarime, Charles Kabeho amezuia mashindano ya kuibua vipaji #EstherMatikoRisingStar yanayoandaliwa na ofisi ya mbunge Tarime Mjini Mh: Esther Matiko akitoa sababu mbili kwa wakati tofauti; 1. Uboreshaji daftari la wapiga kura 2. Uchaguzi wa serikali za mitaa (hii kamueleza katibu wa mbunge ofisini kwake)

Chama cha mpira wa miguu Tarime (TAFA) baada ya kupokea katazo, bila kuhusisha wadau wa michezo/waandaji, wakaandika barua kwenda ofisi ya mbunge kuwataka wasitishe bonanza hilo. Wakirejea sababu zilizotolewa na DC. Kumbuka "bonanza" sio lazima kusimamiwa na chama cha soka

Ofisi ya mbunge ikapokea barua ya TAFA, kuzuia mashindano, wakaandika barua kwenda TAFA, FAM na ofisi ya DC kuwajulisha sababu kadhaa zikiwepo gharama zilizotumika kuandaa, wakaomba mashindano yafanyike jioni au yaanze na kusimama zoezi likianza, yaendelee baadae! DC bado akagoma!

Ofisi ya mbunge ikaomba mashindano yachezwe saa 10:30 jioni baada ya zoezi kumalizika (saa 10:00 jioni), DC akagoma, Mbunge akaomba mashindano yaanze, lakini yatasimama 'siku saba' kupisha zoezi (13-8-2019 hadi 19-8-2019) kupisha zoezi hilo, DC akagoma na kuleta hoja ya kuwepo zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa, ambalo Kimsingi ratiba ni Mwezi November!

TAFA (TARIME Football Association) wakagoma, wanasema wao wanafuata maagizo ya mkuu wa wilaya kwa sababu ni Mwenyekiti wa Baraza la michezo wilaya (sheria ya BMT 1967 na 1971) pia mlezi wa TAFA, hivyo wanafuata agizo lake. Ingawa TAFA wamepokea tayari fedha za uandaaji na vibali vimetolewa, vimelipiwa! DC akasema yeye hajatoa ruhusa mashindano hayo kufanyika!

Ofisi ya mbunge Tarime Mjini baada ya hapo, imegundua kuna maslahi ya kisiasa "yamechopekwa" kutoka kwa DC wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime (kada wa CCM), hata baada ya kupewa mfano wa Babati kuwepo Bonanza la mbunge Pauline Gekul, siku 14 zoezi la uandikishaji likiendelea, bado amesema "shughuli za kijamii zitasimama kupisha zoezi hilo Tarime mjini"

Pia, Mbunge wa Tarime mjini Esther Matiko amempigia simu DC wa Tarime, zaidi ya mara moja (wazungumze) hapokei, Mbunge kaandika SMS bado hazijibiwi (Mbunge yupo DSM kwenye kesi kule Kisutu) hivyo, ameamua kukutana na viongozi wa TFF, waziri wa TAMISEMI na waziri wa Mambo ya Ndani kuwasilisha malalamiko yake kwao.

Hata hivyo,kwa sababu mabonanza yanaweza kuandaliwa nje ya utaratibu wa vyama vya soka wilaya, mashindano hayo yataendelea kama yalivyopangwa, yataanza 08.08.2019, kamati ya mashindano itaundwa nje ya TAFA, na DC atapaswa kuzuia mashindano hayo kwa sababu nyingine sio hizi ambazo ametoa! TFF wanapaswa kufahamu masuala haya yanayofanywa na TAFA

NB; Mkuu wa wilaya, Bwana Charles Kabeho, anasahau kwamba, mashindano kama haya yaliyoandaliwa na UVCCM - Tarime wakati shughuli ya kitaifa ya Mwenge wa uhuru ukipita kwenye wilaya za mkoa wa Mara ikiwepo Tarime, mashindano hayo yalifanyika bila bugudha na hayakuwahi kuzuiwa. Mkuu wa wilaya hatendi sawa

Mfano mwingine ambao ameupuuza: Wakati zoezi la uboreshaji daftari la wapiga kura kwa mfumo wa BVR likiendelea nchi nzima hivi sasa Bonanza la Mbunge wa Bukombe Dotto Mashaka Biteko linaendelea huko Jimboni kwake (Bukombe) na fainali itakuwa mwezi huu 17/08/2019.. Mkuu wa wilaya ya Bukombe, Said Nkumba hajalizuia bonanza hilo.

Wakati Mkuu wa Wilaya ya Tarime akitoa katazo hilo kwa Bonanza la Mhe Esther Matiko huko Kata ya Susuni Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kuna Bonanza la Kata hiyo likiendelea, na wilaya hii ni moja, majimbo ndio tofauti. Kwamba BVR itakuwa Tarime mjini pekee huko Tarime vijijini zoezi hilo halipo? Hizi ni mambo ambazo zinapaswa kukemewa!

Shughuli za kijamii ambazo zinapaswa kusimama ni zipi? Barua yake haikuainisha. Je, wananchi wataacha kufungua maduka? Kwenda shamba? Kwenda misibani? Kufanya ibada? Kwa sababu kuna siku saba za uandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura? Kwani ni suala la lazima? Au kwa sababu ya uwepo wa mashindano hayo? Athsri zake ni zipi!? Hazitajwi..

Mfano kwa sasa kuna kampeni inaendelea Tarime nzima inaitwa "NYUMBA NI CHOO" inaendeshwa na Mrisho Mpoto (msanii wa kuimba), kwanini kapewa kibali cha kuendelea na kampeni hiyo na mashindano ya #EstherMatikoRisingStar yanazuiwa kupisha shughuli ya kitaifa? Je, Mrisho Mpoto ni sawa kufanya hayo lakini mbunge wa jimbo sio sawa?

Hata hivyo, kwa mujibu wa kalenda ya michezo ya TFF na TAFA Mwezi Oktoba kuna mashindano ya ligi ya wilaya (daraja la nne) yanamalizika Mwezi November, lug ya mkoa inafuata (daraja la tatu). Wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, Je atasimamisha mashindano hayo kwa sababu kutakuwa na shughuli za uchaguzi wa serikali za mitaa??

Hizi ndio siasa za nchi yetu zinavyoathiri mpira wa nchi yetu.. Watawala wenye kutokana na vyama vya siasa, hususani CCM wanatumia madaraka na mamlaka yao vibaya, hata wakati ambao tunaopaswa kuletwa pamoja (kutumia michezo) bado tunagawanywa. Sifikirii kama ni sawa! TARIME yetu, mshikamano wetu!

#MMM, Martin Maranja Masese
FB_IMG_1565115150522.jpeg
FB_IMG_1565115156420.jpeg
FB_IMG_1565115138546.jpeg
FB_IMG_1565115125665.jpeg
FB_IMG_1565115121181.jpeg
Screenshot_20190806-212541.jpeg
 

Attachments

  • FB_IMG_1565115156420.jpeg
    FB_IMG_1565115156420.jpeg
    40.8 KB · Views: 36
Hajui kuwa Bwana Luoga alipita hapo ? Rais Magufuli hafurahishwi kwa style hiyo bwana DC. Siku moja ukijichanganya tu unatoka hapo tena kwa aibu. Hapo ulipokalia tunakuchora tu.

Hilo ni jimbo la mpinzani lazima ucheze jwa Akili sana ; wapende hao wananchi ili wananchi waipende serikali yako tofauti na Hapo utaonekana unaichonganisha serikali yako na wananchi kama unavuofanya kwa sasa.

Karibu sana nyama choma kichuri na Ugali mwekundu.
 
Hawa watu wanaogopa nini kama kazi yao ni safi
Woga uliopitiliza na kugeuka kuwa kiburi cha kipumbavu.
Wanatakiwa kufahamu kuwa tawala duniani hazidumu milele. Zinafika wakati vyama tawala vinaondoshwa madarakani kwa njia moja au nyingine.

Aidha, mifumo ya tawala pia hubadilika. Maadam mtu yuko madarakani anajifanya ndiye sheria.
 
Hili jina la Charles Kabeho ni la Waheshimiwa sana. Kuna mmoja alikuwa Waziri miaka ya 90s na mwingine Kiongozi Mkimbiza Mwenge Kitaifa 2018.

Kuzuia mchezo hii nafikiri hakuna u lazima kivileeee zaidi ya kuwapa sifa waliozuiwa. Vinginevyo Tume ya Uchaguzi itoe mwongozo. Mbaya zaidi washiriki ni vijana. Wataambiana na kuleta usumbufu/huruma isiyo na lazima.

Sometime hz Siasa zisahaulike ili maisha yaendeleee. Kufanya siasa muda wote kuna madhara makubwa.
 
Mkilazimisha mjue mnaenda kinyume na maagizo ya bwana DC,anaweza kuwaletea washawasha.
 
Huyo si kapewa tu zawadi ukuu wa wilaya. Kwahiyo kwa kufanya hivyo ndio anarudisha fadhira kwa mfalme Juha!!
 
Yaani sielewagi kabisa, yaani mtu wa kuletwa kwa barua awe na mamlaka eneo husika kuliko mbunge wa kuchaguliwa wa eneo husika?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom