DC nusura amsweke rumande padre

DC nusura amsweke rumande padre

KAUMZA

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
699
Reaction score
240
Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki parokia ya Chumbageni, Padre James Kabosa ameponea chupuchupu kuswekwa ndani na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa wilaya mwenyewe, Padre Kabosa na msemaji wa Askofu, Padre Peter Kagaba walipozungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti.

Imedaiwa kuwa padre huyo aliepuka kuswekwa ndani kwa kuondoka ofisini hapo baada ya kutofautiana na mkuu huyo wa wilaya na hivyo kumuita mkuu wa polisi wa wilaya afike na kumsweka ndani ndipo wazee wa kanisa waliokuwa wameambatana naye kumsihi Padre aondoke.

Imedaiwa kuwa baada ya tukio hilo Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Baba Askofu Anthon Banzi, alifika ofisini kwa mkuu huyo wa wilaya akitaka kujua chanzo cha Padre Kabosa kufukuzwa na kutishiwa kuswekwa ndani.

Habari zimebainisha kuwa baada ya mkuu wa wilaya kuona Askofu ofisini akiwa na waumini alimuelewesha kiini cha kumtimua Padre na kumuomba msamaha.

Waumini waliokuwa wamemsindikiza Askofu wao walishikwa na butwaa baada ya kumuona mkuu wa wilaya huyo akipiga magoti mbele ya Askofu Banzi na kuomba abarikiwe na askofu kwa madai mumewe pia ni mkatoliki abarikiwe ili Mungu amsaidie katika kazi zake za kuiongoza jamii.

Akiongea na NIPASHE kuhusu tukio hilo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Mikael, Kiule Msofe, alisema tukio la kufukuzwa kwa Padre lilitokea Machi 27, mwaka huu majira ya saa 8 mchana na tukio la Askofu kufika kwa mkuu huyo wa wilaya lilitokea Aprili 3 na kuwa matukio yote mawili alikuwapo na kuyashuhudia.

Kuhusu chanzo cha tukio hilo, Kiule alisema ni kutokana na mgogoro wa ardhi wa eneo la wazi lililogawanywa na diwani wa kata ya Nguvumali, Selemani Mhina (sele boss) CCM, lililopo mbele ya kanisa la Kigango cha Majani Mapana kinyume cha sheria za ardhi.

Alisema kanisa katoliki lilishaomba eneo hilo zaidi ya mara mbili kwa Jiji la Tanga na kujibiwa kuwa ni eneo la wazi na lakini lilitolewa kwa wafanyabiashara kwa madai kuwa ni agizo la mkuu wa wilaya ili kujenga mashine za kusaga nafaka.

Kwa upande wa padre Kabosa alikiri kupatwa na kadhia hiyo lakini alidai kuwa tayari suala hilo linashughulikiwa na viongozi wakuu wa kanisa hilo kwa hatua zaidi za kurejesha amani na mshikamano ulioonekana kukosekana.
Naye Mkuu wa wilaya, Dendego alipotakiwa kuelezea shutuma hizo alikiri ujio wa padre Kabosa ofisini kwake na kutofautiana kimazungumzo lakini alidai kuwa alimuamuru kuondoka ofisini hapo kwa kuwa hakumtambua kama ni kiongozi wa dini.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alikanusha tuhuma za kueneza udini na kwamba hilo halikufanyika kwa ajili ya udini bali ni moja ya matokeo ya kiutendaji.

Alimtupia lawama na kumtaja diwani Mhina kuwa ndiye anayechochea mgogoro huo kwa kueneza udini kuwa yeye anawapendelea waislamu jambo ambalo ni hatari.


Chanzo: Nipashe Jumapili
 
Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki parokia ya Chumbageni, Padre James Kabosa ameponea chupuchupu kuswekwa ndani na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego kwa madai ya utovu wa nidhamu.


Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa wilaya mwenyewe, Padre Kabosa na msemaji wa Askofu, Padre Peter Kagaba walipozungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti....

Hii story kama ni kweli, nikiunganisha na ya majuzi ya Madam kuzichapa live kikaoni-wananchi wa wilaya husika wamkatae DC wao. Mkuu wa Wilaya anayeendesha ofisi KAMA KIJIWE cha wababe wanini kuwa naye enyi wakazi wa wilaya husika?
 
Constitutionally speaking, a district commissioner and other officers of similar job design, description and specification posses no POWER OF ARREST except.

Such powers are at all times vested only law enforcement agencies like the police force, a DC's job position being a boss to the police fraternity notwithstanding.

How glad it comes to me that a senior citizen to the calibre of a Priest do understand this so well regardless of a misguided DC's wishfull thinking to ultraviously usurp power of authority only existent in own mind and not legal system of our country.
 
Baba aliyewazaa watoto(Rais) akawapa urithi(vyeo) wafanye wanavyotaka juu ya urithi waliopewa ndo kinachotokea kwa viongozi wetu,

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki parokia ya Chumbageni, Padre James Kabosa ameponea chupuchupu kuswekwa ndani na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego kwa madai ya utovu wa nidhamu.


Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa wilaya mwenyewe, Padre Kabosa na msemaji wa Askofu, Padre Peter Kagaba walipozungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti.....

Like father like son. Unategemea nini kama chanzo cha hili kipo kwenye shina?
 
kama kawida,udini kwenda mbele,hakyamungu hatupumui mwaka huu.
 
Ni kukosa busara. Ningekuwa mwajiri wake ningemuita kwa mahojiano ambayo yangempelekea mambo matatu: kujiuzuru, kufukuzwa kazi au kupewa onyo kali.
 
ukiona watawala wamebatiza wapinzani wao kuwa magaidi, wakawafanya wananchi wanaowatwala kuwa ndodndocha, na sasa wanapambana na viongozi wa kiroho ujue kuwa mwisho wao umekaribia
 
Hhee DC mumewe mkatoliki? Vp tena "walishindwana" na meja jenerali? Maana yule si mkatoliki ati!
 
baba aliyewazaa watoto(rais) akawapa urithi(vyeo) wafanye wanavyotaka juu ya urithi waliopewa ndo kinachotokea kwa viongozi wetu,

sent from my blackberry 9780 using jamiiforums
najazia,nyama kidogo mkuu,ni katabia kawa tawala,ccm ukisema ukweli,unaitwa,unaitwa mchochezi,na kuendeleza kamchezo chao kakulitumia jeshi la polisi vibaya,kamata piga mabomu tiandani fungulia kesi ya uchochezi,haaaaaa,ukiona serikali inashindwa kazi,,,na kutumia polisi ujue imesha poteza sifa za kuwa ongoza watanzania,
 
Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki parokia ya Chumbageni, Padre James Kabosa ameponea chupuchupu kuswekwa ndani na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego kwa madai ya utovu wa nidhamu.


Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa wilaya mwenyewe, Padre Kabosa na msemaji wa Askofu, Padre Peter Kagaba walipozungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti....

Naona imekuwa ndiyo fasion mkoani Tanga. Kila DC anatishia kuweka wananchi LUPANGO!!! Hivi hii ndiyo style mpya ya DCs??? Kwamba, badala ya kutafuta chanzo cha matatizo na kuyatafutia ufumbuzi kulingana na fursa zinazo patikana katika eneo husika, kwa sasa ni mwendo wa kutupa watu LUPANGO!!!!????

Hizi ni dalili za uongozi ulio shindwa. Kwamba hapo ndio upeo wa mwisho wa kiongozi kufikiri. Mwisho wa siku ni serikali iliyo shindwa.

Nadhani hadi mwisho wa 2015 tutasikia na kuona mengi.
 
ni kukosa busara. Ningekuwa mwajiri wake ningemuita kwa mahojiano ambayo yangempelekea mambo matatu: Kujiuzuru, kufukuzwa kazi au kupewa onyo kali.

mkuu sijuhi,,,,sweet,,,wake uko home imekaaje,maana aya ni mapicha picha,yawezekana ,,,,sweet,,,wake anatafuta kituo cha haki ya kina baba wanao saidiwa kibano kama kule kenya,,,,,haaaaaaaaaaa,
 
FIKRA NGUMU;

Mahali popoote duniani ambapo kanisa limestawi jamii husika lazima iwe maskini wa kutupwaaa. Rejea kisa cha Askofu Oscar Romero wa Amerika ya kusini ambako kanisa limeshika hatamu na akaanzisha " Liberation Theology " lakini alipingwa hadi na Papa kutoka Vatican....Kanisa halikutaka jamii ile ikombolewee, Alikufa katika mazingira ya kutatanishaa sanaaa.. !

Kanisa pia halitaki jamii ya Ki Tanzania ikombolewe na Umaskini !
 
Back
Top Bottom