Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Huyu jamaa naye anamikwara sana!
====================
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Albert Msando, amesema serikali haitatoa kibali chochote cha maandamano siku ya kupiga kura, Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa siku hiyo imetengwa mahsusi kwa ajili ya wananchi kushiriki katika zoezi la uchaguzi mkuu.
Amesema hayo leo, Ijumaa Oktoba 24, 2025, katika Kongamano la Vyuo na Vyuo Vikuu lililofanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza
“Niwahakikishie kwa niaba ya serikali, kwanza msitishiwe. Wapuuzieni wanaowajaza hofu wananchi. Jiepusheni na kuwa chanzo cha ghasia ama vurugu, na zaidi niwahakikishie tutawadhibiti wale wote wanaopanga kuleta vurugu. Nisisitize, Oktoba 29 imetangazwa kuwa siku ya uchaguzi, hivyo ni marufuku kuandamana kwa kigezo cha kudai haki ya kikatiba. Hakuna haki inayovunja haki nyingine — uchaguzi ni suala la kikatiba,” amesisitiza Msando.