DC Mpogolo: Bodaboda na Machinga undeni Timu Maalum kuzunguka vijiwe vyenu kutoa elimu ya kudumisha amani

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
654
Reaction score
1,598
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka viongozi wa Maafisa Usafirishaji na Wamachinga kuunda timu maalum itakayozunguka katika vijiwe vya bodaboda na maeneo ya wafanyabiashara kutoa elimu juu ya umuhimu wa kudumisha amani.

Hayo ameyabainisha leo katika kongamano la Maafisa Usafirishaji na Wamachinga wa Wilaya ya Ilala lililofanyika katika Ukumbi wa Drimp Ilala Boma jijini Dar es Salaam, Ambapo Mpogolo amesema amani ni msingi wa maendeleo ya taifa na kila mwananchi anao wajibu wa kuitunza.

Mpogolo ameongeza kuwa bila amani hakuna shughuli yoyote ya kiuchumi inayoweza kustawi, hivyo ni muhimu viongozi hao kuendelea kuwaelimisha vijana na wafanyabiashara juu ya madhara ya vitendo vinavyoweza kuvuruga utulivu.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha ustawi wa wananchi, na juhudi hizo zitafanikiwa zaidi iwapo jamii itashirikiana kulinda amani katika maeneo yote ya jiji.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Wilaya ya Ilala Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (RPC) ACP. Yustino Mgonja ameahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa maeneo mbalimbali kuhakikisha elimu ya kujenga amani inawafikia vijana na makundi yote ya wafanyabiashara pia amesema Jeshi la Polisi litaongeza doria na mikutano ya kijamii ili kuimarisha uhusiano na wananchi.
 
Nyinyi viongozi nendeni mkasikilize changamoto za vijana nn kinawasumbua wajibikeni ipasavyo.Vijana hawana shida sema viongozi ndo mmekua na shida mpaka vijana wanaona acha kiwake..
Mtu anaona ufisadi uonevu utekaji wa hovyo ma tozo ya hovyo harafu unamwambia akahubiri amani ?
 
Amani ya kupigwa risasi?Mtajalibu mtashindwa tarehe 9 tunaingia barabarani sababu ya wapendwa wetu
 
Viongoz Wa Kisiasa Mpaka Wavyombo Vya Usalama Dhahiri Upewao Mdogo Sana Hilo Kundi Wanao Deal Nalo Nidogo Sana Haliwez Leta Hata Matokeo Chanya Kwa Mpango Wao Huo

Chakushangaza Hilo Kundi Wakat Wa Kampen Wamelitumia Sana Na Kufanya Fujo Barabaran Ila Bado Wanaamin Hao Ndy Wanzishaji Maandamano

Kingine Kama Kundi Hilo Wanalitazama Kwa Jicho Latatu Mbona Mpaka Leo Shughul Zao Wamekosa Hata Bima Ya Afya Ya Uhakika Kama Wao Wanaona Wanajal

Tanzania Mifumo Imeshagoma Kulazimisha Nikubomoa Kabisa
 
kwa malipo ya shilingi ngapi
 
Vipi safari hii hamuwapitishi polisi barabarani ili wafanye mazoezi mbali mbali ya kuimarisha ulinzi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…