JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
Mkuu wa wilaya ya mbulu mh chelestino s mofuga Leo 29/11/2018 amefanya mkutano wa hadhara kata ya Dongobesh kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua
Mkuu wa wilaya akiwa na jopo la wataalam ameweza kusikiliza kero/mashauri zaidi ya sitini(60) tangu asubuhi hadi SAA kumi na mbili,ambapo baadhi ya kero zilizojitokeza kwa wingi ni migogoro ya ardhi, familia,ndoa,utawala bora, na mapato na matumizi katika vijiji.
Mkuu wa wilaya akiongea na wananchi baada ya kusikiliza na kutatua migogoro amekemea vikali mila na desturi za kutenga watu ambazo zinapelekea kuchochea uvunjifu wa amani na wizi wa mifugo.
Aidha amehimiza viongozi wa vijiji, kata na Halmashauri kushiriki kikamilifu katika kusikiliza na kutatua kero za wananchi .