DC Makonda amkataa hakimu

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,874
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jana alitinga mahakamani na kumkataa hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi iliyofunguliwa dhidi yake na makada wawili wa zamani wa CCM wanaodai aliwakashifu.

Kesi dhidi ya Makonda, ambayo awali ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Hellen Liwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilishafikia hatua ya utetezi na Makonda alitakiwa kuanza kujitetea jana, baada ya mahakama hiyo kumuona kuwa ana kesi ya kujibu.

Hata hivyo, jana Makonda ambaye ilifika mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kesi hiyo ilipofunguliwa, alishikilia msimamo wa kutokuwa na imani na hakimu huyo na hivyo kuomba apangiwe hakimu mwingine.

Makonda alifikia msimamo huo kutokana na maneno aliyoelezwa na wakili wake, ambayo kwa mtazamo yalionyesha kuwa hakimu atakuwa anawapendelea wadai na hivyo asingemtendea haki.

Kutokana na madai ya Makonda, Hakimu Liwa amejitoa kwenye kesi hiyo na amepanga ianze kusikiliza upande wa mashtaka Machi 23.

Chanzo: Mwananchi On Line
 
Haaa haaa anakuja Mahakamani kwa mara ya kwanza na kumkataa hakimu ni haki yake lakini
 
Sasa hii kesi itakuwa imefikia mahali pa kufurahisha sana. Kama nakumbuka vizuri makada waliofungua ni Guninita na Bashe wakilalamikia Lowassa kudhalilishwa. Sasa hivi Bashe na Makonda wako CCM, Guninita na Lowassa wako CHADEMA!
 
Kwa maana hiyo siku hizi huduma za kijamii na za kiserikali tuzipate kutokana na ukanda au undugu?
Hawa watu hawakwepeki kila sehemu wamo. Serikalini wamo, vyama vya siasa vyote wamo, biashara wamo, kilimo, NGOs mpaka ujambazi huwakosi. Walishakuwa na head start na hii imewapa advantage over makabila mengine. Hawa huwa na tabia ya kunyanyuana na wenyewe kwa wenyewe wana ushindani sana wa maendeleo.
 
Wenzetu wanajali elimu,hakuna miujiza mkuu,,, ni elimu tu ndo inayosababisha kuwamo katika kila sekta hao uwasemao,na kingine wana machungu na maendeleo mno
 
Back
Top Bottom