DC Kiteto kuanza ziara kuongea na wananchi

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, Mhandisi Tumain Magesa, anakusudia kuanza ziara kuongea na wananchi vijijini.

Akizungumza hayo Mhandisi Magessa amesema, maeneo atakayofika ni Kata ya Ndirigishi ambayo inachangamoto ya migogoro ya ardhi.

Alisema Kiteto kwa ujumla imekuwa shwari tofauti na miaka mitatu iliyopita kutokana na uhasama wa wakulima na wafugaji

Alisema wakati huu wakulima wako katika maandalizi ya Kilimo hivyo kuna kila sababu ya kila MTU kuwa na uhakika kuwa atalima wapi ambapo hatokuwa na mgogoro

Kazi yetu viongozi ni kuzuia tatizo lisitokee sio kusubiri litokee ndio tujitokeze kulitatua, alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Kiteto

Alisema miongoni mwa maagizo atakayowaambia wananchi hao ni pamoja na kuwataka waheshimu mipango yao ya matumizi bora ya adhi waliyojipangia

Sitegemei kuona mkulima akilima eneo la malisho halikadhalika mfugaji kuchunga eneo la Kilimo hapa sitokubaliana na hali hii.

Pia wale wanaoingia Hifadhi ya Emboley Murtangos Kinyemela waondoke nimeagiza vyombo vyangu wakikutwa humo hatua kali zitawathibitikia, alisema DC Magessa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani siye ni wananchi wa kiteto..??? Mmnyuuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom