Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 879
- 969

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi Leo asubuhi amekabidhi Vifaa mbalimbali vya hospitali kwa uongozi wa hospitali ya Ocean Road vilivyotolewa na jumuiya ya KIBOSHO Girls ALUMNI.
Wanafunzi hawa wa zamani waliosoma Shule ya Sekondari ya wasichana Kibosho wamejitolea vifaa mbalimbali vya wagonjwa kama vile vyandarua vinavyotosha Vitanda Vyote Hospitalini hapo, Sabuni, Miswaki, Dawa za Meno, baiskeli za wagonjwa, vipimajoto, mashine za kupima presha na vifaa vingine.
Wana Alumni hawa wamewaomba Watanzania na Wanafunzi wengi wa zamani wa shule mbalimbali waliosomeshwa na taifa nao waige mfano huu nakusaidia jamii kwa namna moja ama Nyingine.
Kwa Upande Wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni amewapongeza sana kwa Jitihada zao
na kuwahakikishia ushirikiano kwa kila jambo la kimaendeleo ili kuijenga nchi.
Aidha, Mh. Hapi ametoa wito kwa wadau mbalimbali, mashirika binafsi na ya umma kuona umuhimu wa kusaidia sehemu ya mafanikio yao kwa jamii yenye uhitaji.
Amewaomba Wadau wasichoke kusaidia Maendeleo ya Kinondoni na taifa kwa ujumla, kwani wanao wajibu wa kutoa mchango wao katika ujenzi wa taifa.
