Mhe. Ndumbaro Akabidhi Vifaa Tiba Hospitali ya Rufaa Songea

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,756
1,261

MHE. NDUMBARO AKABIDHI VIFAA TIBA HOSPITALI YA RUFAA SONGEA

Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekabidhi vifaa tiba vya huduma ya utengemao kwa uongozi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, iliyopo Manispaa ya Songea mjini.

Mhe. Ndumbaro amekabidhi vifaa hivyo Desemba 28, 2024, kufuatia changamoto ya muda mrefu katika Kitengo cha “Physiotherapy” ya upungufu wa vifaa hivyo kulinganisha na idadi ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mhe. Ndumbaro amesema kuwa, ni adhma ya Serikali kupitia mfuko wa kuchochea maendeleo jimboni kupambana na changamoto mbalimbali ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Naye, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Majura amesema kuwa vifaa tiba hivyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza muda wa wagonjwa kukaa hospitalini ambapo idadi ya wagonjwa kutibiwa kwa muda itaongezeka.

Uongozi wa hospitali hiyo, umeahidi kutunza vifaa hivyo ili kuleta tija iliyokusudiwa kwa jamii.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.05.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.05.jpeg
    504.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.47.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.47.jpeg
    494.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.47 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.47 (1).jpeg
    502.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.48.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.48.jpeg
    610.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.48 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.48 (1).jpeg
    426.8 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.49.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.49.jpeg
    617.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.49 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 17.37.49 (1).jpeg
    404.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom