DC Kinondoni aagiza wanaoishi mabondeni kupewa makazi mapya

WEKKI

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
477
145
DC HAPI ATOA MASAA 8 KUHAKIKISHA WALIO KTK HATARI YA MAAFA YA MAPOROMOKO UKWAMANI WANAPATIWA MAHALA PAKUISHI.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Salum Hapi leo ikiwa siku yake ya 6 tangu Kuteuliwa na Rais, lakini pia ni siku ya Pili (2) Tangu Kuapishwa kwake.

Mkuu wa Wilaya ametembelea eneo la Kawe Ukwamani ambalo ni Hatarishi sana kwa Kuwa na Bonde la maporomoko ambalo Siku Chache zilizopita kuna Udongo ulikatika nakuponda Nyumba ambayo Ndani kulikuwa na Watu Watano ambao walipoteza Uhai wao.

DC wa Kinondoni Mh Ally Salum Hapi akiwa ameambatana na watendani wa manispaa ya Kinondoni akiwamo Injinia wa Manispaa, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, Mkuu wa Police (OCD Kawe) wa Kinondoni na Maafisa wengine. Majira ya Saa Tano aliwasili Kawe ukwamani kufanya ukaguzi wa eneo la Maafa.

Mkuu wa wilaya alipofika eneo hilo alishtushwa na mazingira yale ambapo Wakazi wa maeneo hayo wanaishi na Vifusi vikiwa vinaning'inia pembeni ya Nyumba zao jambo ambalo ni hatarishi sana kwa Uhai wa maisha yao ukizingatia kuna watu 5 walopoteza maisha siku chache zilizopita.

DC Hapi Ametoa Masaa 8 kwa Watendani wa Mtaa, Kata, Injinia wa Manispaa na Ofisi ya Mkurugenzi Kuhakikisha Ifikapo Saa mbili usiku wawe wamewapatia Mahala pakulala wakazi wanaoishi katika Eneo hilo Hatarishi.

DC amewaagiza Watendaji Kuhakikisha Waliopo katika Eneo hilo Hatarishi wanaondolewa Mara Moja Leo wasilale pale kwani ni Hatari sana hasa kipindi hiki ambacho kuna Mvua zinaendelea Jijini Dar es salaam.

Amewambia wahakikishe Wanakaa na Wananchi hao kuhakikisha wanapata Mahala Pakulala, Mwisho Saa Mbili usiku wa leo wampatie Taarifa ya Utekelezaji wa Maagizo hayo na yeye atakuwa ofisini kwake kungoja taarifa hiyo.

"Sisi watendaji tulopewa dhamana hatuwezi kukaa kimya bila kuchukua hatua huku wananchi wetu wako ktk Hatari kubwa ya maafa, na wapa Muda ifikapo saa mbili usiku nipate Taarifa ya hatua mlizokubaliana na utekelezaji wake, mkishindwa kufanya hivo mtawajibika"

Alisema DC Hapi.

DC amesema Kama Watafeli katika hilo basi Adhabu stahiki zitachukuliwa Dhidi yao.

Mkuu wa Wilaya Huyu ambae amekuja baada RC Paul C. Makonda inaonekana kuwa atakuwa na Speed Kali kama ya Boss wake alomtangulia ambae leo hii ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
 
kwani DSM ina mito mingapi?

na mabonde mangapi?

maana hii generalization ya majukwaa ya siasa itafanya maeneo yenye muinuko kama Pugu,Kinyerezi,Kifuru,Goba,Mbezi louis,Maramba mawili. yaonekane ni bondeni

Pasco Manyerere Jackton Informer
 
jamani jamani hii spidi hatari, njoo taratibu mkuu wa wilaya tutafika tu! Mwisho saa Mbili usiku? utatia watu presha mkuu!
 
Back
Top Bottom