Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,564
- 21,586
Mkuu wa wilaya ya Karagwe iliyoko mkoani Kagera Mhandisi Richard Ruyango ameliagiza jeshi la polisi kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani viongozi wa kata Ngenge ambao ni pamoja na diwani wa kata hiyo Ezekiel Kaganda, Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Binoni Josephat Shimikile na mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kishuro Julius Domician ambao kwa pamoja wanakabiliwa na tuhuma ya kuuza kinyemela ardhi ya kijiji hicho kwa raia toka nchi jirani wanaoingia hapa nchini na mifugo yao ambayo imekuwa ikifanya uharibifu mkubwa wa mazao kwenye mashamba ya wakulima.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo alipofanya ziara katika kijiji cha Kishuro baada ya kusikiliza kero za wananchi ambao wameonyesha kutoridhishwa na uongozi wa serikali ya kijiji hicho ambao umerushiwa tuhuma nyingi ambazo ni pamoja na ubadhilifu wa mali za kijiji na kupokea mifugo iliyoondolewa kwenye hifadhi ya misitu na mapori ya akiba kufuatia operesheni iliyoendeshwa mkoani kagera hivi karibuni ambayo baadhi yao wananchi wameikamata.
Mkuu huyo wa wilaya pia amestushwa na hatua ya mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Binoni ya kuanzisha kinyemela kijiji cha Rukindo kwa ajili ya makazi ya raia toka nchi jirani ya Rwanda ambacho hakina usajili.
Kwa upande wao viongozi waliotuhumiwa wamekana tuhuma zilizoelekezwa kwao na wananchi, naye mkuu wa jeshi la polisi wa wilaya ya Muleba, Lazaro Mwanyasi ameahidi kuwachukulia hatua viongozi watakaowanyanyasa wananchi walioeleza kero za viongozi wao mbele ya mkuu wa wilaya.
Chanzo: ITV