DC Iringa: Marufuku Mikutano ya siasa kwenye Wilaya yangu mpaka mwaka 2020

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,863
image.jpeg

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, amesema kamati ya ulinzi na usalama haitaruhusu mikutano ya hadhara itakayoombwa na vyama vya siasa wilayani humo.

Pamoja na uamuzi huo, Kasesela amesema kamati hiyo itawasaka na kuwafikisha katika vyombo vya dola watu wanaomkashifu Rais Dk. John Magufuli na viongozi wengine wa Serikali.

“Tuendelee na majukwaa ya utendaji, mipasho ya siasa tupumzike ili tuiache Serikali ifanye kazi zake,” alisema.

Alisema uchaguzi mkuu mwaka jana umepita kwa kumpata Rais, wabunge na madiwani, hakuna sababu tena ya kuendelea na mikutano ya kisiasa kila kukicha.

“Kama tunataka mbwembwe za siasa majukwaani, tusubiri uchaguzi wa Serikali za Mitaa au uchaguzi mkuu wa 2020,” alisema.

Alisema hatakuwa na msalia mtume na mtu yeyote awe mwana Chadema au CCM, atakayethubutu kunyanyua mdomo na kumtusi kiongozi yeyote au mwanachama mwenzeke, atakula naye sahani moja ili kuheshimiana na kutii mamlaka zilizo madarakani.

Wakati huo huo, amewataka viongozi wa taasisi mbalimbali za dini ambazo hakuzitaja kumaliza migogoro yao ya uongozi inayoelekea kuhatarisha amani ya wilaya.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdala, ameahidi kuzishughulikia changamoto mbalimbali za kimaendeleo wilayani humo.

Chanzo: Mtanzania.

Note: Huyu ndio DC aliyesifika kwa kurusha picha mitandaoni kwa kila tukio alilolifanya, mpaka wakati wa kula kiapo cha uadilifu Ikulu Rais akasema ameamuwa kumpa U-DC baada ya kuona anasemwa sana na picha zake zinakejeliwa mitandaoni.Akaona ampe huyohuyo anayesemwa semwa sana.
 
View attachment 364196

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, amesema kamati ya ulinzi na usalama haitaruhusu mikutano ya hadhara itakayoombwa na vyama vya siasa wilayani humo.

Pamoja na uamuzi huo, Kasesela amesema kamati hiyo itawasaka na kuwafikisha katika vyombo vya dola watu wanaomkashifu Rais Dk. John Magufuli na viongozi wengine wa Serikali.

“Tuendelee na majukwaa ya utendaji, mipasho ya siasa tupumzike ili tuiache Serikali ifanye kazi zake,” alisema.

Alisema uchaguzi mkuu mwaka jana umepita kwa kumpata Rais, wabunge na madiwani, hakuna sababu tena ya kuendelea na mikutano ya kisiasa kila kukicha.

“Kama tunataka mbwembwe za siasa majukwaani, tusubiri uchaguzi wa Serikali za Mitaa au uchaguzi mkuu wa 2020,” alisema.

Alisema hatakuwa na msalia mtume na mtu yeyote awe mwana Chadema au CCM, atakayethubutu kunyanyua mdomo na kumtusi kiongozi yeyote au mwanachama mwenzeke, atakula naye sahani moja ili kuheshimiana na kutii mamlaka zilizo madarakani.

Wakati huo huo, amewataka viongozi wa taasisi mbalimbali za dini ambazo hakuzitaja kumaliza migogoro yao ya uongozi inayoelekea kuhatarisha amani ya wilaya.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdala, ameahidi kuzishughulikia changamoto mbalimbali za kimaendeleo wilayani humo.

Chanzo Mtanzania.
Note: Huyu ndio DC aliyesifika kwa kurusha picha mitandaoni kwa kila tukio alilolifanya,Mpaka wakati wa kula kiapo cha Uadilifu Ikulu Rais akasema ameamuwa kumpa U-DC baada ya kuona anasemwa sana na picha zake zinakejeliwa mitandaoni..Akaona ampe huyohuyo anayesemwa semwa sana!!

Hongera domokarasia ya ccm! Mnatisha!
 
2015-2020 kitakuwa kipindi cha majanga na mambo kwenda hovyo haijapata kutokea tangia Uhuru. Kama tunaiga Rwanda tunakosea maana Rwanda wao wanayo style yao ya kujieleza pale wasipokubaliana na serikali, nayo ni kuwa msituni na kufanya sabotage.
Sina hakika kama hilo tumejiuliza kabla ya kuiga.
 
Kuna haya yakuwatoa madarakani kabisa 2020, si mlaumu kiongozi najilaumu mpiga kura.
 
Wanavyozuia demokrasia namna hii siku moja kuna watu watakamata dola na kukifutilia mbali chama chao, What goes around comes around!
 
Hili tangazo naona litasaidia kuiondoa CCM 2020 maana tutakuwa tunasikiliza habari mpya kila siku. Maana tukianza kuzisikia sasa watapata muda wa kujitetea.
 
Dah..juzi wakati wa uteuzi wa ma dc nilimsikia jpm akimpongeza huyu jamaa kwa kazi anazofanya...nategemea anaweza kumpongeza tena kwa tamko hili...
Namshauri jpm afute vyama vyote vya upinzani kama ndivyo vinarudisha maendeleo nyuma mpaka 2020
.. na viwanda visipojengwa ccm ijifute yenyewe na kuwapa wapinzani nchi..

Maana hizi akili sijui wanaziokotea wapi...yaani unazuia mikutano ya kisiasa iliyo halali kikatiba tena kwa nchi ya vyama vingi tena tena eti yenye demokrasia...??
 
....jengo linaungua na mtu anafanya kazi ya kusaidia kuzima moto, cha kushangaza ni idadi ya picha zilizopigwa na jinsi zilivyopigwa.

Unajiuliza mpiga picha alijiandaa saa ngapi na inakuwaje anamchukua mtu mmoja tu kwenye tukio.

Umaarufu wa kutafuta kwa nguvu yote hiyo; wanaweza kushikilia hiyo sheria ya kutofanya mikutano na hiyo 2020 kukawa na tume huru ya uchaguzi (kama umemsikia Jaji Lubuva) ambayo itatoa matokeo kama yalivyo na sio kama 'itakavyoletewa' kama uchaguzi uliopita.

Na hapo hiyo sheria ita-apply kwake kwa staili ya 'nyuma geuka' ndio atajua machungu yake. Unadhani miaka mitano ni mbali!!
 
enzi za Chama Kimoja mwalimu akukataza mikutano ya kisiasa sembuse huyu magufuli na serikali yake,
ni uchanga wa kisiasa tu unawasumbua ndio maana hata kuteua hawajua
amejaza MA PHD na Professar ikulu akijua ndio mambo yatakwenda vizuri kumbe sio
katibu mkuu kiongozi ana miaka 61 kisa ni rafiki yake mhandisi kijazi
katibu mkuu tamisemi mhandisi iyombe
jaani hopeless kabisa wao wanadhani mikutano ya siasa ndio chanzo cha sukari kuuzwa elfu 4 (4000) mpaka elfu 6000
shame on you Magu
 
Back
Top Bottom