DC Iringa ampa masaa Diwani wa CHADEMA kuomba radhi kwa kusema Mwenge unatakiwa kupumzishwa

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,315
38,454
Diwani wa Kata ya Kitwiru- Iringa, Baraka Kimata-Chadema asema ikiwa chama chake kitachukua nchi watauhifadhi mwenge huo makumbusho ya taifa.
IMG_20170427_111339.jpg

Diwani wa CHADEMA Kata ya Kitwiru katika Manispaa ya Iringa Ndugu. Baraka Kimata, alishikiliwa kwa muda na Jeshi la Polisi baada ya kutoa maneno yaliyotafsiriwa kwamba ni kashifa kwa mbio za Mwenge. Kimata ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHADEMA Iringa Manispaa aliitwa Jukwaani kuongea kwa niaba ya chama chake baada ya Katibu wa CCM wilaya kuongea.

Kimata pamoja na mambo mengine aliyoongea, alimalizia hotuba yake kwa kusema kwamba kama CHADEMA ikipewa ridhaa ya kuongoza nchi basi wataupumzisha Mwenge wa Taifa. Baada ya hapo wasemaji wote waliofuatia akiwamo Mkuu wa Wilaya ya Iringa na Mkimbiza Mwenge Kitaifa walimshambulia Kimata na chama chake kwa msimamo huo wa kupinga Mbio za Mwenge.
photo.jpg

Diwani wa Kata ya Kitwiru- Iringa, Baraka Kimata-CHADEMA

Baadaye Kimata alikamatwa na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kuhojiwa na kuachiwa. Habari toka kwa watu walio karibu naye wanadai kwamba Kimata ametakiwa kuandika barua ya kuomba radhi kabla ya kesho saa kumi jioni.

Mwendelezo
Diwani Kimata ameandika barua kuelezea ni kwa nini alitoa yale maneno kwamba kama CHADEMA ikishika Madaraka ingeupumzisha Mwenge. Barua hiyo aliikabidhi Polisi!
 
Wakati wenzetu wanaendelea na mauvumbuzi ya teknolojia na wanaonesha mikwara imara kabisa ya kutikisa Dunia, sisi tuko busy na kutembeza Mwenge kwa wananchi kwa kutumia kodi hizohizo za wananchi, jambo ambalo halina hata chembe ya faida labda tukiuweka kwenye sehemu za makumbusho tunaweza kupata japo senti chache kama kivutio cha utalii.

Ajabu sana, unawapelekea wananchi mwenge wauone huku haohao wananchi hawana maji safi, huduma za afya mbovu(kwa sehemu zilizopo) sehemu zingine hamna hata zahanati, umeme bado shida, elimu (walimu hamna kwenye shule za kata). Hayo mabilioni yangetumika kulipa walimu ingekuwa jambo la maana sana kuliko kwenda kuunadi kwa watu ambao wanamatatizo kibao yanayohitaji kutatuliwa na hizo pesa zinazotumika kwenye mbio( mbio za mende huishia sakafuni)

Hongera kwa Diwani kwa kusema ukweli, maana wapo wengi na Taaluma zao lakini wanashindwa kusema ukweli huku wakijua wanachokisema sio kilichopo kwenye mioyo yao bali tu ni kusaka tonge
 
FB_IMG_1493260613511.jpg


Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ampa masaa diwani wa kata ya Kitwiru, Baraka Kimata (CHADEMA) kuomba radhi mara baada ya kutoa kauli jukwaani wakati akitoa salamu za Mwenge, kuwa wakipewa ridhaa wao wataupumzisha Mwenge huo kwenye makumbusho.

Toa maoni yako.

Chanzo: EATV
 
Back
Top Bottom