DC Hapi kunguruma Clouds Tv 360 Live kesho asubuhi

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
DC HAPI KUUNGURUMA CLOUDS TV 360 LIVE KESHO ASUBUHI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi anatarajiwa kuwa live katika kipindi cha Clouds TV cha 360 kesho alkhamisi tarehe 26/5/2016 kuanzia saa 2 asubuhi na kuendelea akizungumzia masuala muhimu ya maendeleo ya Kinondoni ikiwemo mipango mbalimbali ya kiuchumi, afya na elimu, utatuzi wa kero za wananchi wa wilaya ya Kinondoni n.k.

Ewe mtanzania na mwana Kinondoni unaombwa kuwa karibu ya TV yako kufuatilia ili kujua ni nini kitazungumzwa na mkuu wetu wa Wilaya Mh. Hapi.
Pamoja Tujenge Kinondoni yetu na DC HAPI.
 
Back
Top Bottom