Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni leo amefunga mashindano ya vikosi mbalimbali vya JWTZ Brigedi ya Mashariki Lugalo jijini Dar es salaam.
Hii ni kufuatia mualiko wa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha mashindano hayo yaliypfanyika uwanja wa jeshi Lugalo jijini Dar es salaam.
Akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Brigedi ya Mashariki (Chui) Brigedia Jenerali S.S. Othman alimueleza mgeni rasmi kuwa Jeshi la wananchi wa Tanzania limekua na utaratibu wa kushiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi, hivyo mashindano hayo ni sehemu ya maandalizi hayo.
Akizungumza na Maafisa, askari na washiriki wote, Hapi alisema Tanzania imepata heshima kubwa kutokana na jeshi letu kushiriki mashindano mbalimbali kama Olympic na yale ya Afrika Mashariki. Ushiriki huo hauna budi kuendelezwa, alisema Mh. Hapi.
Mkuu huyo wa wilaya alimshukuru Mkuu wa Brigedi kwa heshima kubwa aliyompa kumualika kufunga Mashindano yao.