DC Hapi apokea msaada wa madawati toka kwa NSSF Kinondoni

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
718a22f6a1ea959ec70a8d37f833e279.jpg

7b29f9a75e194f3b58b784080ecc834d.jpg

DC Hapi Apokea Msaada wa Madawati 10 toka kwa NSSF Kinondoni.

DC atoa Wito kwa Makampuni, Mashirika, Watu Binafsi na Kila Kada Kuhakikisha wanatoa Msaada au kusaidia Serikali hasa Wilaya ya Kinondoni.

DC kawaomba, Wabunge, Wastaafu, Wabunge ambao wanatoka Mikoani wakija Dar huishi Kinondoni basi Waisaidie Kinondoni.

Ametoa Wito kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kusaidia Zaidi na Zaidi Kwani Dawati Kumi Zimepunguza Kero ya upungufu lakini Bado kunauhitaji mkubwa wa Dawati Kinondoni.
9cfa8fa586037ed87d39718d277cd769.jpg
 
Mh DC Ally Salum Hapi Apokea Msaada wa Madawati 10 toka kwa NSSF Kinondoni.

Kinondoni ina zaidi ya Wanafunzi 169,388, kuna Shule Za Msingi 148 za Serikali, Kinondoni kuna Idadi ya waalimu zaidi ya 4,788

Kati ya Shule hizo Shule 67 ni za Serikali,
Baada ya Agizo la Mh Rais Kufuta Ada kwa shule za msingi mpaka sekondari kuna changamoto nyingi sana zilijitokeza.

Watoto wengi sana waliandikishwa Mashuleni nakusababisha Upungufu wa Madarasa, Madawati, matundu ya Vyoo nk...

Basi kutokana na hizo changamoto Jitihada nyingi zinaendelea, Mh DC atoa Wito kwa Makampuni, Mashirika, Watu Binafsi na Kila Kada Kuhakikisha wanatoa Msaada au kusaidia Serikali hasa Wilaya ya Kinondoni.

Mh DC kawaomba, Wabunge, Wastaafu, Wabunge ambao wanatoka Mikoani wakija Dar huishi Kinondoni basi Waisaidie Kinondoni.

Ametoa Wito kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kusaidia Zaidi na Zaidi Kwani Dawati Kumi Zimepunguza Kero ya upungufu lakini Bado kunauhitaji mkubwa wa Dawati Kinondoni.
 

Attachments

  • 1463740048371.jpg
    1463740048371.jpg
    59.3 KB · Views: 56
  • 1463740095234.jpg
    1463740095234.jpg
    48.7 KB · Views: 63
Dawati kumi? Wamemdharau....anyway kuna cha kujifunza,kila taasisi ina bajeti ya mambo yake,huwezi kuwavamia tu ukachukua hela,la pili ni hili la kiongozi mmoja wa serikali kuomba pesa kwenye taasisi nyingine serikalini humo humo!! Kwa nini serikali isipange bajeti ya madawati ambayo nchi nzima ni tsh bilioni 150?! Hivi serikali inapangaje bajeti mpaka taasisi nyingine kama bunge linapata ziada ya bilioni sita!!! Mimi nafikiri bwana hapi asingepewa hata dawati moja kwa kuwa halmashauri ya kinondoni ina bajeti
 
DC aende msitu wa Mwabepande akapasue mbao za madawati ili ile dhana ya uongozi ilete mantiki sio kuvaa gwanda za mgambo tu
 
Madawati 10

Inashangaza sana ukirejea wale wabunge walichangiwa millions kwaajili ya kujipongeza kule Dodoma, ninamashaka na mentality za baadhi ya viongozi wa mashirika ya umma
 
Hata Headmaster mwenye majukumu sidhani kama anaweza kuacha ratiba zake sababu ya makabidhiano ya dawati kumi.

I think monitor wa darasa ndiye mtu sahihi kwa hizo 10 desks.
 
Heheh madawati kumi mnaita press conference na mkuu wa wilaya juu,wangeyapeleka tu shuleni wakaendelea na shuhuli nyengine,hata saccos ya hapa mtaani imewashinda NSSF
 
Its real not fear, nssf dawati 10? Mtu binafsi atapeleka ngapi ili naye afanye press na waandishi wa habari? Au waandishi wamepotosha badala ya kuandika dawati 100 wao wakaandika 10?
 
dawati 10,? nccf? huenda mtoa taarifa atakuwa amekosea may b kuongeza 0, ila kama ni kweli kuna hidden agenda ambayo nccf walitaka/wameifanya ili kumkeep buzy DC then wao wapite... achunguze
dawat 10x50000=500,000/= laki tano kwa nccf, eboooooooooooo.!
 
Sijasikia mbunge yeyote wa CHADEMA akichangia madawati ina maana kwenye majimbo yao hamna shida ya madawati shule yeyote?
 
Back
Top Bottom