Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,286
- 10,831
MKUU wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri, ameagiza kukamatwa kwa walimu watakaobainika kuwafanyia vitendo vya kikatili wanafunzi ikiwa hatua ya kukomesha vitendo hivyo vinavyoendelea nchini.
Msafiri alisema hayo jana mjini hapa wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili ulipofika mkoani Njombe kwa ajili ya kutoa elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Alisema serikali haipingi adhabu ya viboko lakini si kutoa adhabu hiyo kupitiliza na kusababisha ulemavu na maumivu kwa wanafunzi.
Mkuu huyo wa wilaya alisema suala la ukatili wa kijinsia ni mapambano makubwa nchini, hivyo jitihada zinahitajika kwa wananchi, wadau na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha wanaunganisha nguvu ili kuondokana na vitendo hivyo.
Alivitaka vyombo vya usalama kuacha kufanya ukatili kwa kuchelewesha kesi za vitendo vya unyanyasaji na kusababisha ukatili wa kihisia kwa waathirika wa matukio hayo.
“Vyombo vya usalama mnachelewesha kesi kwa sababu mnaomba rushwa. Nawaomba msiwe kikwazo cha kupatikana kwa haki ya wahanga (waathirika) wa vitendo vya ukatili,” alisema.
Akizungumza kuhusu msaada wa kisheria unaotolewa na Shirika la Legal Serivces Facility, Joseph Magazi alisema wameweka nguvu katika kuisaidia jamii katika matatizo ya kisheria kwa kuwawezesha wasaidizi wa kisheria katika mikoa na wilaya kutoa elimu husika.
"Tumejipanga kushirikiana na serikali katika kuhakikisha tunaifikia jamii katika kutoa elimu itakayowezesha wenye matatizo mbalimbali ya kisheria kupata msaada na kuyatatua matatizo yao," alisema