Dc anusurika kichapo Kilwa

ELFU-ONEIR

Senior Member
Jun 27, 2012
181
64
Kati hali ya kutaka kuhamasisha waislam kushiriki sensa mkuu wa wilaya alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuhamasisha sensa na kukataa kujibu maswali. Shukrani kwa polisi walio kuwepo eneo hilo kwa kuokoa maisha yake

source: Habari za mitaa: Sensa yamtokea puani mkuu wa wilaya ya kilwa;
 
kati hali ya kutaka kuhamasisha waislam kushiriki sensa mkuu wa wilaya alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuhamasisha sensa na kukataa kujibu maswali. Shukrani kwa polisi walio kuwepo eneo hilo kwa kuokoa maisha yakesource: habari za mitaa: Sensa yamtokea puani mkuu wa wilaya ya kilwa;
we acha uwongo wewe huo ni uzushi na hadithi za kutunga..mimi nilikuwepo hakunakitu kama hicho hata kidogo..acha kupotosha watu. Tafuta uzushi mwingine na sio huo ...naona mnaelekea kushindwa na kina shekhe ponda
 
Kuna watu kazi yao ni kuigeuza kweli kuwa urongo km alivo huyu alieleta hii thred.
 
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Mh Abdallah Ulega amenusurika kipigo kikali toka kwa waumini wa dini ya kiislam baada ya kuwahamasisha kushiriki katika zoezi la sensa. Mkuu huyo wa wilaya yamemkuta hayo alipopewa kipaza sauti awasalimie waislam baada ya kumalizika kwa ibada ya swala la idi-fitri katika msikiti wa Azhaar uliopo kilwa kivinje. Mheshmiwa badala ya kutoa salam za idi,akaanza kuwahamasisha waislam kushiriki zoezi la sensa. Hata hivyo waumini walipotaka kumuuliza maswali mheshmiwa hakuwa tayari ndipo waumini walipoamua kumvamia kwa lengo la kumpa kipigo. Hata hivyo polisi na usalama wa taifa ilibidi waingilie kati kumnusuru na kipigo,

Akiongea baadae katika Baraza la idi,bw Ulega alisema hivi sasa sitazungumzia swala la sensa kwakuwa sitaki kuwakwaza tena waislam. Mheshmiwa aliwataka waislam kujitokeza kwa wingi katika ukusanyaji wa maoni kwa ajili ya katiba mpya pindi tume itakapowatembelea.

Waislam Tanzania wakiwakilishwa na taasisi zao zote ikiwemo Bakwata chini ya Mufti Simba walikubaliana kugomea zoezi la sensa hadi kipengele cha dini kitakapoingizwa katika dodoso la maswali yanayohusiana na zoezi hilo. Madai hayo waislam yametokana na baadhi ya taasisi za serikali na kidini(Kanisa Katoliki) kutoa takwimu za idadi ya watanzania kilingana na dini zao.

Hata hivyo siku chache Bakwata walijitoa katika kundi hilo la waislam na sasa inashirikiana na serikali katika kuwahamasisha waislam kushiriki katika zoezi la sensa.

we acha uwongo wewe huo ni uzushi na hadithi za kutunga..mimi nilikuwepo hakunakitu kama hicho hata kidogo..acha kupotosha watu. Tafuta uzushi mwingine na sio huo ...naona mnaelekea kushindwa na kina shekhe ponda
Sasa si unaeleza kwanza kilichotokea then ndio uzengumzie uzushi unaotaka.
 
Bila shaka heading iltakiwa kuwa ...wasiounga... badala ya ...wanaounga...
 
hivi serikali inaona aibu gani kuahirisa sensa maana haitafanyika hii kitu ..au ndo wameshakula cha juu sasa hesabu hazita balance
 
Hapa ndo unapomisi mijitu kama beni mukapi na Yedu Luwasi. Wakati mwingine demokrasia ikizidi inakuwa kero. Demokrasia ya kugomea sensa!!???.
 
[h=6]

Mkuu wa wilaya ya Kilwa Mh Abdallah Ulega amenusurika kipigo kikali toka kwa waumini wa dini ya kiislam baada ya kuwahamasisha kushiriki katika zoezi la sensa. Mkuu huyo wa wilaya yamemkuta hayo alipopewa kipaza sauti awasalimie waislam baada ya kumalizika kwa ibada ya swala la idi-fitri katika msikiti wa Azhaar uliopo kilwa kivinje. Mheshmiwa badala ya kutoa salam za idi,akaanza kuwahamasisha waislam kushiriki zoezi la sensa. Hata hivyo waumini walipotaka kumuuliza maswali mheshmiwa hakuwa tayari ndipo waumini walipoamua kumvamia kwa lengo la kumpa kipigo. Hata hivyo polisi na usalama wa taifa ilibidi waingilie kati kumnusuru na kipigo,

Akiongea baadae katika Baraza la idi,bw Ulega alisema hivi sasa sitazungumzia swala la sensa kwakuwa sitaki kuwakwaza tena waislam. Mheshmiwa aliwataka waislam kujitokeza kwa wingi katika ukusanyaji wa maoni kwa ajili ya katiba mpya pindi tume itakapowatembelea.

Waislam Tanzania wakiwakilishwa na taasisi zao zote ikiwemo Bakwata chini ya Mufti Simba walikubaliana kugomea zoezi la sensa hadi kipengele cha dini kitakapoingizwa katika dodoso la maswali yanayohusiana na zoezi hilo. Madai hayo waislam yametokana na baadhi ya taasisi za serikali na kidini(Kanisa Katoliki) kutoa takwimu za idadi ya watanzania kilingana na dini zao.

Hata hivyo siku chache Bakwata walijitoa katika kundi hilo la waislam na sasa inashirikiana na serikali katika kuwahamasisha waislam kushiriki katika zoezi la sensa.
[/h]

Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro kimefungua branch/kampasi ngapi tangu kuanzishwa kwa msaada wa serikali ya awamu ya tatu?
 
Usikaririr mkuu, Kufungua branch nyingi sio sifa ya chuo bora, hatufanyi mambo kwa kuiga, tuna vipaombele vyetu kwa manufaa yetu.
 
Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro kimefungua branch/kampasi ngapi tangu kuanzishwa kwa msaada wa serikali ya awamu ya tatu?

ha ha haaa!!! hata ROMA haikujengwa kwa siku moja, ngoja na sie tutengeneze MOU pale ikulu, kampasi na ma-vyuo mbona vitachipua kama uyoga??? hivi wewe kwa akili yako, umeona waislamu ni mambumbu kiasi hicho, ianwezekana hawana utitiri wa taasisi kama dini zingine, lakini haimaanishi kuwa ni mambumbu, au unasahau kuwa ndo waliokuwa mstari wa mbele hata kwenye kudai uhuru wa hii nchi??? p'se DO NOT UNDERESITMATE MUSLIMS, DO NOT, DO NOT DO NOT P'SE.
 
Back
Top Bottom